Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  21 Rabi' I 1444 Na: 1444 / 12
M.  Jumatatu, 17 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Silaha za Nyuklia nchini Pakistan ni Ngao kwa Umma wa Kiislamu kutokana na Maadui Wake

(Imetafsiriwa)

Huku akikabiliwa na kuzorota kwa uchumi, jeshi lililovunjika moyo, machafuko ya ndani na uchaguzi mkali wa katikati ya muhula, Rais wa Marekani, Joe Biden, alitoa meno yake dhidi ya Umma wa Kiislamu, ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu wake. Mnamo tarehe 13 Oktoba 2022, Biden alisema, “Na kile ninachofikiria labda ni moja ya mataifa hatari zaidi ulimwenguni: Pakistan. Silaha za nyuklia bila mshikamano wowote.” Maoni yake ya kijasiri yalizua mjadala ndani ya Pakistan, ambao ulienea hadi iwapo watawala wa Pakistan sasa wataachana na silaha za nyuklia, huku wakililia umaskini.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Biden amekutoleeni meno yake, kwa hivyo mjibuni kwa upole. Hakika, silaha za nyuklia za Pakistan si za kujadiliwa au maridhiano, hata ikibidi tufunge mawe kwenye matumbo yetu. Umma wa Kiislamu lazima uwe na upinzani madhubuti dhidi ya Marekani, ambayo hujiingiza katika vitendo vya kikatili, ambavyo hata wanyama wa msituni huviepuka. Kuhusu madai ya umaskini, ambayo watawala wa Pakistan wanayatumia kuhatarisha usalama wetu, yanasababishwa na mfumo dhalimu wa kiuchumi wa wakoloni, ambao wao wenyewe wanautabikisha kwa niaba ya Biden.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Biden ametoa meno yake dhidi yenu, hivyo basi yavunjeni. Biden ni nani wa kuwakemea? Biden anakukemeeni kuhusu silaha za nyuklia zilizopatikana kwa bidii, huku akiunga mkono Dola ya Kibaniani, huku ikiongeza uwezo wake wa nyuklia na wa kawaida. Biden anakukemeeni kuhusu kujizuia kinyuklia, huku akiwataka mufungue milango wazi kwa ajili yake nchini Afghanistan, baada ya kujiondoa kijeshi kwa fedheha. Hivyo Biden anasubutuje kuwakemea, wakati munaweza, chini ya uongozi wa Kiislamu, kupindua mipango yake yote ya kikanda, ndani ya masaa?

Enyi Majeshi ya Pakistan! Nyinyi ni nani, kwamba Biden anaweza kuwakemea, bila ya meno yake kuvunjwa? Nyinyi ni jeshi la tisa lenye nguvu zaidi ulimwenguni, na la saba kwa ukubwa. Munapatikana katika ardhi zilizobarikiwa na kila aina ya rasilimali na Mwenyezi Mungu (swt), ambazo zilistawi chini ya utawala wa Kiislamu hapo awali, na zitastawi tena chini ya utawala wa Kiislamu. Mumependelewa na Imani kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), ambayo inakuzidishieni sana uwezo wenu wa kimada, ikiwa mutapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt), kutafuta ushindi na kifo cha kishahidi. Hivyo munawezaje kukubali Biden akukemeeni, mithili ya bwana anavyomkemea mtumwa?

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Ni hukmu ya yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt.) ndiyo itakayorudisha heshima, usalama na ustawi wa Umma wa Kiislamu. Ni nyinyi ndio mtakaoleta mabadiliko hayo, mkipata Dua ya Waislamu na Jannah, ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameitayarisha kwa ajili ya waja Wake (swt) watiifu. Toeni Nusrah yenu sasa kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Simamisheni tena Khilafah atakayotia hofu ndani ya maadui zenu hata kabla ya kusonga, na kulazimisha kurudi nyuma kwao kwa udhalilifu na kujisalimisha mara tu mtakapo hamasika. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(وَمَا ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ بِعَزِيزٍ)  

“Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu.” [Surah Ibrahim 14:20].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu