Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 20 Safar 1440 | Na: 1440/006 |
M. Jumatatu, 29 Oktoba 2018 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Yemen yakabiliwa na baa la njaa la kutisha lililowahi kutokea ndani ya miaka 100 ya ulimwengu likisababishwa na mzozo kati ya Uingereza na Marekani ambao umeutia nchi hiyo katika vita wasivyostahiki wakiongozwa na vibaraka wa kitaifa na kieneo!
Kwa mujibu wa duru za Umoja wa Mataifa, Yemen kwa sasa inakabiliwa na baa la njaa baya zaidi ulimwenguni kwa miaka 100. Uzani wa janga hilo umefananishwa na ule uliokumba Afrika katika miaka ya themanini. Ripoti ya hivi majuzi ya shirika la habari la BBC imenukuu kuwa kwa mujibu wa Lisa Grande, Msimamizi wa Misaada ya Kibinadamu wa UN nchini Yemen, zaidi ya raia milioni 13 wako katika hatari ya kufa kutokana na ukosefu wa chakula katika miezi mitatu ijayo. Shirika lisilo la kiserikali la Uswizi CARE limeripoti mnamo Machi 2018 kuwa wanawake na watoto milioni 3.25 walio katika umri wa uzazi wanakabiliwa na ongezeko la hatari za kiafya na ulinzi. Kwa mujibu wa afisa wa UNICEF Juliette Touma, Yemen ni, “mojawapo ya sehemu hatari zaidi kwa mtoto kuwa ndani yake. Pengine ni salama kusema kuwa kwa sasa hakuna sehemu iliyo salama kwa watoto nchini Yemen, karibu watoto wote nchini humo wanahitajia msaada wa kibinadamu kutokana na mzozo huo. Usalama na ulinzi wa watoto umezorota kwa sababu ya mashamulizi ya kuendelea, kwa sababu ya ghasia zisokwisha dhidi ya watoto.”
Maeneo mengi yaliyokuwa na makaazi mengi yameshambuliwa na mashambulizi shirika ya angani, ambayo ni thibitisho kuwa maeneo ya mijini yanalengwa kimakusudi. Ali al-Absi, mwanasayansi wa kisiasa wa Yemen aliye na makao yake jijini Berlin alisema katika ripoti ya habari ya mtandaoni ya shirika la habari la Ujerumani DW mnamo 10 Agosti, “Saudi Arabia inakadiria chochote nchini Yemen kuwa halali kulengwa, ikiwemo shule, masoko, miundo mbinu, maharusi na makao ya mayatima. La kusikitisha ni, Saudi Arabia haionekani kujali kuwaonea huruma raia katika janga hili la vita.”
Huku riyal ya Yemen ikiendelea kuanguka dhidi ya dolari na sarafu nyenginezo za kigeni pasi na manufaa yoyote ya matibabu ya kiuchumi yaliyo tangazwa na ile inayoitwa serikali halali kwa ubadilishanaji wa tuhuma kati yake na Mahouthi wanaodhibiti jiji kuu la Sana’a, na wote wanacheza kamari kwa gharama ya mateso ya watu wa Yemen na kuwauwa, ima kupitia vita au baa la njaa au maradhi ambapo bei ya dolari ya Amerika imefikia zaidi ya riyal 700 za Yemen kutokana na mizozo na vita nchini Yemen kati ya mibabe wanaopata maslahi ya mabwana zao wa kikoloni, hususan Amerika na Uingereza, nchi mbili zinazopigania ushawishi na utajiri (rasilimali) nchini humo, ingawa mishahara imesitishwa katika mikoa mingi nchini humo, hususan maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa wanamgambo wa Houthi ambao wametumia pesa hizo kwa ajili ya juhudi za vita, pamoja na kuvuruga huduma na ukosefu wa ajira na ukosefu wa usafirishaji mafuta, gesi na rasilimali nyenginezo za nchi hiyo ng’ambo. Na ufisadi umeenea pakubwa; ima chini ya udhibiti wa ile inayoitwa serikali halali au chini ya udhibiti wa Mahouthi. Ni hali ambayo pande zote hazimiliki mamlaka ya ufanyaji maamuzi. Hii ni pamoja na uhasama mkali kati yaSaudi Arabia na Imarati juu ya rasilimali za nchi hiyo na bandari zake, ambapo Imarati inadhibiti bandari za kusini mwa Yemen na mradi wa gesi mjini Balhaf, huku Saudi Arabia ikifanya kazi kujenga bomba la mafuta katika eneo la Al-Mahra ili kusafirisha mafuta hadi bahari ya Arabia. Hivyo basi, Yemen imekuwa kinyang’anyiro cha mabwana zake walafi wa kikoloni huku watu wake wakikabiliwa na mateso na kukata tamaa na wanashambuliwa kwa moto wa vita vyao viovu. Nchi mbili hizi, Saudi Arabia na Imarati, ambazo zimetangaza vita chini ya jina la muungano wa Waarabu dhidi ya Mahouthi, wanaopokea usaidizi kutoka Iran, wana maslahi tofauti tofauti na hawajali kuhusu watu wa Yemen na mateso yao.
Huu ndiyo uhakika wa mzozo nchini Yemen na wapiganaji wote wanaostahili kufichuliwa na kuaibishwa. Sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunatoa wito kwa dada zetu wote wa Kiislamu ulimwenguni kutambua hali hii iliyo iathiri Yemen na watu wake, ili kuharakisha kufanya kazi nasi kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume kwani hiyo pekee ndiyo itakayo linda Ummah huu, kukata mkono wa kikoloni wa uingiliaji mambo katika ardhi zetu na kuhakikisha chakula, madawa, makaazi na usalama kwa kila raia chini ya utawala wake. Pasi kwayo Ummah wetu utaendelea kuteseka kila aina ya majanga, na maadui zake watasalia na himaya ya kutoadhibiwa na kulipizwa kisasi. Tunawaambia dada zetu wapendwa na watoto nchini Yemen … mateso yenu biidhnillah (swt) hayatakuwa kwa muda mrefu. Wale wote waliotekeleza uhalifu huu muovu dhidi yenu watahesabiwa na Khilafah hapa ulimwenguni, na kukumbwa na adhabu kali ya Allah ambayo ni mbaya zaidi na ya milele.
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |