Jarida la UQAB Toleo 90 - Julai 2024
- Imepeperushwa katika Jarida la UQAB
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Julai 2024 M.
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Julai 2024 M.
Serikali ya Marekani, kupitia taasisi za kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, inalenga kupata ushindi madhubuti. Ni ushindi ambao haikuweza kuupata, licha ya zaidi ya miaka ishirini ya vita dhidi ya Uislamu na Mujahidina nchini Afghanistan. Utafutaji ushindi huu ulianza pale Marekani ilipoiruhusu Qatar kuwa mwenyeji wa vuguvugu la Taliban, na kufungua afisi kwa ajili ya vuguvugu hilo huko Doha mwaka 2013. Kupitia afisi hii, Marekani ilijihusisha kisiasa na harakati hiyo, na kusababisha duru kadhaa za mazungumzo yaliyohusisha Marekani na waamuzi, ukiwemo ujasusi wa Pakistan.
Mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 6 Juni 2024, kongamano la vikosi vya kisiasa vya kiraia vya Sudan lilizinduliwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo, katika jaribio jipya la Misri kumaliza vita vinavyoendelea nchini Sudan. Waangalizi wanaamini kuwa jaribio hili linaweza kuweka msingi wa mazungumzo mapana, huku wengine wakipuuza umuhimu wa mafanikio ambayo linaweza kufikia. (Al-Araby Al-Jadeed).
Kenya, imekumbwa na maandamano makubwa katika masiku ya hivi majuzi baada ya bunge kupitisha mswada wa kuongeza ushuru – ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kila siku kama vile mafuta ya kupikia, nepi, na mkate – kwa idadi ya watu ambao tayari wanakabiliwa na mfumko wa bei na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira. Rais Ruto alikataa kutia saini mswada huo baada ya maandamano makubwa ambayo kufikia sasa watu 39 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Jana, Jumamosi, tarehe 6 Julai 2024, lile linaloitwa Kongamano la Kisiasa na Majeshi ya Kiraia ya Sudan lilifanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo; nukta muhimu katika taarifa ya mwisho zilizotolewa zilikuwa: “...wanakongamano pia walisisitiza ulazima wa kushikamana na Azimio la Jeddah na kuzingatia taratibu za utekelezaji na maendeleo yake ili kuendana na maendeleo katika vita…
Katikati ya uungaji mkono wa Marekani na Uingereza kwa mauaji yanayofanywa na umbile la Kiyahudi, ambalo liliasisiwa na Himaya ya Uingereza yenyewe, na baada ya zaidi ya miezi tisa ya uungaji mkono wao kwa umwagaji damu wa Waislamu mjini Gaza, kampeni za uchaguzi wa rais na chama zinaendelea hivi sasa nchini Marekani na Uingereza.
Kwa imani thabiti na kujisalimisha kikamilifu kwa Qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir/Kenya inaomboleza kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla, na haswa watu wa Kenya; Seif Omari Mwaruwa
Ili kuonyesha uaminifu wake usioyumbayumba kwa India, Hasina aliondoka bila kuchelewa hadi New Delhi (Juni 21, 2024) kukutana na Waziri Mkuu mpya aliyechaguliwa wa India. Katika ziara hii, Hasina alitia saini Mikataba 10 ya Maelewano (MoU) kwa ajili ya India.
Huku vita vya mauaji ya halaiki vya umbile la Kiyahudi, kwa uungaji mkono muovu wa Marekani ya Magharibi, vikiendelea dhidi ya watu wa Gaza kwa zaidi ya miezi mitano, na wahanga wake kufikia zaidi ya mashahidi na majeruhi 100,000, pamoja na kuangamizwa kwa sehemu kubwa ya majengo yake, kuna mazungumzo mengi kuhusu miradi ya massuluhisho ya kile kitakachokuja baada ya vita vya Gaza na jinsi mambo yatakavyokuwa kisiasa kulingana na mipango ya dola za kikoloni zikiongozwa na Marekani.