Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  11 Jumada II 1441 Na: 1441 H / 03
M.  Jumatano, 05 Februari 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Miezi Sita Imepita, Na Wabebaji Ulinganizi na Watu Maarufu wa maeneo yaliyokombolewa Bado wako katika Magereza ya al-Julani
(Imetafsiriwa)

Utawala wa Uturuki ulisumbuliwa na kazi kubwa ya wabebaji ulinganizi, uliolenga kuzuia kongamano la Sochi na vipengee vyake vya hatari zaidi: kufungua barabara za kimataifa; haswa baada ya watu wengi maarufu wa mkoa kuingiliana na harakati hii, wakati chama kilipanga maandamano baridi mengi kwenye barabara hizi; na ziara nyingi kwa vile vinavyojulikana kama  vituo vya “dhamana” ya Uturuki", na kufanya kongamano ambalo mamia ya watukufu walikusanyika kujadili hali ya mapinduzi; na wakawasilisha suluhisho sahihi lililositisha mporomoko huu kuendelea, ikifuatiwa na taarifa nyingi zilizotolewa na watu maarufu wa mikoa hiyo, ambazo zilichochea utawala wa Uturuki kupeleka moja ya silaha zake (al-Julani) kuzindua kampeni dhidi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir na watu maarufu wa maeneo yaliyokombolewa. Walianza na uzuiaji wa vifaa vya Matangazo ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir.

Ikifuatiwa na kampeni ya kukamatwa walinganizi wengi wa Khilafah na watu maarufu; wakati ambapo wanaume wao wa usalama walitekeleza njia mbaya zaidi za uhalifu ambazo zilielekezwa moja kwa moja wakati wa shambulio na kukamatwa, kama ilivyotokea katika mji wa Killi. Ni muhimu kutambua kuwa matendo haya ya kukandamiza sio maalumu kwa kikundi cha HTS (Hay'at Tahrir al-Sham, “Shirika la Ukombozi wa Al-Sham”), lakini badala yake ni vitendo jumla vya vikundi vingi vinahusiana na ujasusi wa dola; kwa idadi tofauti ya ukandamizaji na uhalifu. Ilitanguliwa na ISIS ambayo iliwakamata wanachama wa Hizb ut Tahrir na kuwanyanyasa na hata kuwauwa baadhi yao. Ilitanguliwa pia na Jeshi la Rahman (Failaq Ar-Rahman), Jeshi la Uislamu (Jaish Al-Islam) huko Ghouta, Suqour al-Sham Brigade na wengine ambao walikuwa tayari kuwa zana mikononi mwa ujasusi wa kimataifa dhidi ya walinganizi wa Khilafah; na dhidi ya kila mtu anayezungumza ukweli.

Enyi Waislamu nchini Ash-Sham Makao ya Uislamu:

Zaidi ya miezi sita imepita na bado walinganizi wa Khilafah na wakuu wa maeneo yaliyokombolewa wako gerezani, kana kwamba wao ndio wanaowaua Waislamu katika vikwazo vya barabara na katika barabara! Kana kwamba wao ndio walioikabidhi dini kwa kushirikiana pamoja na nchi zinazounga mkono, kana kwamba wao ndio wanaowanyanyasa watu wa Ash-Sham katika maisha yao kwa kuwawekea ushuru! Kana kwamba wao ndio wanaozuia kufungua vita vya Sahel na kushikana na vita vingine! Kana kwamba wao ndio waliovisitisha vikundi kwa kuchukia kupigania cheo na ushawishi! Kana kwamba wao ndio wanaotekeleza sera ya kukandamiza, kunyanyasa, kifungo na mauaji ya mateso!!

Enyi Waislamu nchini Ash-Sham Makao ya Uislamu:

Nyote nyinyi mwajua uhalifu wa utawala wa Urusi na tawala nyingine, uhalifu huu ambao hakuna msikiti, shule, duka la kupika mikate, nyumba, au gereza zilizoonewa huruma na nyinyi nyote mwajua kuwa suala la kulenga magereza halijaanzishwa leo. Gereza kuu la Idlib lililengwa zaidi ya mara moja, na mamimia ya wafungwa waliuawa; na jamaa zao wengi, wanawake na watoto waliokuwa wa kizuru waume zao na baba zao. Magereza mengine yalilengwa, na yajulikana na wote kuwa magereza katika maeneo yaliyokombolewa chini ya nidhamu hii ya vikundi iliyoweka sera ya ukandamizaji, uonevu, na kuwafunga watu midomo wasizungumze. Wameongezeka na hawahesabiki. Na kwa kusisitiza kwa nidhamu hii ya vikundi kukamata wale wakweli kutoka maeneo yote na kuwaweka wao gerezani na vurugu hili la kulipua maeneo yaliyokombolewa kwa jumla, tunachukulia usisitizo huu kama mauaji ya makusudi na usitisho uliokusudiwa, kwani haijafichika kwa kila mtu mporomoko wa haraka na ghafla kwa maeneo, na hili linawezesha kwa wafungwa wengi kuanguka katika makucha ya madhalimu wa Ash-Sham.

Kwa hivyo, kila mtu lazima aende mbio kuwatoa wafungwa waliokandamizwa katika magereza ya nidhamu ya vikundi, na kila mkweli, bila kujali nafasi yake, lazima awe na nafasi ya kuhesabiwa na Mwenyezi Mungu; kwa hivyo anafanyakazi ya kuondoa nguvu za yanayoitwa majimbo yanayounga mkono kuhusiana na maamuzi ya viongozi wa vikundi na kusonga mbele na kazi ya kung’oa utawala wa kiuhalifu na kusimamisha utawala wa Kiislamu ambao hakuna anayekandamizwa.

Mwenyezi mungu (swt) asema:

[وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ وَسَتُرَدُّونَ إِلَى عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ]

“Na sema, tendeni vitendo na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.” [At-Taubah: 105]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu