Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  21 Jumada I 1444 Na: HTS 1444 / 17
M.  Alhamisi, 15 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wanatumia Pesa zao kwa ajili ya Kuunda Vibaraka, Watazitumia kisha itakuwa ni Huzuni kwao, Mwenyezi Mungu Akipenda
(Imetafsiriwa)

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya jijini Khartoum ulitangaza utoaji wa kitita cha euro milioni 15, ambapo euro milioni 5 zitatengwa kusaidia na kuimarisha utawala wa sheria kupitia upatikanaji wa haki. Naye balozi wa ujumbe huo, Aidan O'Hara, alieleza kuwa euro milioni 5 zitatengwa kwa ajili ya kusaidia vijana wanaofanya kazi katika kipindi cha mpito cha demokrasia na amani, akisisitiza kuwa wanawake ndio nguvu inayounga mkono mapinduzi, hivyo mpito huo hautafanikiwa bila wao. kuhusu Sudan kuonyesha dhamira yake ya kutetea haki za wanawake kwa kutia saini Mkataba wa Kutokomeza Aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW). Kutangaza nia yao ya kutoa utaalamu wa kiufundi kwa timu zinazoshiriki katika mashauriano kuhusu masuala ambayo hayajakamilika na nyeti katika awamu ya pili ya muundo wa makubaliano, hasa kuhusu uadilifu wa mpito.

Ujumbe huo wa Muungano wa Ulaya ni miongoni mwa taasisi za kikoloni zinazofanya kazi zake nchini Sudan na nchi nyingine za Kiislamu, ili kuunda vibaraka wenye kubeba fikra na fahamu za Kimagharibi kuhusu maisha, hivyo wanawalenga vijana hasa wanawake kwa vile vijana siku zote ndio msukumo wa mabadiliko na ili waweze kukazanisha mshiko wao katika nchi yetu, na kuwazuia vijana kutokana na mabadiliko ya kweli, wanafanya kazi kwa bidii na kulipa pesa ili kuwapotosha kutoka kwenye njia, na kuwalazimisha kufuata njia ya upotofu wa Magharibi. Watawala Ruwaibidha wanawasaidia katika hilo, wameuza Dini yao kwa dolari na euro, na kufungua wazi nchi nzima kwa ajili ya misheni kama hizi za kuwachafua vijana na wanawake wa Ummah huu!

Ujumbe huu mchafu unaitaka serikali kutii na kutia saini CEDAW, mkataba wa ukahaba na upotoshaji. Mkataba unaotaka familia za Kiislamu kusambaratika kwani familia zao zimesambaratika katika nchi za Magharibi. Vile vile inawalipa pesa kwa vijana ili kuwafanya wafungwa wa mfumo wa Kimagharibi hufanya kutenganisha dini na maisha kuwa itikadi kwao, kuwatenganisha na Uislamu wao ili wawe watawala wa baadaye wa nchi hii. Lakini hili liko mbali sana, kwani watatumia pesa zao, kisha itakuwa ni huzuni kwao, Mwenyezi Mungu akipenda, kama alivyosema Aliyetukuka:

[إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنْفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ]

“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [Al-Anfal 8:36].

Kuna vijana katika Ummah huu wanaomwamini Mwenyezi Mungu kama Muumba wao, na Uislamu kama Dini yao, na Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kama Nabii na Mtume wao. Wanafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya mwamko wa Ummah kwa msingi wa Uislamu, na wanatafuta kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Enyi Vijana na Wanawake wa Sudan: Jihadharini na kutumbukia katika mitego ya Shetani, na jihadharini na pesa chafu, na jueni kwamba nyinyi ni watoto wa Waislamu, basi mfanyeni Kafiri kuwa ni adui kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu:

[إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوّاً مُبِيناً]

“Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.” [An-Nisa 4:101]. Ni wajibu wenu kufanya kazi na wanaofanya kazi kwa ajili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na sio kwa ajili ya mabadiliko ya kidemokrasia, na hivyo mtashinda hapa ulimwenguni na Akhera.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu