Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  8 Rajab 1441 Na: 1441/27
M.  Jumanne, 03 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ni Miaka Tangu Kuanguka kwa Khilafah... Mpaka Lini Tutaendelea Kubakia kama Mayatima Katika Meza za Mabwana Walafi?!
(Imetafsiriwa)

Enyi Waislamu:

Katika siku hii, 03/03/1924 M sawia na 28 Rajab 1342 H, wasaliti katika Waarabu na Waturuki wakishirikiana na makafiri wa kikoloni wakiongozwa na Uingereza kwa wakati huo, na kuiangusha dola ya Khilafah, dola ambayo iliwaunganisha na kuwalinda Waislamu. Na kutokana na kuanguka huko dunia ilitikisika chini ya miguu yao na ardhi yao ikawa chini ya ushawishi mkoloni Kafiri na kuikatakata vipande, na kupachika msaliti katika kila kipande cha ardhi kama mtawala (wakimuamrisha naye akifuata, na wakimkataza naye akiacha), na waliwaorodhesha kufanya kila aina ya jambo bila kujali ni baya kiasi gani , ili kuzuia kurejea tena kwa Uislamu na Khilafah, hivyo basi watawala walioko wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza sera hatari dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa ujumla.

Tangu siku hiyo ya huzuni, majanga na mashaka yametufunika sisi Waislamu, mauaji yametuzunguka kushoto, kulia na katikati. Mayahudi, waliokuwa wamekwama katika udhalili, wamewezeshwa na Uingereza kuivamia ardhi ya Palestina - ardhi ya Israa na Mi'raj, na kuimarishwa na Amerika, ambayo imekusanya mataifa kwa ajili ya kupambana na Uislamu na Khilafah, kwa hiyo wakaiharibu Iraq na Afghanistan, na rais wake, Trump, ametembelea India, baada ya muda Wahindu wakaanza kuwadhalilisha na kuwaua Waislamu… ilhali nchini Uchina, Ummah wote umetiwa jela kwa kuwa ni Waislamu. Ama katika nchi ambazo Waislamu wanaandamana kupinga nidhamu ya Kimagharibi na vibaraka wake, mataifa ya kiulimwengu yakaungana dhidi yao kumsaidia mchinjaji wa Ash-Sham katika kuwachinja Waislamu kila siku, na wanaingiliakati nchini Yemen na Libya, na kuziingiza katika vita visivyoisha na kuwapasua.

Ama kuhusu Tunisia, ambayo ilikuwa ndio nukta kianzio cha mapinduzi, wajumbe wa kikoloni, mashirika ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kimataifa yalifurika nchini ili kuzuia kuanguka kwa mfumo wa kisekula wa kirasilimali, na Tunisia kubakia masikini, iliyotengwa na kuwa ni mali ya Wamagharibi. Wamelazimisha katiba za kisekula, na kuwatumia vibaraka wao, kudhibiti vyeo muhimu na idara katika dola na tumebakia kudhalilishwa kiasi kwamba balozi wa Uingereza ndiye anayeamua nani awe Rais, na serikali yote, na kuweka sera zake, na IMF inaamua mipango yake ya kiuchumi…

Enyi Waislamu katika Ardhi ya Zaytuna:

Hii ndio dola na hali ya Waislamu leo; mpasuko, mgawanyiko, ukoloni na udhalilishaji. Takribani miaka miaka mia moja, Ummah umeishi bila dola, bila Khilafah, wala Khalifah, tunaishi kama Waislamu, na ilhali Uislamu umewekwa mbali na uongozi, siasa, uchumi na nidhamu nyingine za maisha. Kwa hiyo, imepelekea uharibifu na ufisadi kuwa juu katika ardhi zetu, na mkoloni Kafiri kutuongoza, na vibaraka kuwa juu yetu mpaka tumekosa fahari na hadhi, kiasi kwamba Muislamu anadhalilishwa popote aendapo. Sababu iko wazi, tumeambiwa na Al-Faruq (ra), alisema: “Tulidhalilishwa na Mwenyezi Mungu akatupa hadhi kupitia Uislamu, kwa hiyo lau tutatafuta utukufu kupitia chochote kile kisichokuwa Uislamu, basi Mwenyezi Mungu atatudhalilisha.”

Enyi Waislamu katika Ardhi ya Zaytuna, Ardhi ya Wakombozi Mashujaa,

Mwenyezi Mungu (swt) anasema

[... وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ]

“… Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu – Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanafiki hawajui.” [Al-Munafiqun: 8]

Ukoloni haukuandikiwa kudumu, ila tatizo ni ukimya wetu kuhusu ukoloni na vibaraka wake katika ardhi zetu. Tunawakukumbusha katika siku hii ya maumivu ya kukumbuka kuangushwa kwa Khilafah, dola ambayo ilifanyakazi ya kutuunganisha sisi pamoja na Waislamu wengine. Wakati huo, Tunisia ndio ilikuwa ndio kiongozi upande wa magharibi wa Khilafah kwa karne nyingi, na ilikuwa ndio kiongozi katika ukanda wa Mediterranean, na wakati Khilafah ilivunjwa ilhali tuko kimya, na Uislamu ukaondoshwa ilhali tumeridhia, na ardhi zetu zikawa duni vijipande!

Leo hii, ilhali mapinduzi yamechipuka katika nchi yenu ambayo yametikisa ardhi za nchi za kikoloni, (kwa sababu ni mapinduzi ya Ummah ambayo yamesambaa katika ardhi zote za Waislamu, na kuashiria kuanguka kwa tawala zao, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu). Tunawahutubia ili kuwakumbusha utukufu ambao ulijengwa na mababu zenu, na tunaweza kuurudisha tena leo kwa sababu Uislamu uliowapandisha daraja mababu zetu bado upo baina yetu kama ulivyoteremshwa kwa Mtume wetu (saw), na miongoni mwenu kunao viongozi wenye akili na utambuzi: Hizb ut Tahrir; kiongozi asiyedanganya. Na munaifahamu vizuri kwa ukweli wa maneno na vitendo vyake, ikiwa haitafuti zawadi wala sifa kutoka kwa yeyote, isipokuwa ikitafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutekeleza shari’ah Zake ardhini, kwa kuitikia mwito wa Mwenyezi Mungu (swt)

[فَلَا وَرَبِّكَ لا يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجاً مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيماً]

“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utakayotoa, na wanyenyekee kabisa.” [An-Nisa: 65]. Hivyo basi, muonyesheni Mwenyezi Mungu (swt) yaliyo mazuri, na ondosheni dhambi ya kutelekeza mwito wa Bwana wenu.  Kama Waislamu hatusamehewi mpaka tufanye kazi kwa bidii ya kusimamisha taji lililipotea la wajibu (taj al-fard); Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume, ambayo kwa uhakika inatarajiwa hivi karibuni. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt): Ambaye alisema: 

 [وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً...]

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.... [An-Nur: 55].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir WilayahTunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu