Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  19 Jumada II 1444 Na: 1444 / 22
M.  Alhamisi, 12 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Licha ya Hifadhi Nyingi za Ngano, Watu Wananyimwa Mifuko ya Unga. Khilafah Itakomesha Siasa za Mgawanyiko za Kifederali Zinazotunyima Mahitaji Msingi

(Imetafsiriwa)

Video kadhaa zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii zimegusa nyoyo zetu, huku watu maskini wakivumilia mateso makubwa, huku wakiwa wamesimama kwenye foleni ndefu kutafuta magunia ya unga.  Baba wa watoto sita, mwenye umri wa miaka 35, alikanyanga katika mporomoko wa watu, huko Mirpur Khas, kwa sababu ya magunia ya unga ya kilo kumi. Watu wanaweza kuonekana waking’ang’ania mfuko wa unga wenye ubora duni, kwa bei ya serikali. Watu wanawalaani watawala, kwani wananunua ngano kwa bei maradufu. Watu maskini, tabaka la wafanyikazi sasa hawawezi hata milo miwili kwa siku. Haya yanajiri licha ya kwamba mkoa wa Punjab kwa sasa una hisa ya ngano ya siku 106, huku mkoa wa Sindh ukiwa na siku 98 na mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa ukiwa na siku 152, ukiwa na jumla ya tani 370,000 za akiba ya ngano. Meli nyingi zimetia nanga bandarini zikiwa zimesheheni ngano.

Mfumo wa kifederali, wa mikoa una dosari. Licha ya kuwa nchi moja, mikoa ya Sindh na Punjab inakataa kutoa ngano kwa Balochistan kwa bei ya chini. Kila serikali ya mkoa inawajibika kwa mkoa wake pekee, na sio kwa nchi nzima. Ni uovu wa mfumo wa kifederali kwamba kila mkoa unaweka bei tofauti za usaidizi wa ngano. Hili liliongeza mgogoro. Ni mfumo wa kifederali ambao serikali za vyama tofauti, katika mikoa tofauti, zinasukumana kwa makusudi katika migogoro, ili kushinda uchaguzi ujao, kupata maslahi yao ya kisiasa ya kibinafsi. Ndio maana serikali za kifederali na mikoa zinashughulika na kulaumiana wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo, watu wa Pakistan wanateseka na matokeo. Ilhali, kulikuwa na rekodi ya uzalishaji wa ngano nchini Pakistan mwaka jana. Hata hivyo, Pakistan inaweza kukidhi mahitaji ya Waislamu nchini Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati, katika upande wa uwezo wake wa kilimo. Hata hivyo, kutokana na mfumo wa kifederali, kidemokrasia, kibepari, watawala hawawezi kupata mahitaji ya chakula kikuu cha wanati, ngano.

Itakuwa ni mfumo wa umoja wa Khilafah, na mageuzi ya kilimo ya Uislamu, ambayo yataifanya Pakistan kuwa kapu la chakula la Ulimwengu wa Kiislamu. Khilafah haitatoa ngano kwa raia wa Khilafah peke yake, bali pia nchi zisizo za Kiislamu. Khilafah, kwa mujibu wa hukmu ya Shariah ya Kiislamu, itaondoa ukodishaji wa ardhi ya kilimo kwa ajili ya ukulima, kwa kodi au uzalishaji shirika. Itachukua ardhi kutoka kwa wale wamiliki ambao wameshindwa kulima ardhi yao kwa miaka mitatu mfululizo, na kuwapa wale ambao wanaweza. Khilafah itazifanya mamilioni ya hekta za ardhi tasa kulimwa kwa njia ya kimapinduzi. Khilafah itazifanya rasilimali za Umma wa Kiislamu, zikiwemo hifadhi za ngano, kupatikana kwa raia wote wa Khilafah kupitia mfumo wa umoja. Khilafah itakataa kuhifadhi ngano kwa ajili ya mkoa au eneo lolote, au tabaka lolote moja. Itatoa chakula, mavazi na makaazi kwa raia wake wote, bila kujali rangi au dini.

Enyi watu wa Pakistan! Hatutaona afueni yoyote kupitia kuwabembeleza wafalme wa Ghuba na maamiri, kuiomba Amerika, China na Ulaya na kuwanyonga watu kupitia masharti ya IMF. Hatua hizi hazitachelewesha maafa yanayokuja, zaidi ya miezi michache, au mwaka, au miwili. Ni wakati sasa wa kuzika siasa hizi za chuki dhidi ya watu za maslahi ya kibinafsi. Ummah unahitaji siasa na dola yenye msingi wa uchungaji wa mambo, ambayo Khilafah peke yake ndiyo inayoweza kutoa. Jitahidini kuweka misingi ya siasa mpya na dola mpya yenye msingi wa Uislamu. Kumbatieni Uislamu kama mfumo kamili wa maisha na mfumo wa utawala. Jitahidini ili mfumo wa sasa ulioundwa na mwanadamu ung'olewe na Khilafah kwa Njia ya Utume isimamishwe mahali pake. Mtegemeeni Mwenyezi Mungu (swt) na mukatae minong'ono ya Shetani. Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran Tukufu;

(إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمۡ عَدُوّٞ فَٱتَّخِذُوهُ عَدُوًّاۚ إِنَّمَا يَدۡعُواْ حِزۡبَهُۥ لِيَكُونُواْ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلسَّعِيرِ)

“Hakika Shet'ani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni.” [Surah Fatir 35:6].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu