Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  7 Sha'aban 1443 Na: BN/S 1443 / 11
M.  Alhamisi, 10 Machi 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Kizazi cha Kwanza cha Hizb ut Tahrir

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzaab: 23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inamuomboleza mmoja wa wanaume wa Hizb ut Tahrir, mbebaji Da’wah kutoka kizazi cha kwanza katika safu zake. Marhum kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt):

Al-Hajj Sa’di Abdul Karim Abu Ramaila At-Tamimi (Abu Anwar)

Aliyekwenda katika rehma za Mwenyezi Mungu (swt) mnamo siku ya Alhamisi, Machi 8, 2022. Al-Hajj, Mwenyezi Mungu amrehemu, alitumia maisha yake kubeba ulinganizi wa Uislamu, akifanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, popote aliposafiri na kukaa. Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa mstari wa mbele kuubeba ulinginizi huu. Alijiunga na safu za Dawah katika miaka ya hamsini na akabaki imara juu ya haki, mwenye kushikamana na hukmu za Shariah, akitumainia nusra ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume wake (saw) ya kuregea Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alibaki hivyo mpaka alipofariki akiwa na umri wa takriban miaka 91.

Inajulikana vyema kuwa Al-Hajj Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa alijitolea kuamrisha mema na kukataza maovu, kudhihirisha hukmu za Shariah na kushikamana nazo. Alikuwa makini kueneza matumaini katika moyo wa familia yake, jamaa na watu kwa jumla. Mara nyingi alitoa machozi alipozungumzia suala la Palestina, na kwamba ukombozi wake uko karibu. Al-Hajj alipata ndoto usingizini (Ru’iyah) ya Mayahudi wakiingia Al-Quds kabla ya kukaliwa kwake, na ikawa kweli. Katika ndoto hiyo hiyo, aliona ukombozi wa Palestina mikononi mwa Majeshi ya Kiislamu nyuma ya Imam, akiwaongoza chini ya bendera ya La ilaha ila Allah Muhammad Rasool Allah. Alitarajia kushuhudia hili katika maisha yake.

Mwenyezi Mungu ambariki marehemu wetu mpendwa kwa Rehma zake Pana, na amjaalie maskani yake katika Mabustani yake makubwa, Inna Lilah Wa Inna Ilaihi Raji’uon, “Hakika Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake Yeye tutaregea”. Mwenyezi Mungu ailipe familia yake thawabu nyingi na awajaalie subira na faraja, na hatusemi ila yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Ni cha Mwenyezi Mungu alichokitoa na ni cha Mwenyezi Mungu alichokichukua, kila kitu kwake kimewekwa kwa muda maalumu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu