Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  18 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 13
M.  Jumapili, 26 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Wanawake wa Kisekula, Tunamuomba Mwenyezi Mungu Asikuinulieni Bendera wala Asikufikisheni Lengo Lenu
(Imetafsiriwa)

Uratibu wa Majeshi ya Kidemokrasia ya Kiraia (Taqaddum) unatangaza uzinduzi wa kikao cha ufunguzi wa Mkutano wa Tafakari wa Wanawake, kama sehemu ya shughuli za kongamano lake anzilishi. (Al Jazeera Sudan, Mei 25, 2024).

Sisi, katika Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, tungependa kufafanua ukweli ufuatao:

Wanawake wa Taqaddum ambao walikuwa ... katika kipindi cha serikali ya muungano ya Kaht (Serikali ya Kiraia ya FFC) na jeshi, ambalo lilidumu sio chini ya miaka miwili, lilifanya vitendo vya kuifanya jamii kuwa ya kisekula, na bado wanaamini kwamba wanafurahia kikamilifu leseni yao ya awali ya kisiasa, ambayo walichukua baada ya wizi wa vuguvugu la vijana mnamo Disemba 2018, wakiwa wamepanda farasi wa mapinduzi ya watu wa Sudan, kwa hivyo walitema sumu ya usekula, wakiahidi maisha ya uhuru, na kujisifu kwa kukanyaga vima na maadili yote, kunyanyua kauli mbiu za uhuru na ukombozi kila mahali.

Sasa, inatosha kukuza udanganyifu wa kisiasa. Mikutano hii haitashufaiya, ila nyinyi wanawake huria, na mnataka wanawake wa Sudan wavue vazi la stara na tohara, na waige wanawake wa Kimagharibi kama nyinyi, ambao hawana uwezo wa kutoa manufaa yoyote kwa jamii yao au kwao wenyewe, zaidi ya kuwa bidhaa za kununuliwa na kuuzwa. Hatutakubali biashara yoyote katika masuala ya wanawake kutoka kwenu, na hamtawadanganya wanawake wa Sudan tena kwa misemo ya kuvutia, kama vile haki za wanawake, dori ya wanawake, na kujitambua wenyewe. Kauli mbiu hizi zimefichuliwa, na zimekuja kuwakilisha sura mbaya ya ombaomba wa afisi za balozi za kikoloni za Magharibi, zinazoasi maadili, viwango na imani za wanawake wa Sudan, ambazo msingi wake ni Uislamu mtukufu.

Mikusanyiko hii na karamu za kisekula ni jino tu katika gurudumu la hadhara inayoporomoka ya Kimagharibi, Mwenyezi Mungu akipenda. Mabadiliko makubwa kwa msingi wa Uislamu, kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo inatabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, yatawatupa kwenye jaa la kisiasa milele, na hata itawawajibisha kwa kupigia debe hadhara inayogongana na fahamu na fikra za Uislamu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu asikunyanyulieni bendera, wala asikufanyeni mufikie lengo la kuwafanya wanawake wa watu wa Sudan kuwa masekula, kwa badali ya malipo ya mateke atakayokupigeni msaidizi baada ya mahitaji yake kumalizika. Uvundo wa kufanya biashara kwa udanganyifu unatosha. Kile alichokisema Petronella White wa Uingereza, baada ya kutumia muda mwingi wa maisha yake kutetea vuguvugu la wanawake, ambapo aliandika makala akieleza majuto yake, akisema: “Sina mume, sina mtoto, na niko peke yangu. Vuguvugu la kutetea haki za wanawake limeniangusha, na limeangusha kizazi changu chote.” (Chanzo: Britain Arabic).

Kamari ya leo sio juu ya ukoloni, wala afisi za balozi za Magharibi, bali ni juu ya Uislamu, ambao unatabikishwa na dola ya Khilafah Rashida (Ukhalifa ulioongoka) kwa njia ya Utume, ambayo muda wake ni umekuwa mrefu, na ambayo alfajiri yake iko karibu, Mwenyezi Mungu. akipenda.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake

katika Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu