Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  27 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: HTS 1442 / 78
M.  Alhamisi, 08 Julai 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maafa ya Bwawa la An-Nahdha juu ya Sudan na Misri Yanatekelezwa kwa Ushirikiano wa Watawala Wao na ni Khilafah Rashida Pekee Ndio Inayoweza Kuyaondoa
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumanne, 07/06/2021, Ethiopia iliiarifu Sudan juu ya kutekeleza ujazo wa pili wa ziwa la Bwawa la An-Nahdha, kwa kiasi cha mita za ujazo bilioni 13.5 za maji, ambayo inasababisha uharibifu wa huduma muhimu za Khartoum na maisha ya wakaazi milioni 20 , kwa mujibu wa taarifa rasmi.

Imejulikana kwa rai jumla nchini Sudan na Misri, ukubwa wa hatari za janga la Bwawa la An-Nahdha, bwawa hili ambalo lilijengwa katika eneo la mtetemeko wa ardhi; Mkondo mkubwa, na limejengwa juu ya msingi wa saruji inayoweza kupasuka, kilomita 20 tu kutoka mpaka wa Sudan, mita 127 juu kuliko Khartoum, mita 505 juu ya uso wa ardhi, na kiwango kikubwa cha maji kinafikia mita za ujazo bilioni 74, ambazo iliwafanya wataalamu wengi kusema kwamba ikiwa litalipuka, ni bomu ambalo litaiangamiza Khartoum na miji yote kwenye Blue Nile kwa masaa tu kama matokeo ya mafuriko makubwa. Na hili lilithibitishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uhandisi katika Wizara ya Ulinzi ya Ethiopia, Jenerali Buta Bachata Debele katika mahojiano na Kituo cha RT cha Urusi, mnamo Ijumaa, 25/6/2021, ambapo alisema: "Endapo bwawa litaharibiwa, hutaiona Sudan wala Misri, kwani mafuriko yatawasomba hadi ndani ya Bahari ya Mediterania," na akasisitiza kwamba "baada ya kujazwa mara ya pili,  kila mtu atakuja kwenye meza ya mazungumzo, niamini kwa sababu ni (bwawa) kubwa; Mita za ujazo bilioni 13.” Lakini licha ya hatari hizi, serikali mbili nchini Misri na Sudan zilishirikiana kwa ucheleweshaji, zikiipa serikali ya Ethiopia muda wa kutosha kujenga bwawa hilo na kukamilisha ujazaji wa kwanza na kisha kuanza ujazaji wa pili, na kutoa taarifa za vyombo vya habari kwa matumizi ya ndani bila kuchukua uzito wowote na msimamo mkali ambao unailazimisha Ethiopia kukomesha tishio hili baya. Mnamo siku ya Jumatano 07/07/2021, "Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi aliionya Ethiopia juu ya hatari ya mzozo juu ya Bwawa la An-Nahdha." Na "Waziri Mkuu Abdullah Hamdok alisema kuwa Bwawa hilo Kubwa la Ethiopia la An-Nahdha linabeba hatari halisi ikiwa makubaliano ya uwajibikaji wa kisheria hayatafikiwa kuhusiana na ujazaji na uendeshaji, na akasisitiza kuwa hatari kwa Sudan ni kubwa kuliko kwa Ethiopia, ambapo bwawa hilo liko katika mipaka yake, na kwa Misri, ambayo iko maelfu ya maili kutoka kwake.” (BBC 04/08/2021)

Duru nyingi za mazungumzo ya kipuuzi zilishindwa kufanya maendeleo yoyote kwenye faili hii, hadi bwawa hilo lilipokaribia kukamilika na kugeuzwa kuwa bomu la wakati, na kwa njia ile ile, kuipa Ethiopia muda wa kutosha kujaza bwawa hilo. Kikao cha leo cha Baraza la Usalama kinajiri kwa ombi la Sudan na Misri, ambazo Rais wa Baraza la Usalama, Nicolas de Riviere, yeye mwenyewe alikidharau na kuthibitisha kutokuwa na faida kwake, ambaye alisema mnamo tarehe 01/07/2021: "Baraza la Usalama halina mengi yanayoweza kufanywa katika mgogoro wa Bwawa la An-Nahdha, isipokuwa kuleta pande zote pamoja ili kuelezea wasiwasi wao, kisha kuwashajiisha kurudi kwenye mazungumzo ili kufikia suluhisho!”

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunazionya serikali hizi vibaraka washirika kutokaa kimya juu ya hatari hizi halisi ambazo wamezikiri, na tunawahesabu kwa maangamivu yoyote ya uhai au mali yanayosababishwa na bwawa hili kwa watu wa nchi hii, na tunawahakikishia watu wetu nchini Sudan na Misri kwamba serikali hizi za kitaifa ni chombo tu mikononi mwa wakoloni, hazipaswi kupewa mamlaka au utiifu. Hakuna suluhisho kwetu isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya Uislamu kwa njia ya Utume, kwani lau tungekuwa na Khalifa, hakuna yeyote angetutisha, sio kwa bwawa hili wala kwa kitu chengine chochote. Mtume (saw) alisema:

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

"Hakika, Imam (Khalifa) ni ngao, watu hupigana nyuma na hujihami kwayo ambayo" [Muslim]. Kwa hivyo, watu wa Sudan na Misri nawafanye kazi kwa ajili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwani ndiyo njia pekee ya kutokea na wokovu wetu.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu