Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  27 Ramadan 1441 Na: 1441/02
M.  Jumatano, 20 Mei 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka kwa Wanachama wa Hizb ut Tahrir

(مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً)
 Miongoni mwa waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea. Wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo” [Al-Ahzab: 23]

(Imetafsiriwa)

Kwa kuamini Qadhaa na Qadari ya Mwenyezi Mungu, tunaomboleza kwa huzuni kubwa kwa Ummah wa Kiislamu kifo cha mmoja wa wanachama wetu, Ndugu Mirzakhanov Mirzabharum, Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu, aliyefariki kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu siku ya Jumatatu, tarehe 18/5/2020.

Mirzabharum, ambaye alizaliwa mnamo 1973 katika mji wa Khujand nchini Tajikistan, alibeba ulinganizi na Hizb ut Tahrir na kufanya kazi bila kuchoka na kujitahidi kila juhudi kurudisha tena maisha ya Kiislamu katika Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hakuogopa lawama yoyote katika kazi yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Amali za kifikra na za kisiasa za Mirzabharum katika safu za Hizb utTahrir hazikutolewa machoni mwa serikali ya kidhulma ya Tajik; kwa hivyo alikamatwa mnamo mwaka wa 2001 ili kukomesha amali zake. Akaangukia kuwa muathirika wa unyanyasaji wa wakandamizaji na madhalimu, na uvimbe ukajitokeza katika ubongo wake kama matokeo ya ukatili gerezani. Mnamo 2009, alikuwa mlemavu moja kwa moja. Baada ya kutolewa gerezani mnamo 2010, Mirzabharum alitumia wakati wake mwingi hospitalini kutokana na ugonjwa wake.

Lakini, licha ya ugonjwa wake, hakuacha amali zake za Ulinganizi hata kwa muda mchache, na hakuacha Ulinganizi licha ya matembezi yake kufungika katika kiti cha magurudumu. Aliendelea kuwalingania Waislamu wote katika wema na ukweli na alizidisha amali zake wakati akiwa katika hali hii. Kwa sababu hii, mawakala wa madhalimu hawakuacha kumhoji hata wakati yeye alipokuwa katika kiti cha magurudumu, na walimtaka aachane na amali zake na kujaribu kuzuia kazi yake. Lakini, ndugu yetu, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisimama kidete na hakuwainamia wakandamizaji, akisema, "Nitaendeleza ulinganizi wangu na sitoondoka katika njia hii hata nikifa, fanyeni kile munachoweza."

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ammiminie Ndugu yetu Mirzabharum na rehema zake nyingi, na kuifanya Pepo kuwa makaazi yake pamoja na Manabii, Waumini, Mashahidi, watu wema, wao ndio marafiki bora, na kuwa atujaalie sisi na familia yake subra, na faraja nzuri.

Licha ya huzuni yetu kubwa kwa kifo cha ndugu yetu, ambaye alikuwa katika safu moja na sisi katika ubebaji ulinganizi, tunasema tu kinachomridhisha Mola wetu:

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake yeye tutaregea.”[Al-Baqara: 156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu