Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  16 Dhu al-Hijjah 1441 Na: HTS 1441 / 63
M.  Alhamisi, 06 Agosti 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Kufuata Mtindo Ule Ule wa Serikali Iliyo Tangulia, Serikali ya Mpito Inahesabu Hasara na Kutofanya Lolote!!
(Imetafsiriwa)

Ripoti moja iliyo tolewa na Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Raia limefichua uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo nchini Sudan, kutokana na mvua iliyo nyesha katika siku zilizopita. Ripoti hiyo imehesabu hasara kuanzia mafuriko na mvua iliyolikumba eneo la jimbo la Khartoum la Nile Mashariki, maeneo mengine ya jimbo hili, Darfur na kwengineko, na kuthibitisha vifo vya watu 10, kuanguka kikamilifu kwa nyumba 1,872, na kuanguka kusio kikamilifu kwa nyumba 1,508, ikiongezewa na uharibifu mwengineo.

Msimu wa mvua unajulikana na kila mtu, na hauji kwa ghafla, lakini serikali zilizofeli, ambazo zimefuatana katika utawala wa Sudan, zimekuwa hazifanyi lolote kila mwaka kuzuia athari za mvua. Kuanzia kufungua mitaro ya majitaka, kujaza vifusi sehemu zinazo hitaji kujazwa, na marekebisho mengine yanayo julikana ambayo ni lazima yafanywe kabla ya mvua kuja, lakini kila mwaka maafa yanatokea, na tunapoteza idadi kadhaa ya wapendwa wetu, nyumba zinavujika, mimea kusombwa na maji, mifugo kufa, watu kukosa makao, na serikali zinatazama tu maafa haya na kuhesabu hasara, ambayo ndiyo yaliyotokea mwaka huu. Kama serikali iliyo kuja baada ya mapinduzi, na ambayo watu walidhani ilikuja kuleta mabadiliko, inafuata njia ya serikali iliyo tangulia, hatua kwa hatua; inahesabu hasara na uharibifu, na kisha haifanyi lile inalolazimika kufanya, kabla na baada ya maafa, na kumuacha kila mmoja kupotea.

Hizb ut Tahrir, kiongozi asiye wadanganya watu wake, imethibitisha na kuthibitisha kila wakati, kwamba serikali hizi ambazo zimetawala nchi yetu tangu wakoloni waondoke kijeshi na hadi leo, bila ya kuzingatia miundo yake; ya kidemokrasia, kijeshi, na kidikteta, ambayo yote haikujengwa juu ya nidhamu ya uangalizi, bali juu ya nidhamu ya urasilimali iliyo jenga juu ya msingi wa ukusanyaji kodi, hivyo, serikali zinabadilika, nyuso zinabadilika, lakini nidhamu inabakia ni ile ile, na sera zinabakia zile zile.

Enyi watu wa Sudan: Wekeni mikono yenu katika mikono ya Mashabab wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha dola ya uangalizi, inayo chunga mambo yenu kwa msingi wa imani yenu, na kuweka maisha mazuri kwa ajili yenu, kwa sababu utawala katika mfumo mtukufu wa Uislamu ni "Amana" na jukumu, kama alivyo sema kipenzi Al-Mustafa (saw):

«...وَإِنَّهَا أَمَانَةُ وَإِنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ إِلا مَنْ أَخَذَهَا بِحَقِّهَا وَأَدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا»

“... na hakika ni "Amana" na Siku ya Kiyama ni fedheha na majuto isipokuwa kwa yule aliyeuchukua kwa haki yake na akatekeleza majukumu yaliyo juu yake kwa sahihi”, sio kama ilivyo hivi sasa, "keki" na mgao ambao kila mmoja ana hamu ya kupata sehemu yake!

Kwa kheri ya ulimwengu huu na Akhera, tunawalingania kusimamisha dola ya Uislamu, Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, ambayo Mtume (saw) ametoa bishara yake njema:

«...ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ نُبُوَّةٍ، ثُمَّ سَكَتَ»

“…Kisha itakuwep Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha (saw) akanyamaza”.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu