Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  18 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 1444 / 40
M.  Jumatano, 07 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ramani Utendakazi ya Uislamu ya Kuepuka Mgogoro wa Sarafu wa Pakistan

(Imetafsiriwa)

Kwa muda sasa, watu wenye mamlaka wa Pakistan wanapambana na mgogoro wa sarafu. Hawawezi kupata njia ya kutoka, kwa uwazi. Maandalizi yao ya kibajeti ni ishara zaidi ya hilo. Mgogoro wa sasa wa sarafu ya Pakistan unatokana na mfumo maalum wa fedha, ambao watawala wa Pakistan wameutabanni. Pakistan imetabanni mtindo wa sarafu ya isiyo na thamani ya dhati (fiat), unaounganisha thamani ya sarafu yake na dolari ya Marekani. Katika mtindo huu, thamani ya fedha inategemea uwezo wa uzalishaji wa uchumi, akiba ya fedha za kigeni na uwezo wa Pakistan kupata fedha za kigeni. Wakati wowote kiwango cha ukuaji wa Pakistan kinapopungua, akiba yake ya fedha za kigeni inapungua, uwezo wake wa kupata fedha za kigeni unapungua. Thamani ya Rupia ya Pakistan inashuka, na kuleta wimbi la mfumko wa bei kwa Waislamu wa Pakistan.

Mipango ya Waziri wa Fedha itafeli, licha ya uhakikisho wake wa mara kwa mara. Kurekebisha kiwango cha rupia kwa dolari kwa thamani fulani, au kutabanni kiwango cha ubadilishaji kinachotegemea soko, hakutasuluhisha mgogoro wa sarafu ya Pakistan. Mawazo haya yote mawili ni matoleo mawili ya muundo ule ule wa fedha wa sarafu ya fiat, ambapo sarafu haina thamani yoyote ya ndani. Badala yake, inapata thamani yake kutokana na mambo mengine, kama vile nguvu ya uchumi, muundo wa biashara ya kimataifa ya nchi na thamani na upatikanaji wa dolari. Kwa hivyo, watu wenye mamlaka hawataiokoa nchi kutokana na mgogoro wake wa sarafu.

Uislamu unatoa mfumo wake wenyewe wa fedha. Uislamu umeamuru kwamba sarafu ya dola iegemezwe na utajiri wa madini ya thamani, na kumaliza sababu kuu ya mfumko wa bei na mgogoro wa sarafu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliridhia ufinyanzi wa Dinari za Dhahabu, zenye uzito wa 4.25g, na Dirham za Fedha, zenye uzito wa 2.975g, kama fedha za dola. Dhahabu na fedha zina thamani ya kindani na hudumisha thamani yake bila kutegemea nguvu ya uchumi wa nchi au kiasi cha akiba yake ya fedha za kigeni. Katika hali ya nakisi ya biashara wakati dhahabu na fedha za dola zinaondoka katika dola, upunguzaji wa kiasi cha dhahabu na fedha husababisha kushuka kwa bei ndani ya dola. Kushuka huku kwa bei kunasaidia kukuza mauzo ya nje ya dola, na kusababisha uingiaji wa dhahabu na fedha kwenye hazina ya dola. Kwa hivyo, dhahabu na fedha zina utaratibu wa kujirekebisha zenyewe, ambao unashughulikia moja kwa moja tatizo la nakisi ya biashara.

Hairuhusiwi kwa Muislamu kutabikisha tiba ya Uislamu ya mgogoro wa sarafu, kupitia njia ya Demokrasia. Demokrasia ni mfumo ambapo maamuzi ya wanadamu ni matukufu, juu ya amri za Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Ni mfumo wa utawala wa Uislamu, Khilafah, ndio ambao unatabikisha tiba zote za Uislamu kwa matatizo ya Waislamu. Khilafah kwa Njia ya Utume itatabanni Dinar na Dirham kama sarafu ya Dola ya Kiislamu, na kumaliza mgogoro wa sarafu ya Pakistan kabisa na kuleta enzi ya ustawi, ambayo huletwa na pesa thabiti. Kwa hivyo, Enyi Waislamu, fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Kwa hiyo, Enyi Waislamu wa majeshi ya Pakistan, ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir sasa, ili muweze kufanya mabadiliko ya kweli ambayo Umma wa Kiislamu unayasubiri na kuyaomba.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu