Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  17 Muharram 1444 Na: HTS 1444 / 02
M.  Jumatatu, 15 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mapendekezo ya Kongamano la Majadiliano ya Ombi la Watu wa Sudan Hayakutengana na Hazina ya Mfumo wa Kibepari wa Kidemokrasia

(Imetafsiriwa)

Kongamano la majadiliano ya pande zote ya kile kinachoitwa Wito wa Watu wa Sudan lilihitimisha kazi yake jana, Jumapili, kwenye Ukumbi wa Urafiki jiji Khartoum, na lilitoka na mapendekezo kadhaa, mengi yakiwa ni matakwa, na mazungumzo ya kujirudia ambayo hayakutengana na hazina ya mfumo wa kibepari wa kidemokrasia. Mapendekezo mabaya zaidi yalikuwa ni mazungumzo juu ya kuoanisha Katiba ya 2005 na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini huko Juba, na kuainisha shirikisho la serikali.

Mapendekezo hayo pia yalizungumzia uchaguzi kwa msingi wa kidemokrasia wa Kimagharibi mwishoni mwa kipindi cha mpito.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunathibitisha yafuatayo:

Kwanza: Mpango wa kuwaita watu wa Sudan haukuegemezwa kwenye Uislamu, bali uliegemezwa kwenye uzalendo alioundwa na mkoloni, na kujitolea kulichana taifa hili vipande viapnde, na ndio kikwazo kwa umoja wake kwa msingi wa Uislamu chini ya dola yake moja; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambao ndio msingi wa batili katika Shariah, na chochote kinachojengwa juu ya batili ni batili. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَى تَقْوَى مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَمْ مَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَى شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ)

“Je! Mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora au mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalo burugunyika, na likaburugunyika naye katika Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.” [At-Tawbah:109].

Pili: Kukiri kupitia kuifanya katiba ya 2005 kuwa ndio msingi na kuioanisha na Mkataba wa Amani wa Juba kunathibitisha kwamba makongamano hayo mawili yako mbali na Uislamu, kwani katiba ya 2005 ni katiba kamili ya kisekula, iliyoanzishwa na Rabbi wa Kiyahudi wa Amerika John Danforth, kisha ikawa ndio sababu ya kuitenganisha Sudan kusini na kaskazini, na kuyaandaa maeneo yake mengine. Vile vile aliufanya uraia kuwa msingi wa haki na wajibu na hakuifanya itikadi ya Kiislamu kuwa ndio msingi, na hukmu za Shariah kuwa ndio kipimo kwani ni faradhi juu ya Waislamu.

Tatu: Maandiko ya shirikisho la serikali, pamoja na kugongana kwake na Uislamu, unaolazimu umoja wa dola, kwa hakika ni hatua ya kivitendo ya shirikisho ambayo imezua mizozo na vita vya kikabila, na ndiyo iliyoileta nchi hadi ukingoni mwa shimo wakati wahusika wanadai haki ya kujiamulia wenyewe eneo la mashariki na magharibi mwa Sudan, ambayo kwayo kusini ilitenganishwa.

Nne: Juhudi zinazotafuta mbinu ya maafikiano ya utawala nchini Sudan zote zimefeli, na nyengine zitaanguka, kwa sababu utawala na mamlaka lazima viegemezwe kwenye fikra msingi, na kwetu sisi Waislamu, utawala umejengwa juu ya itikadi ya Kiislamu ambayo kwayo mifumo huchipuza ili kushughulikia matatizo ya watu. Na kupangilia maisha kwa hukmu za Shariah zilizoletwa kwa wahyi.

Kwa kutamatisha: Sisi katika Hizb ut Tahrir tunamlingania kila mtu, vyama na harakati, wanajeshi na raia, vijana kwa wazee:

Kuisoma katiba iliyo vuliwa kutokana na wahyi iliyo tabanniwa na Hizb ut Tahrir, na kufanya kazi nasi katika kuileta madarakani ili tutoke nje ya sanduku la Magharibi kafiri na mkoloni ambalo tumekuwa ndani yake kwa miongo kadhaa, na bado ingali ina hamu ya kutubakisha ndani yake, kuufanya utenganishaji dini na maisha kuwa ndio msingi wa utawala, siasa, uchumi na kadhalika. Katiba ya Kiislamu ni kuregesha tena kwa maisha kamili ya Kiislamu ambayo Kafiri wa kikoloni aliyakata kupitia kuiangamiza dola ya Kiislamu Khilafah, ni ahadi ya Mola wetu Mlezi aliye sema:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur:55].

Ndiyo ambayo Mtume wetu kipenzi, rehema na amani zimshukie, alitoa bishara njema kwayo.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu