Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 17 Rajab 1441 | Na: 1441 H / 015 |
M. Alhamisi, 12 Machi 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimezindua Kampeni ya Kiulimwengu: “Beijing+25: Je, Barakoa ya Usawa wa Kijinsia Imeanguka?”
Mwaka 2020 unaadhimisha miaka 25 ya Azimio la Beijing na Mpango wa Utendaji (BPfA), ni waraka mpana ambao ulikuwa ni matokeo ya Kongamano la Kiulimwengu la nne la UN kuhusiana na Wanawake lililofanyika mnamo Septemba 1995, huko Beijing, Uchina. Lengo lake likiwa ni kupanua haki na kuboresha maisha ya wanawake ulimwenguni kupitia kuasisiwa kwa ‘Usawa wa Kijinsia’ katika nyanja zote za maisha: kisiasa, kiuchumi na kijamii, na kuhusisha mitizamo ya kijinsia katika sera, sheria na mipango yote ya dola katika kila ngazi ndani ya dola. Waraka ambao ulitambuliwa kuwa ndio ajenda ya ruwaza pana ya kuwawezesha wanawake na wasichana kimataifa na ndio “ruwaza na sera pana ya kiulimwengu ya kutendewa kazi” ili kufikia usawa wa kijinsia na haki za kibinadamu za wanawake na wasichana kila mahali. Azimio lilipitishwa na nchi 189, ikijumuisha serikali nyingi katika ulimwengu wa Waislamu, ambazo zilikubali kutekeleza ahadi zake ndani ya dola zao na kulingania ajenda yake miongoni mwa mataifa yao. Malengo ndani ya azimio yalipigiwa debe kwa nguvu ndani ya dola.
Kwa miongo kadhaa, ‘Usawa wa Kijinsia’ ndani ya azimio la BPfA na makubaliano mengine ya kimataifa yamekuwa ndio alama ya kimataifa ya kustaarabika, kuendelea kwa dola na kiwango cha kupimia namna mataifa yanavyo watendea wanawake wao. Na pia unatizamwa kama msingi wa kiulimwengu ambao watu wote lazima waukumbatie pasi na kuzingatia thaqafa na imani zao za kidini, licha ya fahamu hii kuwa imezaliwa na Umagharibi ambayo inatokana na mfumo fikra yake ya kisekula. Na pia unatizamwa na wengi kuwa ndio njia pekee ya kuwawezesha wanawake wote, kuboresha ubora wa maisha yao na kupanua maendeleo ya mataifa. Matokeo yake ni kuwa thaqafa au mfumo wowote unaogongana na usawa wa kijinsia hukemewa na kubandikwa kuwa ni dhidi ya wanawake, ulionyuma na unakandamiza. Sheria za Kiislamu kuhusiana na mujtama na familia zimekuwa zikilengwa pakubwa na kulaumiwa na wanaharakati wa kijinsia, serikali za kisekula na mashirika ya UN. Hivyo basi, tawala tofauti ndani ya ulimwengu wa Waislamu wametafuta kufanya marekebisho au kuvipiga marufuku vipengee vya Kiislamu nchini mwao kwa kisingizio cha kuhifadhi haki za wanawake na kufikia usasa na maendeleo. Hata hivyo, kiukweli ulazimishaji mpana wa fahamu ya Kimagharibi ya usawa wa kijinsia ndani ya dola zenye Waislamu wengi na jamii za Waislamu duniani kote ilikuwa ni njia tu iliyotumiwa na dola za Kirasilimali za kikoloni katika mvutano wa kimfumo dhidi ya Uislamu ili kuzuia kunyanyuka ndani ya ulimwengu wa Waislamu kama nidhamu ya kisiasa: Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo itatoa changamoto kwa ubabe wao na kutishia maslahi yao duniani. Hakika, kumekuwepo ndoa baina ya ukombozi wa mwanamke na ukoloni.
Miaka ishirini na tano tangu kwa BPfA na ajenda yake pana ya kumakinisha usawa wa kijinsia ulimwenguni, matatizo ya kisiasa, kiuchumi, kimazingira na kijamii yanayowakumba wanawake Waislamu duniani kote na hasa wanawake kimataifa yanabakia kutamausha na kuzidi kila kukicha. Ahadi za kuwawezesha na kuwaboreshea maisha yao hazijatimizwa. Hii Machi, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimezindua kampeni ya kiulimwengu kwa kichwa, “Beijing+25: Je, Barakoa ya Usawa wa Kijinsia Imeanguka? ambayo itaisha kwa uzinduzi wa kitabu chenye mada hiyo katika warsha za wanawake zitakazofanyika Aprili katika nchi tofauti duniani kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kampeni inalenga: kutoa changamoto kwa mitazamo iliyokita ya ‘Usawa wa Kijinsia’ na madai yake ya kupigia debe haki za wanawake na maendeleo ya mataifa; kufafanua ikiwa usawa wa kijinsia kweli ni msingi wa kiulimwengu; kuchunguza sababu za kufeli kwa sera na sheria za usawa wa kijinsia katika kuboresha maisha ya wanawake; ukweli wa wa kimfumo na kinidhamu wa sababu msingi zinazosababisha matatizo mengi wanayokumbana nayo wanawake leo; kufichua ajenda ya kweli ya Azimio la Beijing na makubaliano mengine ya kimataifa ya wanawake na kampeni itaelezea Uislamu kwa ruwaza yake pana yenye maelezo ya kina kuhusiana misingi, sheria na nidhamu zinazotekelezwa na nidhamu yake ya kisiasa, Khilafah kwa msingi wa njia ya Utume, ambayo inatoa ruwaza mbadala ya kutegemeeka ili kunyanyua hali ya wanawake kuhifadhi haki zao na kuboresha viwango vyao vya maisha na kuleta maendeleo ya kweli ndani ya dola. Kwa wale wote ambao wanataka kikweli kujenga mustakbal ulio na ustawi, uadilifu na usalama kwa wanawake duniani kote, tunawaalika kufuatilia na kunusuru kampeni hii muhimu.
Kampeni hii yaweza kufuatiliwa katika: http://www.domainnomeaning.com/sw/index.php/kampeni/554.html
na Ukurasa wa Faceboook: https://www.facebook.com/WomenandShariah2
Link ya video ya uzinduzi wa kampeni: https://youtu.be/kI0sfssW1ZQ
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
#BarakoaYaUsawaWaKijinsiaImevuliwa
#سقط_قناع_المساواة
#GenderEqualityUnmasked
#CinsiyetEşitliğiMaskesiDüştü
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |