Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  23 Rajab 1444 Na: 1444/10
M.  Jumanne, 14 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Palestina Inakombolewa kwa Majeshi, Sio kwa Makongamano na Sheria ya Kimataifa
(Imetafsiriwa)

“Wakati umewadia wa amani...” Risala za Al-Sisi kutoka kwa Kongamano wa Kuinusuru Al-Quds, chini ya kichwa hiki Gazeti la Al-Dustour liliandika mnamo Jumapili 12/2/2023, kuwasilisha kile lilichokiita risala za rais wa Misri, ambaye alisema: Kadhia ya Palestina bado ni kipaumbele kwa Misri na Waarabu. Akielekeza hotuba yake kwa Wapalestina, alisema: “Kufikia azma yenu halali ya kusimamisha dola yenu na Al-Quds (Jerusalem) Mashariki kuwa ndio mji mkuu wake, na tunasalia kuunga mkono ukakamavu wenu huko Al-Quds na pembe zote za Palestina.” Al-Sisi ameongeza kuwa anaelekeza hotuba yake kwa umbile la Kiyahudi, serikali na watu, na anasema kuwa wakati umefika wa kuendeleza utamaduni wa amani, kuishi pamoja na hata ushirikiano kati ya watu wa eneo hilo. Kwa madhumuni haya, tumenyoosha mikono yetu na Mpango wa Amani wa Waarabu, ambao unahakikisha kwamba hili litafikiwa kwa mujibu wa muktadha wa kina wa haki. Kwa hivyo, tuiweke pamoja katika kuitekeleza kivitendo na tufungue ukurasa wa matumaini kwa vizazi vijavyo vya Wapalestina na Mayahudi vile vile. Aliendelea: Misri inaonya tena juu ya matokeo mabaya yanayoweza kutokea kutokana na kukiuka hili au kujaribu kuzuia au kulazimisha yale ambayo tayari yameshafanywa ambayo yanaathiri vibaya upeo wa mazungumzo ya hadhi ya mwisho kati ya pande za Palestina na (Israel).”

Kongamano hili linalenga kuiweka pembeni kadhia ya Palestina na kuelekeza macho ya Waislamu kando nayo, na kuidunisha kuwa mzozo kati ya watu wa Palestina na Mayahudi, kutatuliwa kupitia sheria za kimataifa na Umoja wa Mataifa, na kujaribu kulioanisha umbile lemavu katika eneo hili na kufikia uhalalishaji wake kwa watu. Wazo hili ni ndoto ambayo haiwezekani kufikiwa, ushahidi bora zaidi kwa hili ni kushangilia kwa watu katika kila janga linalowapata Mayahudi na kila operesheni ya mmoja wa mashujaa wa Palestina ambayo majeraha ya Mayahudi ni mabaya, hata mashabiki wa mpira wa miguu waliokuwa wametengwa (na Palestina) na watawala, waliimba viwanjani kwa ajili ya Palestina na watu wake. Hii ndiyo hisia jumla miongoni mwa Ummah kwamba kama lau ungepata mwanya, ungeling'oa umbile hili kwa mikono yake mitupu.

Tulisema na tukarudia, pengine baadhi hujifunza kutokana na kurudia rudia: Suala la Palestina si mahususi kwa watu wa Palestina pekee, bali ni suala la Ummah mzima kwa jumla. Al-Aqsa ni Qibla cha kwanza kati ya vibla viwili na ya watatu ya Misikiti Miwili Mitukufu. Ni eneo la Al-Isra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na kukombolewa kwake na kulindwa ni wajibu kwa Ummah mzima, hasa zile zinazoitwa nchi za pete, hususan Misri.

Enyi Wenye Ikhlasi wa Jeshi la Kinana: Nyinyi ni kizazi cha wakombozi wakubwa kama Salah al-Din al-Ayyubi, Mwenyezi Mungu amrehemu, mshindi wa Makruseda na mkombozi wa Al-Aqsa. Ni aibu kwenu kuona Al-Aqsa inanajisiwa mukiwa hai, na katika mojawapo ya kazi muliyokabidhiwa na watawala vibaraka wenu ni kuwalinda wale walioinyakua ardhi yenu, wakayanajisi matukufu yenu, na kukiuka matukufu yenu, hivi ni aibu gani inakupateni wakati huu umekuwa ndio uhalisia wenu?! Ni damu gani hii inayopita kwenye mishipa yenu?! Uko wapi utukufu wenu, na iko wapi hasira yenu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Dini yake, Shariah yake, na matukufu yake?! Mutakutana vipi na Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal ilhali haya yote yanautokea Ummah wenu mbele ya macho yenu huku mukiwa kimya?! Je, hamupendi Mwenyezi Mungu akusameheni kwa yale mliyoyafanya huko nyuma na kuyabadilisha maovu yenu kwa mema?!

Je, sio wajibu wenu kuinusuru Dini yenu kwa kuwang'oa watawala hawa wa madhara na kusimamisha dola ya Uislamu; Khilafah Rashida ambayo unarudisha heshima na ukombozi wa Ummah wenu, na inayahamasisha majeshi kuzikomboa nchi zake zote zinazokaliwa kwa mabavu, sio Palestina peke yake. Huu ndio wajibu wenu mtakaoulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Jueni kwamba munakabiliwa na machaguo mawili, na hakuna la tatu. Ama kukaa katika furaha ya watawala wenu ambao bila shaka watapita; kutokana na mishahara, vyeo, nishani, na fadhila ambazo hazitakufaeni kitu kwa Mwenyezi Mungu, bali Mwenyezi Mungu atawafanya kuwa udongo upeperukao, na watakuwa ni laana kwenu na weusi katika vitabu vyenu vya amali. Au muwe upande wa Ummah wenu na kuukomboa kutokana na utawala wa makafiri wakoloni wa Magharibi juu ya rasilimali na mali yake; hiyo ni kwa kuipa Nusra (msaada wa kimada) Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itairegesha Al-Quds yake, matukufu yake, na ardhi yake yote, hivyo msiache yeyote kukutangulieni katika hilo, kwani nyinyi mnastahiki zaidi, enyi wanajeshi watukufu wa Kinana, Mwenyezi Mungu (swt) akupeni ushindi na Misri yenu itakuwa Misri Al-Munawarra.

[رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ]

“Ewe Mola Mlezi wetu! Tuhukumie baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanao hukumu.” [Al-A’raf: 89].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu