Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  29 Jumada II 1445 Na: 1445/16
M.  Alhamisi, 11 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jumuiya ya Kimataifa Haijanyanyuka, na Haitanyanyuka!

Kwa hivyo Jeshi la Kinana liko wapi Kuwanusuru Ndugu zetu, Bwana Waziri wa Mambo ya Nje?!
(Imetafsiriwa)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, wakati wa mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Ujerumani uliofanyika mnamo Jumanne, Januari 9, 2023, alisema: "Ikiwa mtoto mmoja amejeruhiwa, ilitarajiwa kwamba jumuiya ya kimataifa itakimbilia kuwanusuru na kuwalinda. Watoto elfu kumi wanayo wamepoteza maisha yao, huku wengine bado wakiwa chini ya kifusi, na jumuiya ya kimataifa haiwezi kudai kabisa kusitisha mapigano na kisha kushughulikia maswala mengine." Alisema pia, "Kuwasikiliza watoto ambao wamepoteza familia zao na mateso yao ni katika kiwango kile kile cha kibinadamu ambacho ulimwengu lazima ushughulikie, sawa na jinsi inavyoshughulikia suala la wafungwa." (Mtandao wa Al-Shorouk)

Jumuiya ya kimataifa, kama ilivyotajwa na Waziri, ni mshirika anayehusika katika uhalifu wa umbile la Kiyahudi, na inajua vizuri hili. Kwa kuongezea, serikali za Kiarabu ambazo uwepo wake unasaidiwa na jamii ya kimataifa ni sehemu ya njama na washirika katika uhalifu wa umbile hilo. Wao ni kama walinzi na watetezi wa umbile hili dhidi ya hasira ya watu na majeshi. Marekani, inayoongoza mfumo, inathibitisha hili. (Wizara ya Ulinzi ya Mayahudi ilisema mnamo Jumatano, Disemba 6, 2023, kwamba idadi ya ndege 200 za Marekani zilikuwa zimewasili nchini 'Israel' zikiwa zimesheheni vifaa vya Kimarekani, silaha, na magari ya kivita. Wizara hiyo iliongezea katika nukuu ya tweet kwenye wavuti wake rasmi kwamba ilikuwa imepokea zaidi ya tani 10,000 za silaha na vifaa vya Marekani tangu mwanzo wa vita vya 'Israel' juu ya Gaza, yakiwemo magari ya kivita, silaha, vifaa vya kinga ya kibinafsi, vifaa vya matibabu, risasi, na nyengine nyingi. Tangu kuanza kwa vita,  Rais wa Marekani Joe Biden amesisitiza katika hotuba ya runinga msaada kamili wa nchi yake kwa 'Israel,' akielezea utayari wake wa kutoa msaada wote wa kijeshi unaohitaji.) (Al Jazeera Net, 12/06/2023)

Marekani, inayozingatiwa kuwa kiongozi wa jamii ya kimataifa iliyotajwa na Waziri, imeanzisha daraja la ndege kati yake na umbile vamizi, ikitoa mahitaji yote ya uhai wake, moja kwa moja au kupitia vibaraka wake kati ya watawala wa nchi zetu. Licha ya kuwa maelfu ya maili mbali na umbile hilo, ikitenganishwa na bahari, imeongeza msaada wake. Hivyo, jeshi la Kinana liko wapi na msaada wake kwa watu wa Palestina, Bwana Waziri? Ni nguvu iliyo jirani na Ardhi Iliyobarikiwa, iliyoaminiwa ukombozi wake kama ilivyoamriwa na Mwenyezi Mungu kwani Palestina yote ni ardhi takatifu inayomilikiwa na Ummah. Jukumu la ukombozi linaangukia juu ya Umma wote, na linafungamana sana na nchi zinazoizunguka, na Misri ikiwa mbele na jeshi lake kali katika eneo hilo. Wanawake, watoto, na wazee wa Palestina wamekuiteni, basi muko wapi na yako wapi majeshi na vifaa vyenu vilivyo jaa kutu?!

Jumuiya ya kimataifa haijanyanyuka, Bwana Waziri wa Mambo ya nje, na haitanyanyuka. Ni nini kinachozuia uasi wa jeshi la Kinana, na wako wapi kujibu maneno ya Mpalestina huyu kwa mjukuu wake, “Mwambie Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwamba Waislamu wametutelekeza”? Ndio, majeshi ya Ummah yamewatelekeza, wanasonga tu kuukandamiza uasi wa watu na kulinda viti vya watawala waliozongwa na ufisadi. Damu ya watu wa Palestina haijawachochea, na mishipa yao haijapata hasira wakati runinga zinaonyesha picha za kutisha, kunakili matukio ambapo Umma na majeshi yake wamewabwaga, usaliti unaochujua uso!

Jukumu la kweli ni kuwasaidia watu wa Ardhi Iliyobarikiwa kwa aina zote za msaada, kuondoa mipaka ambayo inatenganisha Misiri na Ukanda wa Gaza na Palestina yote. Inajumuisha kutangaza uhamasishaji jumla, kupeleka jeshi la Misri kuwanusuru na kuwalinda, na kuwatetea. Hili ndio jukumu, Bwana Waziri wa Mambo ya nje, na hakuna kitu kinacholazimika au kinachostahili kuliko hili. Ikiwa Jeshi la Kinana halitasonga, basi ni jukumu la Wamisri wote kutoka kwenye viwanja vya umma, kuwachochea askari wa jeshi la Kinana, na kuwatia moyo kutimiza wajibu uliowekwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwanusuru watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa na kuikomboa ardhi yote ya Kiislamu. Kabla ya hilo, inajumuisha kuondoa kitu chochote kinachoweza kuwazuia kutokana na kazi hii na kusimama katika njia ya kuikomboa ardhi yetu iliyobarikiwa na kuling’oa umbile la Kiyahudi.

Enyi askari wa Kinana! Mnalalaje huku utukufu wa Israa wal Miraj ya Mtume wenu ukinajisiwa na Mayahudi?! Mnalalaje, mnakulaje na kunywaje na ilhali wanawake wa Palestina wanakuombeni msaada wenu, wakituma maombi kwenu mmoja baada ya mwengine? Je! hamna maji kwenye nyuso zenu au damu kwenye mishipa yenu?! Iko wapi imani yenu, ujasiri wenu, na fahari yenu?! Wallahi, kunyamaza kwenu ni kosa na fedheha, na mtawajibika mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kimya hiki na kwa damu hiyo. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alilalamika kuhusu nyinyi kwa Mola wake Mlezi, basi mtajibu vipi?

Wallahi, starehe zote za dunia hazina thamani ukilinganisha na dakika moja kwenye moto wa Jahannam, vipi kuhusu kuwa milele ndani yake? Jikomboeni kutokana na utawala huu unaosimama kati yenu na kuling'oa umbile lililopotoka, kuwanusuru watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa.

Enyi askari wa Kinana, askari bora! Kheri yenu umefungamana na kutimiza wajibu alioweka Mwenyezi Mungu juu yenu kuulinda Uislamu, itikadi yake, sheria zake, ardhi yake, na matukufu yake. Kuweni kweli askari bora, rudisheni urithi adhimu wa mababu zenu kama vile Salah al-Din na Qutuz. Anzeni misheni yenu kwa kuung’oa utawala huu unaokuleteeni aibu na udhalilifu, huku ukitumieni kulinda usalama wa Mayahudi. Itangazeni kuwa ni ghadhabu kwa Mwenyezi Mungu, ing'oeni kutoka kwenye mizizi yake, na zana zake zote, wasimamizi wake, na sera zake, na kila kitu kinachotokana nalo. Simamisheni dola kwa ajili ya Uislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, yenye kutangaza uhamasishaji wa kuikomboa ardhi yote ya Kiislamu na kuwanusuru wanaodhulumiwa kila mahali, sio tu katika Ardhi Iliyobarikiwa pekee, ingawa inaanzia hapo.

Enyi askari wa Kinana, hasira zenu na ziwe ni ishara inayosimamia ukweli kwa maneno ya Mwenyezi Mungu na kukata njia ya wahalifu.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Surat Al-Anfal:74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu