Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  25 Shawwal 1443 Na: 1443 / 66
M.  Jumatano, 25 Mei 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Demokrasia ndio Jukwaa Pekee la Uongozi wa Kisiasa Unaoungwa Mkono na Marekani, Bila ya Kuwepo Nafasi ya Kuvuka Mstari Wowote Mwekundu Unaochorwa na Marekani.

Kataeni Demokrasia, Simamisheni Khilafah

 (Imetafsiriwa)

Demokrasia huru ya udanganyifu ya Pakistan, kwa hakika, inaifanya Pakistan kuwa mtumwa wa maslahi ya Marekani kupitia mistari mekundu. Uongozi wa kisiasa unapewa nafasi tu kwa kadri ya mistari-mekundu ya ajenda ya Marekani kwa kanda hii, ikiwa ni pamoja na yale Pakistan, inayoruhusu. Uvukaji wowote wa mistari-mekundu ya Marekani, inamaanisha kuwa serikali, vyombo vya habari na nyanja za umma zote zimefungwa kwa nguvu, huku haki zote zikichukuliwa kikatili. Demokrasia inapiga vita jaribio lolote la uhuru kutokana na ukoloni. Kwa hakika, mabadiliko ya kweli yanawezekana tu kupitia njia iliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu ya Sunnah ya Mtume pekee, kupitia kujenga hitaji kubwa la umma la kuhukumiwa na yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) huku watu wenye uwezo, ulinzi na vita watoe Nusra yao kwa ajili ya kusimamishwa kwake mara moja.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Mabadiliko katika Demokrasia daima ni ya juu juu, kwa sababu sera zote kuu huamuliwa na Marekani. Sera ya Marekani inatabikishwa na kikundi kilichochaguliwa ndani ya uongozi wa kijeshi. Ingawa kikundi hiki cha kijeshi kinafanya kazi kama mlinzi wa maslahi ya Marekani, nafasi hutolewa kwa uongozi wowote wa kisiasa ambao uko kwenye ukurasa huo huo, ulioandikwa na Washington. Mikutano, vikao na maandamano yamo ndani ya mitindo inayovumiliwa, mradi tu mistari-mekundu isivukwe, hata kwa neno moja. Ama kuhusu uchaguzi katika Demokrasia, ni upotezaji juhudi, wakati na pesa, unaolenga tu kujenga imani ya umma kwa uongozi mpya wa kisiasa unaounga mkono Amerika. Ndiyo maana mnamo tarehe 12 Disemba 2012, kabla ya uchaguzi wa 2013, Balozi wa Marekani wa wakati huo, Richard Olson, alitangaza kwa ujasiri, "Farasi wetu ni demokrasia." Enyi Waislamu, mabadiliko ya kweli yatakuja tu baada ya kuhakikisha kuondolewa kwa mfumo wa Demokrasia ulioletwa kutoka nje, kwa kujitahidi kusimamisha Khilafah Rashida badala yake. Mabadiliko ya kweli yatakuja wakati ambapo majeshi ya Pakistan yatasimama na Waislamu, dhidi ya wakoloni wa kigeni na washirika wao wa ndani, kwa kutoa Nusra kwa ajili ya kusimamishwa tena kwa Khilafah Rashida.

Enyi Waislamu wa Majeshi ya Pakistan, Mashirika ya Maafisa Wastaafu wa Jeshi, Uongozi wa Kisiasa na wenye Ushawishi na Maoni! Demokrasia haiwezi kutupa chochote ila unyonge na utumwa. Demokrasia kamwe haiwezi kutoa uhuru kutokana na ukoloni. Demokrasia inahakikisha maangamivu yetu ya kijiografia na kiuchumi mikononi mwa IMF na FATF. Demokrasia inamwokoa jasusi muuaji wa India, Kulbhushan Jadhav, kutokana na kunyongwa. Demokrasia inazuia uhamasishaji wa vikosi vyetu vya kijeshi kwa ukombozi wa Kashmir, na kumuongezea Modi kiburi chake. Demokrasia ilihakikisha kuajiri uwezeshaji wa kuinasa Taliban, ndani ya wavu wa mfumo wa Kimarekani, kupitia Makubaliano ya Doha. Demokrasia ilitoa usafiri salama kwa Waamerika waoga, walipoondoka kwa haraka kutoka Kabul. Demokrasia huweka Njia ya Mawasiliano ya Anga ya ‘The Boulevard’ wazi, juu ya vichwa vyetu, ili droni za kijeshi za Marekani ziweze kuwasha moto wa fitina kwenye Laini ya Durand.

Mabadiliko ya kweli ni kupitia tu kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume pekee. Msimuogope yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt) na tembeeni pamoja na uongozi wa kisiasa wa Hizb ut Tahrir ili kuisimamisha. Simamisheni Khilafah itakayowaunganisha Waislamu kutoka Indonesia hadi Morocco kama dola moja yenye nguvu, na kupindua mipango ya wakoloni makafiri. Tembeeni sasa pamoja na uongozi wa kisiasa wa Hizb ut Tahrir, uliofanya maandalizi kamili kwa ajili ya utabikishaji wa kivitendo wa Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 [وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا]

“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Surah Al-Ahzab 33:36].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu