Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  18 Jumada I 1445 Na: 1445/13
M.  Jumamosi, 02 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Umbile la Kiyahudi Linaregelea Mauaji ya Watu Wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Huku Maelfu ya Wanajeshi Wetu Wakizuiliwa ndani ya Kambi Zao!!
(Imetafsiriwa)

Utawala wa Firauni wa Misri, uliosaidiwa na kuungwa mkono na watawala wa Qatar, iliibuka na kuchukua hatua, chini ya maagizo ya bwana wa umbile la Kiyahudi, na bwana wa Firauni wa Misri, kinara wa ukafiri, Marekani. Walihamasisha "kuwakomboa" wafungwa wa Kiyahudi. Hii ni wakati miongo kadhaa imepita, ambayo idadi ya wafungwa wa Kiislamu nchini Palestina, imefikia zaidi ya elfu nane. Zaidi ya hayo, Mayahudi bado wanawafunga Waislamu kadhaa kila siku. Ilhali, hili halijamgusa hata chembe raisi wa serikali ya Firauni ya Misri. Serikali wala wasemaji wake hawajatamka neno hata moja, ikitaka mwisho wa, au hata kukemea, utumwa wa watu wa Ummah huu. Hii ni huku ikiuthibitishia ulimwengu kwamba haitapumzika hadi waachiliwa huru watu kadhaa wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirika. Ni ishara wazi kwamba Firauni wa Misri ni wa jinsi moja na wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirikia, na yeye ni mwaminifu kwao. Anawachukulia mateka wao kama wanadamu, huku akiwachukulia mateka wa Waislamu kama mawe! Utawala huu iko mbali na kuwa mtiifu kwa Mwenyezi Mungu (sw) na Mtume Wake Mtukufu (saw), ambaye haongei kutoka kwa matamanio ya kibinafsi, lakini kwa wahyi peke yake. Yeye (saw) alituamuru kuwakomboa wafungwa wa Kiislamu, kwani yeye (saw) amesema,

«فُكُّوا الْعَانِيَ، وَأَطْعِمُوا الْجَائِعَ، وَعُودُوا الْمَرِيضَ»

“Waacheni huru mateka, na walisheni wenye njaa, na watembeleeni wagonjwa.” [Bukhari]

Baada ya serikali ya Misri, pamoja na Qatar, kumaliza juhudi zao za "kuwakomboa" wafungwa wengi wa Kiyahudi kama walivyoweza, umbile la Kiyahudi lilianza tena mauaji yake. Lilimwaga damu ya watu wetu na majirani zetu, chini ya pua na macho ya jeshi letu. Jeshi letu haliko mbali na upeo wa dola ya Kiyahudi. Kwa kuongezea, dola ya Kiyahudi iko ndani ya masafa ya mizinga yetu, bunduki, na ndege zetu, ambazo zote ni hazina ya silaha za Ummah kwa kuanzia, na hatumkabidhi tu mtu yeyote. Kwa hivyo, hairuhusiwi kwa jeshi letu kukosa fursa hii. Lazima lirekebishe mapungufu yake ya sasa, na yale ya miongo minane iliyopita, kuhusiana na uvamizi wa Mayahudi kwa Ardhi Iliyobarikiwa. Lazima lifidie upuuzaji wake kwa watu wetu huko Gaza wakati huu. Ikiwa halitafanya hivyo, jeshi hili litakuwa katika hali sawa na ile ya jeshi la Firauni wa Misri, kwa kuingia katika madhambi na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ]

“Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.” [Surah Al-Qasas 28:8].

Sisi tunajua kwa hakika kuwa ndani ya vikosi vyetu kuna wale maafisa na askari, ambao damu yao inachemka kwenye mishipa yao. Wanahamasishwa kulipiza kisasi damu ya ndugu zao huko Gaza, na katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Tunajua kuwa wana nguvu zaidi kuliko Mujahidina, ambao walizika kiburi cha umbile la Kiyahudi mchangani, mnamo Oktoba 7. Hata kama walikuwa sawia na mashujaa 7 Oktoba katika Iman, wao ni mara maelfu kadhaa kwa idadi na vifaa. Zaidi ya hayo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِذَا فَتَحَ اللهُ عَلَيْكُمْ مِصْرَ فَاتَّخِذُوا فِيهَا جُنْداً كَثِيفاً، فَذَلِكَ الْجُنْدُ خَيْرُ أَجْنَادِ الْأَرْضِ، فَقَالَ لَهُ أَبُو بَكْرٍ: وَلِمَ ذَلِكَ يَا رَسُولَ اللهِ؟ قَالَ: لِأَنَّهُمْ فِي رِبَاطٍ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ»

“Pindi Mwenyezi Mungu atakapokufungulieni Misri, pelekeni jeshi kubwa huko. Jeshi hilo ni bora zaidi ardhini. Kisha Abu Bakar akamuuliza, ‘Kwa nini hivyo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ Akasema (saw), ‘Ni kwa sababu wao watakuwa katika kuihami mipaka (ribaat) mpaka Siku ya Kiyama.” Pia hairuhusiwi kwa yeyote aliye katika ribaat kushusha silaha zake, vyenginevyo atachukuliwa kuwa mithili ya yule aliyekimbia vita, wakati vita vinaendelea. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفاً فَلَا تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ * وَمَنْ يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفاً لِقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزاً إِلَى فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِنَ اللهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ]

“Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru vitani msiwageuzie mgongo. (15) Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu. (16)” [Surah Al-Anfal 8:15-16].

Kwa hivyo jihadharini, Enyi askari wa Kananah, isije hatima yenu ikawa kama hatima ya wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirikia, na wale ambao makao yao ni Motoni. Badala yake, kuweni miongoni mwa wale ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliwataja katika Hadith tukufu, hata bila ya kukutana nao. Jueni kuwa jihad yenu katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) sio wazimu wala ushabiki. Badala yake, ni utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt), kujikurubisha naye, na kutarajia Pepo yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

«رِبَاطُ يَوْمٍ فِي سَبِيلِ اللهِ خَيْرٌ مِنْ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَمَوْضِعُ سَوْطِ أَحَدِكُمْ مِنَ الْجَنَّةِ خَيْرٌ مِنْ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَالرَّوْحَةُ يَرُوحُهَا الْعَبْدُ فِي سَبِيلِ اللهِ أَوْ الْغَدْوَةُ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا»

“Kuchunga na kulinda mipaka (Ribaat) kwa siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko dunia na vilivyomo ndani yake. Na sehemu katika Pepo iliyo na udogo mithili ya mchapo wa farasi ni bora zaidi kuliko dunia na vilivyomo ndani yake. Na vita mja anavyotoka kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu jioni au asubuhi ni bora zaidi kuliko dunia na vilivyomo ndani yake.” [Bukhari na Muslim]

Enyi wale ambao tunawachukulia kuwa miongoni mwa askari bora duniani! Hizb ut Tahrir ni kiongozi asiyewadanganya watu wake. Inawataka mutie hofu ndani ya adui. Hatuwaombi hili kwa majirani na kaka zenu peke yake, lakini pia kwa familia zenu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Wanajua kuwa munao uwezo wa kutia hofu kwa adui. Kwa hivyo, toeni Nusrah kwa Hizb ut Tahrir ambayo inakuongozeni kuipindua serikali ya Firauni wa Misri, ambaye ndiye asili ya maumivu ya watu wa al-Kinanah. Hivyo simamisheni, pamoja na Hizb, Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume, ambayo Mtume wetu Mtukufu (saw) alitupa kwayo bishara njema, pindi yeye (saw) aliposema, «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume.” [Ahmad] Ni Khilafah ndiyo itakuongozeni kuwakomboa wafungwa na mateka. Italipiza kisasi cha wanawake wasafi wa Kiislamu, waliofiwa, mayatima, na wale wanaosujudu, ambao wamedhulumiwa na ndugu za nyani na nguruwe. Kwa hili pekee, dhambi zenu zitasafishwa, huku mkiokolewa kutokana na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ]

“Kwa mfano wa haya nawatende watendao.” [Surah As-Saffat 37:61]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu