Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  10 Shawwal 1444 Na: H.T.L 1444 / 11
M.  Jumapili, 30 Aprili 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon Wamzuru Mbunge wa Zamani Elie Ferzli
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon, unaowakilisha Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon, mnamo Ijumaa asubuhi, 28/4/2023, ulimtembelea Naibu Spika wa Bunge na Mwakilishi wa zamani Elie Ferzli, ambapo walijadili hali ya sasa ya kisiasa nchini Lebanon hasa na eneo kwa jumla na tatizo la sasa kuhusu wakimbizi wa Wasyria nchini Lebanon na hatari za kukabiliana na faili hii kwa namna inavyoshughulikiwa kwa sasa ilijadiliwa. Suala la urais na bahati ya majina yaliyowasilishwa pia lilijadiliwa, na kwamba nukta muhimu katika suala hilo, kwa mujibu wa Mwakilishi Mheshimiwa Al-Ferzli, ni kuwepo kwa maelewano juu ya rais, iwe kutoka ndani au pande za eneo. Kisha ujumbe huo ukawasilisha maoni ya Hizb ut Tahrir kuhusu suala la makubaliano ya Saudia na Iran, mzozo wa kijeshi nchini Sudan na athari zake. Mheshimiwa Mwakilishi Al-Ferzli alionyesha kupendezwa na jambo hilo, kwa hivyo ujumbe ukampa maoni ya kina ya kimaandishi ya Hizb.

Ujumbe huo ulisisitiza kuwa Umma wa Kiislamu ni Ummah mmoja, na istilahi au fahamu ya walio wachache haipo katika dola yake. Kwa sababu Umma wa Kiislamu huwasomesha watoto wake kuchunga mambo ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Ujumbe huo ulisisitiza kuwa Lebanon ni sehemu ya Ummah, na msingi ni kwamba uhusiano kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu unatokana na mtazamo huo. Na kwamba Uislamu ni dini, ikijumuisha dola ambayo kwayo Waislamu na wasiokuwa Waislamu waliishi ndani yake kwa miaka mingi bila ya matatizo yoyote makubwa, hadi nchi za Magharibi zilipoingilia kati, zikaikalia na kuigawanya, na kukuuza ushabiki wa kitaifa, kimadhehebu ili kuidhibiti na kudhibiti uwezo wake.

Mwishoni mwa mkutano, Mheshimiwa Naibu aliukabidhi ujumbe huo toleo la tatu la kitabu chake, "Historia Nzuri Zaidi Ilikuwa ni Kesho". Ujumbe uliondoka kwa matumaini ya kuendelea kuwasiliana ili kujadili hali ya kisiasa na kumpatia maoni ya kisiasa ya Hizb mara kwa mara.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu