Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  2 Rabi' I 1446 Na: HTM 1446 / 06
M.  Alhamisi, 05 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wakati Msambazaji Mkuu wa Silaha Anapozungumza juu ya Usitishaji Vita na Amani, Hakika ni Dhihirisho la Udanganyifu na Unafiki

(Imetafsiriwa)

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Malaysiakini iliripoti mahojiano yake na Balozi wa Marekani nchini Malaysia, Edgard D. Kagan, ambapo alizungumzia, pamoja na mambo mengine, msimamo na sera za Marekani katika Asia Magharibi, haswa kuhusiana na Palestina. Alipoulizwa kuhusu mgongano unaoonekana wa wito wa kusitishwa kwa mapigano na upunguzaji kasi ya ghasia nchini Palestina huku wakati huo huo kukisafirishwa silaha kusaidia ‘Israel,’ Kagan alijibu kwamba Washington imejitolea kukomesha umwagaji damu lakini haiko tayari “kupamba mgongo” kujitolea kwake kwa muda mrefu kwa usalama wa ‘Israel.’ Balozi huyo alisisitiza zaidi kuwa uhusiano wa Marekani na kujitolea kwake kwa ‘Israel’ unaipa uaminifu wa kupatanisha mchakato wa amani katika eneo hilo.

Matamshi ya balozi huyo wa Marekani yanaweza kufasiriwa kuwa, “Tunataka amani Palestina, na tunataka kukomesha mauaji ya Wapalestina kwa kuipatia ‘Israel’ silaha na mabomu kadiri inavyohitaji kuwamaliza Wapalestina na kuangamiza ardhi yote ya Palestina!” Huu ndio ukweli wa msimamo wa Marekani - haifichi tena unafiki wake wa wazi wakati wa kujadili sera zake katika Asia Magharibi. Mshirika wa karibu wa ‘Israel’ na msambazaji mkubwa wa silaha kwa umbile la Kiyahudi sasa anazungumzia usitishaji vita, amani, na kukomesha mauaji nchini Palestina! Je, ni urongo au unafiki gani unaweza kuwa mkubwa kuliko huu? Hakika, Marekani imepoteza sura yoyote ya aibu au akili timamu inapokuja kuhusu Palestina!

Malaysiakini iliripoti kwamba Kagan alihojiwa wakati wa ziara yake katika afisi ya chombo cha habari huko Petaling Jaya. Inashangaza jinsi mtu wa hadhi ya Kagan angeweza kutembelea afisi ya Malaysiakini kwa mahojiano, haswa ikizingatiwa kuwa Malaysiakini sio chaneli ya serikali. Lazima kuwe na kitu “spesheli” kuhusu Malaysiakini ambacho kilihitaji uangalizi wa mwakilishi kutoka mojawapo ya dola kubwa zaidi ya kikoloni duniani kutumika kama jukwaa la kufikisha ujumbe wake kwa wakaazi wa Malaysia!

Wakati wa mahojiano hayo, balozi wa Marekani alipongeza mafanikio ya demokrasia nchini Malaysia na aliwatambua viongozi wa Malaysia ambao wanatambua umuhimu wa ASEAN kwa Marekani. Kama mwakilishi wa maslahi ya Marekani nchini Malaysia, pongezi za balozi huyo zina uzito mkubwa na ziko mbali na maneno ya kawaida tu. Haswa, sifa hii inaelezwa wakati Anwar Ibrahim anashikilia wadhifa wa Waziri Mkuu. Inafaa kukumbuka kuwa wakati wa ziara ya Al Gore nchini Malaysia mwaka 1998, Makamu wa Rais wa Marekani alipongeza waziwazi vuguvugu la mageuzi lililoongozwa na Anwar, akitambua ujasiri wao katika kutetea mabadiliko ya kidemokrasia, jambo ambalo lilileta pigo kubwa kwa utawala wa Mahathir wakati huo. Inaonekana kana kwamba Anwar ana “msimamo spesheli” machoni mwa Marekani.

Ni muhimu kwa Waislamu kuelewa muktadha ulio nyuma ya kusifu kwa Marekani na kuidhinisha demokrasia nchini Malaysia. Kama mtetezi mkuu wa demokrasia duniani kote, Marekani inamuunga mkono kiongozi au nchi yoyote inayokumbatia demokrasia, hasa katika ulimwengu wa Kiislamu. Kinyume chake, Marekani inawataja wale wanaopinga demokrasia, hasa wale wanaotaka kuanzisha dola nje ya mifumo ya kidemokrasia, kuwa ni watu wenye itikadi kali, wenye msimamo mkali au hata magaidi. Kwa hiyo, Marekani inadhihirisha uadui dhidi ya juhudi za kusimamisha Khilafah, taasisi ya kisiasa ya Kiislamu ambayo inaleta tishio kubwa kwa maslahi ya Marekani, pindi itakaposimamishwa. Kwa hivyo, demokrasia hutumika kama ala ya kimkakati ya Marekani kuzuia juhudi zozote za kusimamisha Khilafah. Marekani inafahamu wazi wazi kwamba maadamu Waislamu wanajitolea kwa demokrasia, Uislamu utabaki kuwa hautabikiki, kwani ni Khilafah pekee ndiyo inayowakilisha njia pekee ya Uislamu kutabikishwa kikamilifu.

Marekani itawaunga mkono wale wanaotetea demokrasia na iko tayari kuchukua hatua zote kuhakikisha kuwa Waislamu wanasalia kujitolea kwa demokrasia. Hata sifa ndogo tu kwa demokrasia nchini Malaysia inatosha kwa Marekani kufikisha ujumbe huu: “Hii ndiyo njia moja tu na ya kipekee ya sawa ninayoidhinisha kwa ajili yenu (Enyi Waislamu) kuifuata ikiwa mnatafuta idhini yangu.” Hakika, ni kweli aliyosema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلَنْ تَرْضَى عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ]

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao.” [Al-Baqarah (2): 120].

Hivyo basi, tahadharini, enyi Waislamu! Achaneni na demokrasia, kwani ni njia iliyoidhinishwa na maadui wa Mwenyezi Mungu (swt), haswa Marekani. Zingatieni uhalifu na unafiki ulio wazi wa Marekani, ni jambo la kusikitisha kwamba Malaysia inaendelea katika kudumisha mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara na kukuuza mafungamano ya kirafiki na dola hii ya kibeberu. Tangu Malaysia ilipopata ule unaoitwa “uhuru” na tangu kukaliwa kimabavu kwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, kumekuweko na Mawaziri Wakuu tisa wa Malaysia. Ilihali hakuna hata mmoja, akiwemo Waziri Mkuu wa sasa wa kumi, aliyekuwa na ujasiri wa kumfurusha balozi wa Marekani na kufunga ubalozi wake nchini humu kama jibu kwa dori ya kihalifu ya Marekani nchini Palestina

Kwa kuzingatia dhurufu za ukweli na hukmu za Mwenyezi Mungu, ni wajib kwetu (Waislamu) kuwa na Khalifa aliye mwaminifu na jasiri, ambaye sio tu atawakataza maadui kuweka mabalozi na afisi zao za ubalozi nchini kwetu lakini pia atatekeleza amri ya Mwenyezi Mungu (swt) ya kuwashinda maadui hadi nchi zao ziunganishwe ndani ya Khilafah, kuwalazimisha kusalim amri kwa Uislamu na kulipa Jizyah (kodi ya kila kichwa) kama ishara ya unyenyekevu wao kwa Uislamu. Hivyo basi, kuthibitisha maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَنْ يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ]

“Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii.” [At-Taubah (9): 29].

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu