Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  20 Rabi' II 1446 Na: 1446 / 15
M.  Jumapili, 20 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mswada wa Marekebisho ya 26 ya Katiba:
Chini ya Khilafah, Madaraka na Mamlaka Vinaamuliwa na Qur'an Tukufu na Sunnah, Wakati Kuna Mivutano ya Kuendelea ya Madaraka Chini ya Demokrasia

(Imetafsiriwa)

Hatimaye, baada ya mvutano wa muda mrefu wa mamlaka, serikali ilifanikiwa kupitisha Mswada wa Marekebisho ya 26 ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba mnamo Jumatatu, tarehe 21 Oktoba 2024. Katiba sasa inaipa serikali mamlaka ya kuteua Jaji Mkuu inayomtaka. Pia inabatilisha arifa za suo motu na Mahakama ya Upeo. Aidha, inaipa serikali mamlaka ya kuunda benchi la katiba kwa ajili ya ‘mambo ya kikatiba.’ Hivyo kwa sasa, katika mvutano huu wa madaraka kati ya uongozi wa kisiasa na kijeshi na mahakama, mahakama imedhoofika. Hata hivyo, ni wazi kwamba mapambano haya yataendelea. Ikipata fursa, mahakama itakataa marekebisho haya kwa jina la kuingilia ‘uhuru wa mahakama.’ Ama bunge, litaendelea kupambana na mizani mpya ya utawala, kwa wingi wa theluthi mbili. Kwa upande wa watu, wataendelea kuumia chini ya mzigo wa mfumo tawala wa Demokrasia, kama watazamaji wa mvutano huu wa kugombea madaraka. Ndani ya mvutano huu wa madaraka, hakuna uhusiano na masuala “yasiyohusika” kama vile ustawi wa watu, uboreshaji wa utawala, utoaji wa haki!

Chini ya mfumo tawala wa Demokrasia, mzizi halisi wa ufisadi ni uwezo wa walio wengi waliochaguliwa kubadili kila sheria, kila kifungu cha katiba, kila kanuni na kila agizo. Nguvu ya kutunga sheria inavipa vikundi tawala uwezo wa kubadilisha sheria kulingana na maslahi yao, sio tu kupitia mlango wa nyuma, lakini kupitia mlango wa mbele. Nguvu ya sheria ndiyo inayoliruhusu Bunge kuhalalisha wizi unaofanywa na waporaji na wafujaji kupitia Sheria ya Maridhiano ya Kitaifa, kukubali kunyang'anywa madaraka na madikteta kwa nguvu, kupitisha mipango kadhaa ya msamaha kwa mirengo inayotawala na kutoa kinga ya kikatiba ya kutoshtakiwa kwa wale wanaohusika na mambo muhimu zaidi ya nchi. Ni katiba na sheria chini ya mfumo tawala wa Demokrasia ambayo inaharamisha ukosoaji wa maafisa wakuu wa kijeshi na mahakama. Nguvu ya sheria inafunga mlango wa uwajibikaji wao. Inaidhinisha marupurupu yanayoongezeka kila mara kwa wenye nguvu, wakiwemo wabunge.

Nguvu hii ya sheria pia inahakikisha uwasilishaji wa nchi kwa maslahi ya wakoloni. Inaruhusu kuiwasilisha kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ambao uliitumbukiza nchi katika mtego wa deni kubwa. Iliruhusu kuwasilisha matakwa ya Jopo Kazi la Kifedha, ambalo liliharamisha jihad kama uungaji mkono ugaidi, lilihalalisha Vita vya Amerika dhidi ya Ugaidi na kukita mizizi potovu na mibovu ya maadili ya kiliberali ya Magharibi. Maadamu wanadamu ndio wanaomiliki mamlaka ya kutunga sheria, sheria zitabaki kuwa mtumishi wa vipote tawala, na sheria zitafinyangwa kwa manufaa ya vipote hivyo tawala, ndani ya uwanja wa mivutano ya madaraka. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[فَٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُۖ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ عَمَّا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡحَقِّۚ]

“Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [Surah Al-Maaidah 5:48].

Chini ya mfumo wa utawala wa Khilafah madaraka na mamlaka ya mtawala, raia, na maafisa wengine huamuliwa na Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume. Hata mtawala mwenye nguvu zaidi hana budi kujisalimisha kwa sheria za Mwenyezi Mungu (swt), kwa sababu haya ni maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu (swt). Khalifa wa Nne wa Waislamu, Imam Ali (ra) alipoteza kesi yake kuhusu silaha zake zilizoibiwa, dhidi ya asiyekuwa Muislamu katika mahakama ya Khilafah, kutokana na ukosefu wa mashahidi halali. Hakuruhusiwa kubadilisha hukmu za Shariah zinazohusiana na utoaji ushahidi. Ilikuwa ni sharti katika sheria ya Kiislamu, na Khalifa pia alikuwa amefungwa na sheria hii. Ibn Kathir amepokea katika Al-Bidayah wan-Nihayah kwamba kadhi Shuraih alimuuliza Khalifa, يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ هَلْ مِنْ بَيِّنَةٍ؟  “Ewe Amirul-Mu’minin kuna ushahidi?” Imam Ali (ra) akajibu, أَصَابَ شُرَيْحٌ مَا لِي بَيِّنَةٌ “Shuraih yuko sahihi. Sina ushahidi.” Hivyo kadhi Shuraih akatoa hukmu kwa upande wa asiyekuwa Muislamu, dhidi ya Khalifa. Kabla ya kusilimu na kukiri kosa lake, yule asiyekuwa Muislamu alitangaza, أَمَّا أَنَا فَأَشْهَدُ أَنَّ هَذِهِ أَحْكَامُ الْأَنْبِيَاءِ أَمِيرُ الْمُؤْمِنِينَ قَدَّمَنِي إِلَى قَاضِيهِ وَقَاضِيهِ يَقْضِي عَلَيْهِ “Ama mimi nashuhudia kwamba hii ni hukmu ya Mitume. Kiongozi wa waumini mwenyewe ananipeleka kwa kadhi wake na kadhi wake anatoa hukmu dhidi yake!”

Khilafah kwa Njia ya Utume iko sawia na thabiti kwa sababu sheria ni ya Mwenyezi Mungu (swt) Pekee. Iko huru kutokana na misukosuko ya ndani na machafuko ya kisiasa, na hakuna mivutano ya madaraka ambayo inabadilisha sheria. Baada ya kulazimishwa utekelezaji wa demokrasia katika Ulimwengu wa Kiislamu, Ummah daima unateseka kutokana na ukosefu wa utulivu na vibaraka wa kikoloni. Wakati umefika sasa wa kuondokana na mfumo huu uliokamatwa na kipote cha mabepari, kwa kutabikisha mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[اَلَا یَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ ؕ وَهُوَ اللَّطِیْفُ الْخَبِیْرُ۠]

“Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” [Surah Al-Mulk, 67:14].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu