Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  1 Rabi' I 1442 Na: 1442 H / 05
M.  Jumapili, 18 Oktoba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Usekula Umefeli Wakati Ambapo Uislamu Utafaulu

Siku nyingine shambulizi jengine dhidi ya Uislamu na Waislamu. Kilichokuwa kikiachiwa vyombo vya habari sasa kinazidi kuchukuliwa na wanasiasa. Vyombo vya habari havikuweza kuwatishia watu na Uislamu vya kutosha, na hawavikujaribu hata kuweka hoja ya kifikra kwa usekula wao au dhidi ya Uislamu; sasa ni zamu ya wanasiasa kuleta ubabaishaji kutokana na kushindwa kwao kwa jumla kuwaangalia watu, wasije wakageukia Uislamu katika kutafuta kwao badali ya uongozi mbaya wa kirasilimali.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatamani siku tukufu za ukoloni, wakati Waislamu walipojua mahali pao (chini ya udhibiti wa Magharibi) na kukubali kiholela kutawaliwa na mabwana wao wa kikoloni. Anazitamani siku hizo na analalamikia Mapinduzi ya Kiarabu ambayo Waislamu walianza kuwakataa wakoloni na kudai uhuru wao. Anahitimisha kuwa Uislamu lazima uwe katika mgogoro, ikiwa unawaongoza walio koloniwa kukataa udhibiti wa mkoloni msekula! Anasahau kuwa Algeria pia ilikataa ukoloni wa Ufaransa na ukatili wake na njia zisizo za kibinadamu za mateso na kutiisha. Anasahau kuwa Ufaransa iliitumia Algeria kama jaa la taka za nyuklia, na hadi leo anakataa kufichua maeneo ya siri ya taka zao za mionzi. Anasahau kwamba mtu yeyote aliye na uoni wa wazi anaweza kuona kupitia madai ya uongo ya usekula kuwa ndio gundi inayoshikilia jamii pamoja. Usekula ndio shina la tatizo ambapo mfumo hutumikia maslahi ya wenye nguvu, kwa gharama ya watu wa kawaida. Nguvu ndio kitu kikubwa kinachozingatiwa katika demokrasia; na wasekula hata hawaoni haya kusema hili.

Lau kama wanajua aibu na heshima, watetezi wa usekula kama Macron mwenyewe wanapaswa kuhisi aibu kutokana na ukatili ambao unafanywa kote ulimwenguni kwa jina la usekula. Lau kama wanajua akili na busara, wanapaswa kuukataa mfumo wa kisekula moja kwa moja; kwani sio tu kwamba unashindwa waziwazi kuunda maelewano yoyote nyumbani, bali haukujengwa juu ya msingi wa kiakili. Wasekula hawawezi kuikinaisha akili kwa imani yao, kwa hivyo wanamkandamiza kila anayesimama kuipinga, halafu bila aibu anajisifu juu ya utovu wao mkali wa uvumilivu. Kwao haki inajulikana kwa nguvu, sio uthibitisho wala ushahidi. Hawana tofauti na mnyanyasaji wa kawaida, anayejua udhalili wake, na kumfanya kila mtu mwingine ateseke kwa nguvu zake zote na kutoweza kuukabili ukweli.

Uislamu hauko katika mgogoro na hauwezi kamwe kuwa. Tofauti na usekula na demokrasia, sio fikra ya kupumbaza lililootwa na kipote cha wasomi matajiri ili kumtiisha kila mtu mwingine. Uislamu uliteremshwa kwa Nabii Muhammad (saw) kama ujumbe wa mwisho na wa hitimisho kwa wanadamu wote.

Inajulikana kutoka kwa vyanzo vyake viwili: Qur’an na Sunnah (maneno na vitendo vya Mtume). Huthibitishwa kupitia mapambano yake ya kifikra kwa watu wote na kuafikiana kwake na umbile la mwanadamu.

Kipengele cha kisiasa cha Uislamu huwapaza watetezi wa kisekula usingizi usiku. Maisha ya Nabii Muhammad (saw) ni dhahiri na waziwazi ya kisiasa, kwani yeye (saw) alikuwa akihusika na kuangalia mambo ya watu kulingana na Wahyi. Pamoja na hayo, wasomi wa Magharibi, taasisi, wanasiasa na vyombo vya habari hawaachi kwa gharama yoyote kukataa kwao Uislamu kuwa ni wa kisiasa, na majaribio yao duni ya kuelezea fikra ya "Waislamu wenye siasa kali" kama uvumbuzi wa kisasa na uchafuzi wa dhati ya Uislamu.

[إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُون]

“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [TMQ 8: 48]

Uislamu una mwongozo kamili juu ya jinsi ya kuunda jamii ambayo mahitaji ya watu wote yanatimizwa. Uislamu sio msamiati mfupi katika sera na maono yake. Uislamu hauvumilii viongozi wanaopima maamuzi yote kulingana na jinsi wanavyoonekana kuwa maarufu kwa wapiga kura. Hao ndio viongozi wa sasa wa dola kuu za Kimagharibi leo, ambao usimamizi wao wa kihalifu wa uchumi, janga la maambukizi na sera ya kigeni umefichua wasiwasi wao halisi, kwa kuacha msururu wa vifo nyuma yao.

Khilafah ambayo kipote cha wasomi wa Magharibi wanaiogopa na kujaribu kuipaka matope kwa kuilinganisha kwao na kirongo na udanganyifu wa ISIS yao, itasimama kama ngao ya kulinda raia wake kutokana na uvamizi wa wakoloni. Hawataweza tena kuwafanya watumwa watu wengi wa ulimwengu na kuwazibaka karibu rasilimali zake zote. Hawataweza tena kupuuza uharibifu wa mazingira ambao mashirika yao hufanya katika hamu yao ya kutotosheka ya ukuaji. Ulimwengu kwa haraka utaona upotovu wa mfumo wa kirasilimali, mtindo wake wa uchumi uliofeli na itikadi yake ya kirongo ya kisekula. Hili ni jambo ambalo kipote cha wasomi wenye ubinafsi kihakika wanapaswa kuliogopa. Lakini kwa watu wa kawaida, ni uokovu wao kutokana na maonevu ya kisekula na ya kikoloni.

Khilafah kwa njia ya Utume itarudi hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Ni ahadi ya Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na ndio ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi usiku na mchana kuisimamisha tena. Imejengwa juu ya kanuni za utunzaji wa haki za kila mtu, sio wenye nguvu pekee. Haki inajulikana kwa ushahidi na sio yeyote anayetumia nguvu. Watawala wanawajibika kikweli mbele ya watu, na sio tu kuwajibika kirongo kwenye sanduku la kura. Vyombo vya habari ni huru kweli kweli na sio kundi linalowakilisha maslahi makubwa ya kibiashara kama ilivyo leo katika Magharibi ya kisekula.

Tunakualika ujisajili na ujiunge na Hizb ut Tahrir / Uingereza kwa kongamano lake la kimataifa la mtandaoni: Kurudi kwa Mfumo wa Kiulimwengu wa Kiislamu.

Wazungumzaji watahutubu mada zifuatazo:

Kutoka kwa Janga la Maambukizi hadi BLM: Wanadamu Wanatafuta Badali kwa Hamu

Nidhamu ya Khilafah, Utunzaji wa Watu

Kuasisi Uongozi wa Uislamu Duniani na Wajibu wetu

Jumamosi, 31 Octoba Saa Nane Mchana GMT

Jisajili katika

 Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@domainnomeaning.com / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu