Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  19 Rajab 1445 Na: 1445 / 21
M.  Jumatano, 31 Januari 2024

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوفْ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الأَمَوَالِ وَالأنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُواْ إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعونَ]
“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri, Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara 2:155-156]
(Imetafsiriwa)

Baada ya kuridhika na Qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan inamuomboleza kwa masikitiko makubwa zaidi aliyesamehewa, Mwenyezi Mungu akipenda:

Sheikh Abdul-Fattah Othman Muhiyidin

Ambaye alifariki dunia kwa hatma hii isiyoepukika mnamo siku ya Jumatano asubuhi, tarehe 19 Rajab 1445 H, sawia na tarehe 31 Januari 2024 M, katika eneo la Wad al-Mahdi mashariki mwa Khartoum. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amjaalie rehema na msamaha wake mkubwa, na aijaalie pepo ya juu kuwa ndio makaazi yake na kimbilio lake.

Marehemu alikuwa kinara wa amali na shauku katika kubeba Dawah ili kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume tangu miaka ya sabiini. Nyumba yake ilikuwa mashukio ya wabebaji dawah. Alikabiliwa na kukamatwa katika jela za madhalimu akiwa katika njia ya kubeba Dawah. Misimamo yake ilikuwa ya kuheshimika, na alibaki imara licha ya ugonjwa ambao ulimkosesha uwezo katika siku zake za mwisho.

Rambirambi zetu za dhati kwetu sisi wabebaji Dawah kwa kufiwa kwake, na rambirambi zende kwa familia yake, watoto wake, jamaa na marafiki zake.

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara 2:156]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu