Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  24 Shawwal 1443 Na: HTS 1443 / 37
M.  Jumanne, 24 Mei 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Haifanyi Kazi Shirika na Upande Wowote
(Imetafsiriwa)

Chama cha Sheria na Maendeleo kilitoa habari zenye kichwa: "Chama cha Sheria na Hizb ut Tahrir zinajadiliana hatua ya pamoja ya kuelimisha taifa," ambapo ndani yake kilitaja ziara ya ujumbe wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika makao makuu ya Chama hicho cha Sheria, na mkutano wa kiongozi wa chama hicho, Dkt. Muhammad Ali al-Jazouli, jana, Jumatatu, 23/05/2022, na kutokana na kile kilichoelezwa kwenye habari hizo: “Vyama hivi viwili vinaamini umuhimu wa kazi shirika katika kunyanyua utambuzi na ufahamu wa taifa, na kuhamasisha nguvu zake kuendeleza uvamizi wa kifikra unaolenga itikadi na kitambulisho chake."

Na ili habari hii isieleweke kando na uhalisia wake, sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunathibitisha yafuatayo:

Kwanza: Hizb ut Tahrir inataka kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na kwa ajili hiyo hukutana na viongozi kutoka kwa wanasiasa, wanafikra, wanataaluma wa vyombo vya habari na wengineo, kama inavyokutana na umma kwa jumla, na tunaonyesha kila mtu mpango wetu tunaoutabanni ili wafanye kazi nasi kwa lengo adhimu.

Pili: Tunafanya kazi nyingi za kisiasa, na tunawaomba wanasiasa, viongozi wa kazi ya Kiislamu na wengineo kushiriki kwa kuzungumza, na baadhi yao wanashiriki katika hilo. Baadhi ya ndugu katika mashirika na vyama pia hutualika tushiriki katika kuzungumza katika baadhi ya amali zao, nasi tunashiriki nao kwa kuwasilisha ruwaza yetu juu ya mada husika. Kwa vyovyote vile, sisi huwatambulisha wengine kama walivyo na kuwaomba watutambulishe kama tulivyo.

Tatu: Hatufanyi kazi yoyote shirika na chama chochote, kwa sababu tunatabanni fikra iliyo wazi na la komavu, na tunafuata njia maalum yenye jinsi sawa kama fikra katika usafi na uwazi wake. Kwa hiyo, hatubadilishi njia yetu, bali tunamlingania kila mmoja kutembea kulingana na njia yetu, ambayo tunaiona kuwa ndio njia pekee ya Shariah ambayo itatuongoza kwenye lengo tunalifanyia kazi. Matatizo ya Sudan, nchi zote za Kiislamu, na hata dunia nzima hayawezi kutatuliwa isipokuwa kwa Uislamu, ambao hauwezi kutekelezwa chini ya dola za kitaifa za Sykes-Picot, bali unatekelezwa ndani ya dola yake ya kiulimwengu inayofafanuliwa na Uislamu; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

 [قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ]

“Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.” [Yusuf: 108]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu