Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  14 Safar 1445 Na: 1445 H / 01
M.  Jumatano, 30 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maelezo juu ya Siku ya "Uhuru" ya Kyrgyzstan
(Imetafsiriwa)

Agosti 31 inaadhimishwa kama Siku ya Uhuru ya Kyrgyzstan tangu 1991. Kwa hivyo, je! Kyrgyzstan kweli ni dola huru? Tunatafuta kulijibu swali hili kwa kuchunguza ukweli wa kihistoria na istilahi.

Kwanza, wacha tuangalie katika historia ya uhuru katika karne ya 20 kuhusiana na suala hili. Neno "uhuru," baada ya Vita vya Pili vya Dunia, lilikuja kuashiria ukombozi kutoka kwa ukoloni. Kiuhalisia, hii ndio maana yake ya kindoto tu. Ukweli ni kwamba mmiliki wa jambo hili ni Marekani, ambayo ililivumbua ili kuunda fursa ya kuyavua makoloni kutokana na wakoloni wengine. Hati ya Atlantiki ni hatua ya kwanza katika mchakato huu.

Hati ya Atlantiki ni mojawapo ya hati muhimu za programu ya muungano dhidi Hitler, ambazo zilikubaliwa na Waziri Mkuu wa Uingereza na Rais wa Marekani katika Kongamano la Atlantiki na kutangazwa mnamo Agosti 14, 1941. Mnamo Septemba 24, Muungano wa Soviet ulijiunga nayo. Hati hii ilitolewa kufafanua mfumo wa ulimwengu baada ya ushindi wa Washiriks katika Vita vya Pili vya Dunia. Lakini, kiuhalisia, Marekani ilikuwa haijaingia vitani wakati huo. Baadaye, neno "Umoja wa Mataifa" lilitumiwa pia kama kielezi cha Muungano wa Kupambana na Hitler, na hili baadaye likawa ndio msingi wa Shirika la Umoja wa Mataifa.

Katika kongamano hili, Marekani ilitaka njia ya kuyafikia makoloni ya nchi zengine kwa badali ya kuingia kwake vitani upande wa Washirika. Imefafanuliwa rasmi katika vifungu vya Hati, ambavyo baadhi yake ni kama vifuatavyo:

- Kuregeshwa kwa ubwana na haki za kuitawala serikali wenyewe kwa watu ambao walinyimwa kwa nguvu. Hii inamaanisha kuunda fursa kwa Marekani kuzichochea nchi zilizo koloniwa dhidi ya dola za zamani za kikoloni chini ya bendera ya uhuru na kuzikoloni tena.

- Ushiriki huru wa nchi zote katika biashara ya ulimwengu na ufikiaji wa malighafi muhimu kwa maendeleo ya dola. Hii inamaanisha kufungua mlango wa kuchukuliwa kwa malighafi za nchi zilizo koloniwa na dola zengine za kikoloni, kwa kuitwa kama biashara.

- Ushirikiano wa kiuchumi wa kiulimwengu. Hii inamaanisha kuingia kwa makoloni chini ya udhibiti wa dola zengine za kikoloni kupitia ukoloni wa kiuchumi.

Utabikishaji wa vifungu hivi vya Hati hiyo ulianza baada ya vita. Operesheni hizi zinajulikana kama kuondoa ukoloni (mchakato wa kutangaza uhuru na ubwana kamili katika maeneo na koloni kubwa na zilizodhibitiwa). Inaweza kusemwa kuwa mchakato wa uondoaji ukoloni ulianza na India kupata uhuru mnamo 1947. Lakini, kiuhalisia, pindi Marekani ilipoanza kuchochea mapinduzi ya uhuru katika nchi hii, Uingereza ilitoa uhuru bandia kwa India na Pakistan, ikizibakisha chini ya udhibiti wake. Mifano mithili ya hiyo ilitokea katika nchi ambazo baadaye zilipata uhuru. Mzozo kati ya Marekani na Uingereza unaendelea nchini India hadi leo. Chama cha Wananchi cha India (Bharatiya Janata), chama tawala huko, ni kibaraka wa Marekani, na Chama cha Kitaifa cha India (Indian National Congress Party) ni kibaraka wa Uingereza. Marekani imeichukua kikamilifu Pakistan. Michakato ya kuondoa ukoloni kimsingi ilifanyika katika nchi za Asia hadi miaka ya sitini.

Uondoaji ukoloni (decolonization) ulipokea msaada mkubwa kutoka kwa Umoja wa Mataifa katika miaka ya sitini. Katika mwaka huo huo, Umoja wa Mataifa ulikubali tamko la "kutoa uhuru kwa nchi na watu walio chini ya ukoloni." Mnamo 1961, Rais Kennedy wa Marekani na Waziri Mkuu Khrushchev wa Muungano wa Soviet walikubaliana huko Vienna kugawanya makoloni kati yao. Baada ya hapo, juhudi za kufikia uhuru ziliongezeka, haswa barani Afrika.

Kama ilivyoelezwa hapo awali, Marekani na Muungano wa Kisovieti zilitoa njia ya kuingia kwa Uingereza, Ufaransa, na nchi zengine ndogo za kikoloni kupitia mapambano ya uhuru. Wakoloni wa zamani walijaribu kudumisha ushawishi wao katika koloni zao na kuzuia wakoloni wapya kuingia. Kwa mfano, Uingereza ilijaribu kutunza nchi katika koloni zake kupitia shirika la Jumuiya ya Madola. Marekani imepenya kiasi katika baadhi ya nchi katika shirika hili, huku ikijiondoa kutoka kwa zengine kikamilifu. Ufaransa ilifanya kazi kupitia shirika la nchi zinazozungumza Kifaransa (Francophonie). Hivi ndivyo mizozo ya kikoloni ya wakoloni hawa ilitatuliwa kupitia makubaliano ya kisiasa, kiuchumi, kijeshi, na kitamaduni. Upande huu iliitwa kama "ukoloni mpya." Nchi ambazo zilizokuwa waathirika wake ziliitwa nchi zinazoendelea au nchi za ulimwengu wa tatu.

Baada ya hapo, vita vinavyojulikana kama Vita Baridi au Vita visivyo vya vurugu kati ya Marekani na mshindani wake, Muungano wa Soviet, vilianza. Muungani wa Soviet ulishindwa katika vita hivi na kuanguka. Nchi washirika ndani ya Muungano wa Soviet zilipata uhuru bandia. Urusi ilianzisha Jumuiya ya Madola ya Mataifa Huru (CIS) kudumisha koloni zake. Hata hivyo, haikuweza kuhifadhi udhibiti kamili juu ya koloni zake, na ushawishi wake ulianza kudhoofika. Baadaye, iliunda Shirika la Mkataba wa Usalama wa Pamoja (CSTO) kutokana na mtazamo wa kijeshi na Jumuiya ya Uchumi ya Eurasia (EAEU) kutokana na mtazamo wa kiuchumi. Ushawishi wake ulipungua zaidi huku nchi zilizo chini ya utawala wake wa zamani wa ukoloni zikawa washiriki wa mashirika mengine ya kimataifa, ikifungua njia kwa wakoloni wengine kuingia.

Kyrgyzstan, kama nchi zengine huko Asia ya Kati, ilipata uhuru bandia na sasa imekuwa ni shabaha ya kampeni mpya za ukoloni. Licha ya kutawala kikoloni kwa Urusi nchini Kyrgyzstan, Marekani iliendelea kuingilia kati katika maswala yetu ya ndani. China, ambayo imeanza ukoloni wake mpya kwa kulikamata jimbo la OSH, imekuwa mkopeshaji na mwekezaji mkuu nchini Kyrgyzstan, na kuongeza upanuzi wake wa kiuchumi.

Kwa hivyo, Agosti 31 sio siku ya uhuru kwa watu wa Kyrgyzstan; Badala yake, ni siku ya ukoloni mpya.

Tunatoa wito kwa watu wa Kyrgyzstan kukumbuka habari iliyotajwa hapo juu: Sisi ni Waislamu, na njia pekee ya kujiondoa kutoka kwa ukoloni ni kupitia Uislamu pekee. Kwa hivyo, hebu na tujifunze Uislamu wetu sote pamoja na tuharakishe kuutabikisha.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu