Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  12 Rabi' I 1443 Na: 1443 / 17
M.  Jumanne, 19 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mapenzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) Yahitaji Kusimamishwa kwa Khilafah kwa Njia ya Utume

(Imetafsiriwa)

Mwezi wa Rabi ul-Awwal ni mwezi uliobarikiwa ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikuja hapa ulimwenguni. Ni wajibu kumpenda Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kumtanguliza (saw) kwanza juu ya kila jambo la kidunia, kwani ni wajibu kumtii (saw). Mwenyezi Mungu (swt) katika Surah At-Tauba, Ayah 24 amesema,

 [قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَآؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللّهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُواْ حَتَّى يَأْتِيَ اللّهُ بِأَمْرِهِ وَاللّهُ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ]

“Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.” Kwa hivyo, nini maana ya mapenzi kwa Mtume (saw)? An-Nawawi amesimulia maana ya mapenzi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kutoka kwa Sulayman ibn al-Khattabi katika maelezo yake kuhusu Muslim, ambayo yanasema, "لا تصدُق في حبي حتى تفني في طاعتي نفسك، وتؤثر رضاي على هواك، وإن كان فيه هلاكك"  "Huwezi kuwa mkweli katika mapenzi yangu isipokuwa ujitume kwa kunitii mimi na uweke radhi zangu mbele ya matamanio yako mwenyewe, hata ikiwa itakugharimu maisha yako." Kwa hivyo, mapenzi kwa Mtume (saw) leo hayawezi kuonyeshwa kupitia maneno matupu ya serikali ya 12 Rabii 'al-Awwal, mipangilio ya taa zinazong'ara ng'ara na domo tupu la likizo ya umma, bali kwa kupitia tu kusimamishwa kwa Khilafah kwa Njia ya Utume.

Enyi Waislamu na Watu wao wanaomiliki Nguvu! Leo Waislamu kote ulimwenguni wako katika rehema ya makafiri, katika hali ya umaskini na udhalilishaji kwa sababu ya mfumo wa Magharibi, huku watawala wao wakijifakhiri kuwa washirika wa maadui makruseda. Wakati heshima ya Mtume (saw) inachafuliwa kwa kuungwa mkono na dola za wakoloni wa Magharibi, watawala hawa wanakataa kumfukuza hata balozi mmoja, achilia mbali kuhamasisha vikosi vyetu vya majeshi ili mikono na ndimi ovu zikatwe. Hata baada ya kuona masaibu ya wale wanaompenda Mtume (saw) katika nchi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu, watawala wetu wanawafunga minyororo vikosi vyetu kambini mwao. Kwa kuzingatia hali hizi zote, mapenzi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) yahitaji kwamba nyinyi, kwa kumtii Nabii wenu kipenzi (saw), muwapindue watawala wasaliti wa sasa. Ni hapo tu ndipo mtakaporudisha nguvu ya umoja wa kisiasa, kupitia kurudisha Khilafah ambayo itairithi kikweli Dola ya Kiislamu  aliyoianzisha Mtume (saw) mjini Al-Madina Al-Munawwarah. Hakika mapenzi ya Mtume wetu (saw) yanastahili zaidi kuliko mapenzi ya ulimwengu huu, watu wote waliomo ndani yake, biashara zetu na hadhi yetu. Lazima tushinde kila kikwazo na kuikumbatia kila hatari ili kumtii yeye (saw). Hili ndilo litakalotutumikia kikweli Siku ya Kiyama mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), in shaa Allah na kutuleta karibu naye (saw) kesho Akhera. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ» “(Kesho Akhera) utakuwa pamoja na yule umpendae.” (Bukhari na Muslim).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu