Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 22 Jumada I 1441 | Na: 1441 H / 010 |
M. Ijumaa, 17 Januari 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watoto Wanazama Baharini – Wanazama kupitia Fikra za Kitaifa na Kirasilimali Zinazofanyiwakazi na Wanasiasa!
Watoto wanane walikuwa ni miongoni mwa wahamiaji 11 waliozama mnamo Januari 11, 2020 wakati mashua yao ilipozama katika pwani ya Uturuki magharibi. Viatu vyao, nguo zangu na vitambulisho vyao vyote vilitupwa ufukweni. Saa chache kabla, mashua nyingine ya wahamiaji ilizama katika Bahari ya Lonian ikitoka katika kisiwa cha Ugiriki cha Paxi kabla kuwasili nchini Italia, ikiwaacha takribani watu 12 wamekufa. Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji na UNHCR mnamo Disemba 2019; kila mwaka takribani watu 3,000 wanapoteza maisha yao wakiwa wanajaribu kwenda Ulaya kwa kupitia Mediterranean. Vifo 2,275 vilisajiliwa mnamo 2018 na idadi ya ambao hawakusajiliwa ni kubwa zaidi.
Kwa kujipiga kifua kuwa inatoa msaada kwa wahamiaji milioni 4.5 kutoka Syria, Uturuki ya kitaifa na kisekula inawatizama kama wageni. Hivyo basi hawawezi kupata usalama, ulinzi na kutizamwa sawa ndani ya nchi, watoto na wanawake wasiokuwa na hatia, ambao wamekimbia vita, wanalenga kufika Ulaya, lakini wanazama katika bahari ilhali wakiwa katika mchakato huo. Pili kutizamwa kitabaka, walimu wakitaifa wanawafedhehesha watoto wa Syria ndani ya shule, kwa kuwanyima kila huduma na msaada katika kipindi cha miezi ya baridi kwa kuwa na sehemu za makaazi ambayo hayana milango, kwa kuwa eti tu hawana makaratasi ya kujitambulisha, waajiri walafi ambao hawawalipi mishahara inayostahiki wafanyikazi wa Syria; na hususan ubaguzi kwa misingi ya utaifa na rangi kutoka kwa wanasiasa wasiokuwa na mtazamo mpana, ambao hawawaoni wa Syria kuwa wanastahiki maisha nje ya kambi zao zisizokuwa na mustakbali na ambao pia wanatoa matamshi yenye uchochezi kwa watu wa Uturuki dhidi ya wa Syria, masuala yote haya ni sababu zinazo walazimisha watu hawa kuingia katika idhilali ya vimbunga na baridi ya bahari katika miezi ya baridi…
Haya yote ni licha kwamba Uislamu haumtizami Muislamu yeyote kutoka sehemu yoyote duniani kuwa mgeni, wacha kuwa mgeni katika ardhi ya Waislamu. Watu hawa walikuja katika ardhi yao haki yao ambayo ilifunguliwa na Uislamu kupitia kujifunga na Maamrisho ya Mwenyezi Munngu na Ahadi ya Mtume Wake (saw). Kwa msingi huu wa haki ya Kiislamu, Muislamu hatakiwi kuwa na visa, cheti cha kuishi au kufanyakazi anapowasili katika ardhi yoyote ya Kiislamu. Kwa kuongezea, Uislamu unapinga mitazamo yote ya kitaifa na kumtizama kila mtu anayeishi katika maeneo ya Kiislamu kama mmoja wa raia wake pasi na kuzingatia itikadi, rangi, kabila, ardhi anayotoka na haiwatizami kama wageni na hususan Muislamu yeyote. Watu wote walio na uraia wa Kiislamu wanatizamwa sawa, pasi na ubaguzi baina yao kutoka kwa mtawala, katika kusimamia mambo yao na katika kulinda maisha, heshima na mali zao, au kutoka kwa hakimu kwa kuzingatia usawa wa haki. Katika kipindi chote cha historia ya Kiislamu, watawala Waislamu walipinga kuangaliwa Waislamu kama wageni, bali waliwapa wakimbizi kutoka ardhi zisizokuwa za Kiislamu, walio kimbia mateso, na kuwapa sehemu tulivu na salama katika ardhi za Waislamu na kuwatizama kama raia wao. Kwa kuongezea kutizamwa kwa uzuri Dhimmi (raia wa dola wasiokuwa Waislamu) ni wajib katika Uislamu, kwani Mtume (saw) alisema lau yeyote atamtendea vibaya Dhimmi
«فَأَنَا حَجِيجُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ» “Nitakuja kuzozana dhidi yake Siku ya Kiyama.” Inawezakana vipi ukandamizaji ukatokea kwa Muislamu chini ya nidhamu kama hiyo, pale ambapo hata haki za wasiokuwa Waislamu zinalindwa kwa ubora? Je, Muislamu ataangaliwa kama raia wa tabaka la pili?
Enyi Watawala wa Uturuki! Oneni, namna mulivyokuwa kutokamana na utaifa wenu. Kukimbilia kwenu fikra za kitaifa na kisekula zimewafanya kuhesabiwa kwa kila uhai uliotoka kutokamana na milipuko, mateso na kuzama katika bahari! Kwa kuongezea, mikono yenu imejaa damu za Waislamu wanawake, watoto na wanaume, kwa kuwa hamuku nyamaza tu dhidi ya Kafiri ambaye anawanyima makaazi na maisha yao; bali mumekuwa washirika, muungano na marafiki na munapeana mikono na wauaji.
Enyi Waislamu nchini Uturuki na ardhi zote za Waislamu! Lau watawala wangeli tawala kwa Uislamu, kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt) na kuunganisha Ummah kuwa pamoja, kuwa ngumi moja kama ilivyoamrishwa na Uislamu, sio tu Waislamu bali dunia nzima, kila mwanadamu, pasi na kuzingatia dini, rangi na kabila angeliokolewa kutokamana na kila aina ya ukandamizaji! Kwa hiyo, changamkeni kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa Njia ya Utume, ambayo Muumba wenu (swt) na Mtume Wake (saw) wamewaitieni kuisimamisha na ambayo itawapa maisha!
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) domainnomeaning.com |