Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  1 Rabi' I 1444 Na: 1444 / 09
M.  Jumanne, 27 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Rupia Kubanwa kwa Dolari, Inahakikisha Kushuka kwa Thamani Yake. Katika Uislamu, Sarafu Inayoegemezwa juu ya Dhahabu na Fedha Itaokoa Pakistan na Ulimwengu wa Kiislamu kutokana na Utumwa wa Dolari

(Imetafsiriwa)

Serikali ya PDM inakabiliwa na hasira kali ya umma kutokana na mgogoro mkubwa wa sarafu, na dhoruba ya mfumko wa bei. Ili kutuliza umma, serikali imetangaza kuwa Waziri wa Fedha, Miftah Ismail, amebadilishwa kwa Ishaq Dar, ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kuimarisha thamani ya Rupia. Hata hivyo, hatua hii ya serikali ni kuwahadaa tu wananchi. Sababu kuu ya kushuka kwa thamani ya Rupia ni kubanwa Rupia kwa dolari. Kwa hivyo, sababu kuu ya mfumko wa bei ni msisitizo wa watawala wa Pakistan, juu ya kufanya biashara ya kimataifa kwa dolari za Marekani.

Mnamo tarehe 21 Septemba 2022, Hazina ya Serikali ya Marekani ilitoa uamuzi wa kuongeza viwango vya riba kwa asilimia 0.75, kwa mara ya tatu mfululizo, ikionya kwamba ongezeko zaidi la kiwango cha riba linatarajiwa. Kadiri thamani ya dolari ya Marekani inavyoongezeka, wawekezaji wanaanza kutoa dolari zao kwenye soko la madeni la nchi nyingine, na soko la kimataifa la madeni, ili kuwekeza katika bondi za Marekani. Matokeo ya kuondolewa kwa dolari katika masoko ya mitaji, na kuongezeka kwa thamani ya dolari duniani kote, yanasababisha kushuka kwa thamani ya sarafu ya nchi zinazofanya biashara ya kimataifa kwa dolari. Kushuka kwa thamani ya dolari huongeza bei ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, na kuongeza mfumko wa bei nchini Pakistan, huku rupia ikidhoofika.

Enyi Waislamu! Hazina ya Serikali ya Marekani huongeza viwango vya riba na sarafu zinaporomoka duniani kote! Ni aina gani hii ya mfumo wa kiuchumi kwamba sera ya fedha iliyotungwa na Marekani, ili kupata maslahi ya kiuchumi ya Marekani, inaharibu thamani ya sarafu duniani kote? Watawala wa Pakistan hawana dori yoyote katika kuamua sera ya fedha ya Marekani, ilhali bado kutokana na mfumo huu wa fedha, mfumko wa bei unaongezeka nchini Pakistani. Sarafu ya Pakistan inazama, hivyo mfumko wa bei unapanda na mgogoro mkubwa wa kiuchumi unazuka nchini Pakistan. Je, sio wakati sasa wa kuundoa mfumo huu wa kiuchumi na kusimamisha ule uliojengwa juu ya Uislamu?

Enyi Watu wenye Nguvu na Uwezo! Je, ni mfumo gani huu wa kiuchumi wa kilimwengu ambao watawala wa Pakistan wametuwekea, unaoleta mtikisiko wa kiuchumi duniani kote, kwa ajili ya maslahi ya Amerika na Magharibi? Watu wanakufa kwa sababu ya njaa na mfumko wa bei, huku uchumi wa Amerika unastawi. Je, munakubalije hili? Sababu ya mgogoro wa kiuchumi wa Pakistan ni kwamba uchumi wa Pakistan ni mtumwa wa mfumo wa kiuchumi wa Magharibi. Mfumko wa bei nchini Pakistan hauwezi kukomeshwa kwa msingi wa kudumu, hadi tuiondoe sarafu yetu kutoka katika utumwa wa mfumo wa kiuchumi wa wakoloni. Sarafu ya Kiislamu ni dhahabu na fedha, yenye kuzuia mfumko wa bei wenye kukandamiza. Khilafah haina sarafu moja ya matumizi ya ndani, na sarafu nyingine ya biashara ya kimataifa. Biashara ya ndani na nje zote zinafanywa kwa sarafu ya dhahabu na fedha.

Enyi Watu wenye Nguvu na Uwezo! Ustawi wa sarafu nchini Pakistan hautakuja kupitia kubadilisha waziri wa fedha. Itakuja kupitia kuitoa Pakistan kutoka katika utumwa wa mfumo wa kiuchumi wa Kimagharibi, kupitia utabikishaji mfumo wa kiuchumi uliojengwa juu Shariah ya Kiislamu. Kwa hivyo jitokezeni na muwaokoe watu wenu kutokana na mateso ya kiuchumi, yaliyosababishwa na mfumo wa uchumi wa kirasilimali. Kuweni Answaar wa Mwenyezi Mungu (swt), mkitoa Nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Mtaitwa Ansar wa leo, huku vizazi vya Umma vitakukumbukeni katika Dua zao. Basi je hamtafuti izza, heshima na mafanikio katika dunia hii na kesho Akhera, ile waliyopewa Ansar wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يٰۤاَيُّهَا الَّذِيۡنَ اٰمَنُوۡا كُوۡنُوۡۤا اَنۡصَارَ اللّٰهِ]

“Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu.” [Surah As-Saff 61:14].

 

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu