Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  2 Sha'aban 1442 Na: 011 / 1442 H
M.  Jumatatu, 15 Machi 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Mapinduzi ya Ash-Shama, Msiwe kama Yule ambaye Kuzunguka kwake Kulikoma Baada ya Nguvu ikawa Maangamivu

(Imetafsiriwa)

Kumbukumbu ya miaka kumi ya Mapinduzi ya Ash-Sham imetufikia na huku tukiona ni mambo gani yamegeuka, na hali ya mapinduzi imefikia wapi, baada ya kafiri Magharibi kufaulu kuyapotoa njia yake kwa msaada wa ala zake, na baada ya kukaribia kuyamaliza kwa lile linaloitwa suluhisho kisiasa, moja ya hatua ya kwanza ambayo ni kuunda kamati ya katiba ambayo kazi yake ni kuweka katiba inayofafanua aina ya serikali, mifumo yake, na vyombo vyake; Ili kwamba dola ya kisekula iwe mbali na Uislamu katika mfumo wake wa serikali na umbo la dola yake, vyombo vyake, na mifumo yake, na hivyo kudhamini kubakia kwa udhibiti wake juu ya nchi na uwezo wake, na Waislamu wanabaki katika ardhi ya Ash-Sham ndani ya duara la udhibiti hata ikiwa itapita amri kuwabadilisha wachinjaji wao katika uchaguzi "huru na wa haki" - hakuna chochote kibaya kwake katika kuwa huru kumchagua ni nani atakayekuchinja - na yote ambayo Magharibi kafiri imeyafanya kwa njia ya mikataba ya amani, mazungumzo na makongamano ni utangulizi wa uhalifu huu unaoitwa suluhisho la kisiasa; Kwa sababu suluhisho hili halitabadilisha chochote katika ukweli wa uhalisia, bali uchumi wa dola hii wa baadaye utabaki kutegemea sera za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia, ambazo zinafanya kazi kudhibiti uwezo wa nchi na umaskini wa watu, na nidhamu na kanuni zitabaki kutoka kwa mtazamo wa kafiri Magharibi ambayo hutenganisha Uislamu na maisha, ambayo inategemea kuivuruga familia ya Kiislamu kwa kisingizio cha haki za wanawake na usawa wake pamoja na wanaume na kueneza uovu kupitia mashirika ya jamii ya kimataifa kama UNICEF na mengine, na tabaka la kisiasa linalotawala ambalo linafanya udhalimu, ukandamizaji, ubabe na udikteta litabaki kuwa vibaraka wa kafiri Magharibi na wastwa wake wa kisiasa, na jeshi litabaki kulitegemea tabaka hili kibaraka la kisiasa na kutegemea silaha na mafunzo yake ya kafiri Magharibi, Na litaendelea kutumiwa kulinda tabaka la kisiasa linalotawala kutokana na jaribio lolote la mageuzi, na kuua watu wa Ash-Sham kila inapobidi kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kuweka usalama na utulivu, na shule na vyuo vikuu vitaendelea kufundisha mitaala ya elimu ambayo inapotosha Uislamu na kuondoa hukmu zake na kueneza kutengwa, ujinga na kurudi nyuma miongoni mwa watoto wa Waislamu kupitia mipango yao iliyoendelezwa chini ya uangalizi wa wale ambao wana chuki na Uislamu; Ili kuhakikisha kuwa inabaki katika mzunguko wa zile zinazoitwa nchi za ulimwengu wa tatu, na sera ya kigeni itabaki kutegemea sera za Umoja wa Mataifa na Baraza lake la Usalama, kwa maana nyengine, uvamizi na utumwa utaendelea kututawala katika nyanja zote za maisha, na yote haya ni chini ya misamiati tofauti tofauti inayotakiwa katika kila hatua, Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

﴿وَلَنْ تَرْضَى عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴾

"Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu." [Baqara: 120]

Enyi Waislamu katika ardhi ya Ash-Sham, makao ya nyumba ya Uislamu:

Baada ya ukweli huu kubainika, hakuna budi kwenu basi mtambue umbile la mapambano, kwamba ni mapambano baina ya haki na batili, na kwamba hakuna suluhisho nusu, na haiwezekani kukutanisha haki na batili katikati ya njia; Hakuna suluhisho la kati na kati, kulegeza msimamo, wala kuwategemea madhalimu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ﴾

"Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa." [Hud: 113]

Hapana budi kuwe na mageuzi ya kimsingi ili kuhifadhi kujitolea kwenu na kudhamini kuishi kwenu maisha yenye hadhi chini ya utawala wa Uislamu chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya utume ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu alitoa bishara njema ya kurudi kwake baada ya kumalizika kwa utawala wa kiimla ambao tunaishi ndani yake, na hili linahitaji kwenu ukakamavu juu ya haki na kujitenga na dola zote hizi kwa sababu ni ala za kuhakikisha maslahi ya mabwana zao, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿وَلَوْلَا أَنْ ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدْتَ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئاً قَلِيلاً * إِذاً لَأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيراً﴾

"Na lau kuwa hatukukuweka imara ungeli karibia kuwaelekea kidogo* Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo. Kisha usinge pata mtu wa kukunusuru nasi." [Isra: 74-75]

Hapana budi kutembea katika njia ya mageuzi ya kweli ambayo inategemea mwongozo wa Mwenyezi Mungu ili kuhakikisha ushindi na msaada wake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ﴾

"Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu." [Muhammad: 7]

Mwenyezi Mungu (swt) hatayanusuru mapinduzi ambayo lengo lake ni kusimamisha dola ambayo haikuhumu Sharia Yake maishani, inaruhusu riba na kamari kwa kisingizio cha uhuru wa umiliki, inaruhusu ushoga na kutembea uchi kwa kisingizio cha uhuru wa kibinafsi, inaruhusu uasi dhidi ya Uislamu na kupinga Sunnah ya Mtume mtukufu kwa kisingizio cha uhuru wa imani, na inaruhusu kutukanwa kwa Mtume wake kwa kisingizio cha uhuru wa rai na kujieleza .. Nusra imikononi mwa Mwenyezi Mungu peke huwatunuku tu wale wanaofanya kazi, ili neno la Mwenyezi Mungu liwe kuu zaidi.

Tunapoishi kwenye kumbukumbu ya miaka kumi ya kuanza kwa Mapinduzi ya Ash-Sham, lazima turekebishe mwenendo wetu, turudishe uamuzi wetu, na tuzingatie malengo na msimamo wetu, huku tukimtegemea yule ambaye nusra iko mikononi mwake pekee, tukiwa tumeshikamana na kamba imara ya Mwenyezi Mungu, na HAPO ndipo bendera za ushindi zitarudi kufurahisha tena nyoyo zetu.

﴿... وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ﴾

"Na siku hiyo Waumini watafurahi* Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu." [Ar-Rum: 1-7]

Ahmad Abdul Wahhab

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu