Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  2 Sha'aban 1445 Na: 1445/20
M.  Jumatatu, 12 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa nini Rafah Inapigwa Mabomu na Kuzingirwa na Serikali ya Misri?!
(Imetafsiriwa)

Katika matangazo ya moja kwa moja kwenye Chaneli ya Al Jazeera mnamo Jumatatu asubuhi, Februari 12, 2024, msemaji wa Wizara ya Afya, Ashraf al-Qudra, alizungumza na Al Jazeera akielezea uharibifu uliotokea huko Rafah na nyumba zilizolipuliwa, ambazo zilikuwa zinakaliwa na wakaazi na watu waliohamishwa makao yao. Huu ni mfano unaoonyesha ukubwa wa maafa yanayoweza kutokea iwapo Rafah ingevamiwa na jeshi linaloikalia kwa mabavu. Kwa mujibu wa ripoti za kimataifa, kuna zaidi ya watu milioni 1.4 waliokimbia makaazi yao huko Rafah, ambayo ina maana kwamba operesheni yoyote ya chini inaweza kusababisha maelfu ya mashahidi. Kisha, mkurugenzi wa hospitali ya Kuwait huko Rafah alizungumza juu ya majeraha mabaya waliyopata, ambayo hawawezi kushughulikia, na wote ni raia waliotengwa, wakiwemo watoto, wanawake, na wazee, pamoja na zaidi ya mashahidi 67. Alisisitiza uhaba wa rasilimali na kwamba misaada imesitishwa kuingia Rafah tangu Alhamisi, Februari 8, 2024, ambayo ni siku tano zilizopita, na kuthibitisha kuwa watu wa Palestina wanakufa kwa njaa, baridi, hofu, magonjwa ya milipuko na uhaba wa dawa.

Yanayotokea sasa huko Rafah, umbali wa kidogo tu kutoka mpaka na Misri, yanatisha. Mji huu wa mpakani unapokea misaada na usaidizi mwingine kupitia Misri. Mlengo wa matukio haya, sanjari na kuwepo kwa mjumbe wa Marekani katika eneo hilo na mkataba uliofadhiliwa na Marekani kubadilishana wafungwa, unaashiria jaribio la kuwashinikiza wanamgambo waliomo ndani kulikubali, kulitii, na kupunguza matakwa yao ili kuwiana nalo. Hii inaweza kuwa kile mkuu wa ujasusi wa Misri alidokeza katika onyo lake na kuwataka kukubali makubaliano ya kubadilishana wafungwa ndani ya wiki mbili. Kwa hiyo, kuzingirwa kwa nguvu na mashambulizi ya mabomu yanalenga kuwalazimisha kupunguza madai yao kwa kile ambacho Waisraeli wanakubali, na kupata ushindi wa kimaadili wanaotafuta au labda kukidhi kiu yao kwa damu ya watu wetu katika Ardhi Takatifu.

Yanayotokea kwa watu wetu katika ardhi hiyo iliyobarikiwa ni uhalifu kamili, unaohusisha jumuiya ya kimataifa inayounga mkono umbile la Kiyahudi na watawala wa nchi zetu ambao ni walinzi halisi wa umbile hili. Wanalipatia njia zote za uhai na wanazuia Ummah na majeshi yake kutokana na kuling'oa kwa mikono mitupu. Umbile hili halina sifa za kustahamili Umma mtukufu wa Kiislamu. Vipi basi ikiwa majeshi yake yangekombolewa kutokana na minyororo ya watawala waovu na kusonga kuikomboa? Majeshi yetu yote yanatamani hili na yanatamani wote bila ya ubaguzi, hasa tukiangazia jeshi la Kinana kuwa ndilo lililo karibu zaidi, lenye uwezo zaidi, na linalostahili zaidi hili. Tunajua hasira inayowaka ndani ya nafsi, zilizozuiliwa na serikali.

Enyi Wanajeshi wa Kinana: Hasira ya haki inayotokea ndani yenu lazima iwe moto mkubwa unaowateketeza wale wanaokiuka ardhi za Uislamu, wanaonajisi maeneo matakatifu, na wanaokiuka matukufu. Ni lazima izizunguke njama zote za Kimagharibi dhidi ya Ummah na majaribio yake ya kutatua masuala yake kwa kuanzisha miradi yake ya kikoloni katika nchi zetu, kimsingi kupitia kuwepo kwa umbile la Kiyahudi, ambalo linachukuliwa kama kambi ya kijeshi ya hali ya juu kwa nchi za Magharibi katika ardhi zetu. Moto huu unapaswa kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kusababisha kuanzishwa kwa Ummah ulioungana na kuregeshwa kwa ubwana wake na serikali yake upya. Ni lazima umchome mtu yeyote anayesimama baina ya Ummah na kukombolewa kwa matukufu yake na kuregeshwa kwa ubwana wake kutoka kwa watawala madhalimu, vibaraka wa Magharibi katika nchi zetu, na wale wote wanaowasaidia, wakiwemo wasomi wao na wapangaji njama wao. Huu ni wajibu wenu, enyi askari wa Kinana, na matokeo ya hasira zenu zilizokandamizwa yanapaswa kuwa kupinduliwa kwa utawala wa Kimagharibi unaotawala nchi zenu na kuzifedhehesha, na tangazo la uungaji mkono wenu kwa Mashababu wa Hizb utTahrir wanaofanya kazi kwa ikhlasi, wanaojitolea kwa ajili ya kusimamisha tena Uislamu chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kupitia nyinyi, dola itaibuka ambayo itarudisha adhama na heshima ya Ummah, itakusanya majeshi yake ili kuwanusuru watu wa ardhi iliyobarikiwa na nchi nyenginezo za Kiislamu, na wale wote wanaokandamizwa duniani. Huu ni wajibu wa Ummah na kazi ya majeshi yake: kuupeleka Uislamu na uadilifu wake kwa ulimwengu kuwa ni ujumbe wa uongofu na nuru. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akufanyeni muwe ni wabebaji wa ujumbe huu na watu wake.

Enyi Wanajeshi wa Kinana: Wajibu wenu sio kuwashinikiza watu wa Gaza na wapiganaji miongoni mwao kukubali masuluhisho ya Magharibi na kuamiliana na washirika. Msiwe chombo mikononi mwao cha kuendeleza miradi yao na kuwazingira watu wenu katika ardhi iliyobarikiwa, na kuwalazimisha kukubali mikataba yenye sumu na masuluhisho yenye maangamivu, ambapo damu ya mashahidi inauzwa kwa bei nafuu kwenye meza za biashara za wasaliti na vibaraka. Jueni kwamba wajibu wenu, na wajibu wa Ummah wote, ni ukombozi kamili wa Palestina na nusra kwa wanaodhulumiwa, na kuondoa dhulma kutoka kwao. Palestina ni ardhi ya Ummah mzima, na ni wajibu kwa Umma, hasa majeshi yake, na hasa nchi zinazoizunguka, zikiongozwa na jeshi la Kinana, kuikomboa. Mko wapi wajibu huu? Je! hamtaki kurudisha heshima aliyokusifuni kwayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)? Je! hamutamani heshima ya kuinusuru na kuishindia Dini hii na watu wake?

Enyi Wanajeshi wa Kinana, Enyi wanajeshi bora: Utukufu wa kweli unakuamuruni muwe ngao ya Ummah huu, mukibeba bendera yake. Kwa hivyo, angalieni ni bendera gani munayoibeba na munapigana chini ya uongozi wa nani, ili mujue ikiwa utukufu uko ndani yenu au la. Ili kuurudisha utukufu huu, ni lazima mutupilie mbali minyororo ya watawala madhalimu kutoka shingoni mwenu, mukikatisha mafungamano yote yanayokufungamana nao, na muunganishe mafungamano yenu na wafanyikazi wenye ikhlasi wanaojitahidi kuutabikisha Uislamu na kuunusuru. Wapeni uwezo wa kuanzisha upya maisha kamili ya Kiislamu kupitia dola ya Kiislamu Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ni dola ambayo inaregesha mamlaka ya Ummah, inakusanya majeshi yake kwa ajili ya vita dhidi ya maadui zake, inairudisha ardhi yake na utakatifu wake, na kuwanusuru wanaodhulumiwa kote ulimwenguni. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akujaalieni kuwa wanajeshi na wasaidizi wake. Amin, Ewe Mwenyezi Mungu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu