Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  20 Muharram 1446 Na: 1446 / 02
M.  Ijumaa, 26 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ajenda ya Mapinduzi ya Uislamu
Kurekebisha Uchumi wa Pakistan, Baada ya Kuharibiwa kupitia Sera za Wakoloni

(Imetafsiriwa)

 Utabikishaji wa sera za wakoloni umeharibu uchumi wa Pakistan, ambao una rasilimali nyingi sana. Kwa hatua na vipimo vyote, serikali na watu wa Pakistan wako kwenye ukingo wa kufilisika. Madeni ya mzunguko wa sekta ya nishati na bili za umeme haziwezi kumudika. Licha ya ongezeko la mara nne la ukusanyaji wa ushuru katika miaka tisa iliyopita, nakisi ya kifedha ya bajeti ya shirikisho, ya rupia bilioni nane na nusu, inazua maswali mazito kuhusu uwezo wa serikali. Watu wanalazimishwa kila mara kuafikiana na mahitaji yao ya kimsingi, huku wengi wakikimbia nchi. Katika miaka miwili iliyopita, mfumko wa bei kwa mwaka umekuwa zaidi ya 30%, huku uchumi ukitegemea fedha za kigeni, ukosefu wa ajira ulioenea, utumwa wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na kusujudu kwa uchumi mbele ya mfumo wa kilimwengu wa Kimagharibi. Uchumi wa Pakistan uko katika mshiko wa wahasiriwa wa uchumi wa Magharibi. Ili kuepuka mgogoro huu wa kiuchumi, Hizb ut Tahrir inawasilisha ajenda ya mapinduzi ya Uislamu kwa watu wenye ushawishi na mamlaka nchini Pakistan.

1) Kukomeshwa kwa sarafu ya isiyo na thamani ya dhati (fiat) na kutoa fedha kwa msingi wa dhahabu na fedha kutakomesha uchapishaji usio na kikomo wa fedha, ambao utapunguza sababu kuu ya mfumko wa bei. Kuibadilisha biashara ya kimataifa hadi kwa dhahabu na fedha pia kutakomesha utawala wa dolari, na faida ya kimkakati ya utawala wa nchi moja wa shughuli za kimataifa. Sarafu ya dhahabu na fedha itaondoa nakisi za kifedha, kupunguza nakisi ya sasa ya biashara za kigeni na kuleta utulivu wa biashara ya ndani na ya kimataifa. Uislamu umenasibisha sarafu na dhahabu na fedha katika hukmu mbalimbali za Shariah, kama vile nisab ya Zakah, kiasi cha wizi kinachoamrisha kukata mkono wa mwizi, pesa za damu (diyah), kuharamisha ulimbikizaji na ubadilishanaji wa fedha (sarf). Ni wazi kwamba sarafu ya Uislamu inategemea dhahabu na fedha.

2) Katika mfumo wa sasa, Pakistan inalipa takriban Rupia bilioni 10,000 kama riba kulipia deni la shirikisho, na zaidi ya Rupia bilioni 2,000 katika malipo ya uwezo wa mitambo ya umeme ambayo pia inategemea malipo ya riba. Ikijumuishwa na riba ya mikopo ya kampuni, uchumi wa Pakistan umezama katika deni. Hukmu za Uislamu zinajulikana sana na ni za uhakika kuhusiana na Riba. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَييْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا]

“Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.” [Surah Al-Baqarah 2:275]. Khilafah itakataa kata kata malipo yote ya Riba ya ndani na ya kimataifa.

3) Kupitia ubinafsishaji, rasilimali muhimu na vitengo vya viwanda vyenye thamani ya mabilioni na matrilioni ya rupia hukabidhiwa kwa makampuni machache na mabepari. Unafanywa kwa jina la fahamu ya uliberali mamboleo ya “sekta ya kibinafsi kuwa injini ya ukuaji.” Ubinafsishaji umefanya hazina ya serikali kuwa duni, ambayo imesababisha ushuru zaidi, nakisi ya kifedha na kuongezeka kwa deni. Uislamu unaleta rasilimali za madini na nishati, zenye thamani ya mabilioni ya dolari, ambazo ni mali ya umma katika Uislamu, chini ya usimamizi wa serikali. Hili linasababisha utoaji wa mahitaji muhimu kwa umma kwa bei nafuu, huku ikizalisha mapato ya kushughulikia mambo ya umma. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «المسلِمونَ شُركاءُ في ثلاثٍ؛ في الكَلَأِ والماءِ والنَّارِ» “Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho na moto (nishati)” (Abu Dawood). Khilafah Rashida pia itaanzisha viwanda vyenye nguvu vya kijeshi vinavyoendeshwa na serikali, na vile vile kuhakikisha dori kubwa ya serikali katika viwanda vizito.

4) Uislamu unatoa mtazamo wa kipekee juu ya kodi. Kama ilivyo uhai wa watu, heshima, sifa, utajiri wao pia ni utakatifu unaolindwa. Akitoa khutba katika Ibada ya Kuhiji ya Kuaga Siku ya Udh’hiya huko Mina, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema,  إنَّ دِماءَكُم، وأمْوالَكم وأعْراضَكُم حرامٌ عَلَيْكُم كَحُرْمة يومِكُم هَذَا، في شهرِكُمْ هَذَا، في بلَدِكُم هَذَا، ألا هَلْ بلَّغْت “Damu zenu, na mali zenu, na heshima zenu, ni ni tukufu kwenu kuzikiuka, kama utukufu wa siku yenu hii, katika mwezi wenu huu, katika mji wenu huu. (Muslim na Bukhari). Mapato ya serikali kama Zakat, Ushri, Kharaj, Jizya yanakusanywa kwa msingi wa dalili ya Shariah, na Uislamu unatoa muundo kamili kwa hili. Hakuna mtu, ikiwa ni pamoja na serikali, ana haki ya kuchukua chochote kutoka kwa mtu yeyote bila ya dalili yoyote ya Shariah. Kwa hivyo, kwa kuzingatia kanuni hii, Kodi ya Jumla ya Mauzo (Sales Tax), Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ushuru wa forodha kwa wafanyibiashara wa ndani, ushuru wa uzalishaji wa ndani (excise), pamoja na malipo ya ziada, ushuru wa zuio (withholding tax), ushuru wa mapato, ushuru wa kampuni na ushuru mwingine wowote wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja ni haramu katika Shariah. Uislamu hauwatozi kodi masikini na wenye madeni, wanaostahiki Zaka. Unaruhusu ushuru wa dharura kwa matajiri, ambao wanaweza kutumia kikidhi mahitaji yao ya kimsingi na baadhi ya ziada pia, katika dhurufu fulani ili kutimiza wajibu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّ صَاحِبَ الْمَكْسِ فِي النَّارِ» “Hakika mwenye kutoza ushuru ataingia motoni.” (Ahmed).

5) Katika mfumo wa Magharibi, mali ya umma huhamishwa kupitia mifumo ya benki, masoko ya mitaji na soko la hisa kwenda kwa makampuni makubwa,  yenye umbo la makampuni makubwa ya hisa, kupitia mikopo ya riba au mtaji, na hivyo kulimbikiza faida nyingi katika mkono ya michache. Hakuna wigo katika Uislamu kwa muundo wa ufadhili uliojengwa juu ya riba au ushirikiano wa makampuni yasiyo ya Kiislamu. Badala yake, Uislamu una aina maalum za makampuni, al-anan, al-abadan, mudharabah, wajuh na mufawadhah, ambapo washirika wanajulikana, na kudhibiti kiasi cha mtaji kinachoweza kuunganishwa, ambapo inaruhusu serikali kutawala viwanda vinavyohitaji mtaji mwingi. Kwa hivyo, mapato ya sekta hii inayomilikiwa na serikali huboresha hazina, na kupunguza utegemezi wa ushuru.

6) Uislamu pia una ajenda ya kimapinduzi kuhusu kilimo, ambayo inaweza kugeuza kilimo cha Pakistan. Sera ya utwaaji wa umiliki kwa ajili ya kufufua ardhi iliyokufa, ardhi kame, ugawaji upya wa ardhi baada ya miaka mitatu ya kutolimwa, na uharamishaji wa Uislamu wa kukodisha ardhi ya mashamba, yote yanasababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa ardhi, usalama wa chakula, mgawanyo wa mali na kutokomeza umaskini. Hii pia itasababisha kupunguzwa kwa bei ya ardhi ya makaazi na kodi. Khilafah itatekeleza amri hizi kama hukmu ya Shariah. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «مَنْ أَحْيَا أَرْضًا مَيِّتَةً فَهِيَ لَهُ» “Mwenye kuhuisha ardhi iliyokufa, kame, basi inakuwa yake”. (Tirmidhi).

Hukmu za Shariah ya Kiislamu zinahusu mambo mengi yakiwemo uagizaji na uuzaji bidhaa nje ya nchi, gharama na mapato, udhamini wa mahitaji ya kimsingi, uharamu wa haki miliki, ambazo zinatekelezwa tu chini ya mfumo wa Khilafah. Baadhi ya vipengele vya ubepari mamboleo na ujamaa vimeharibu uchumi wa Pakistan. Je, sio wakati sasa wa kutekeleza ajenda hii ya Uislamu? Je, ni watu wangapi zaidi wanapaswa kukwama kwenye kinu cha njaa na umasikini kabla hatujaanza kutabikisha Uislamu? Je! Mpaka lini watoto wetu watanyimwa hata feni kwenye jua kali? Je, si tayari imepitiliza? Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُواْ التَّوْرَاةَ وَالإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيهِم مِّن رَّبِّهِمْ لأكَلُواْ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم]

“Na lau kuwa wangeli ishika Taurati na Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao.” [Surah Al-Maidah, 5:66]. Hizb ut Tahrir tayari imewasilisha maelezo ya nukta hizi zote katika machapisho yake. Basi jitokezeni na mshirikiane na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya utabikishaji wake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu