Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 19 Dhu al-Hijjah 1444 | Na: 1444 H / 044 |
M. Ijumaa, 07 Julai 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sudan Inavuja Damu na Inalilia Msaada... Je, Kuna Mwokozi kwa Watoto na Wanawake?
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 15/4/2023, mapigano yalizuka jijini Khartoum kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka. RT mtandaoni ilinukuu yafuatayo kutoka kwa AFP: "Mapigano yanaendelea kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka huko Khartoum, wakati ambapo shirika moja la misaada lilionya juu ya mlipuko wa ukambi na utapiamlo miongoni mwa watoto katika kambi za waliohamishwa, na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.'' Na liliripoti kwenye Twitter, "kambi 9 zinahifadhi mamia ya maelfu ya watu, wengi wao wakiwa wanawake na watoto," likionya kuwa "hali ni mbaya" kwa kuzingatia visa vinavyoshukiwa vya ukambi na utapiamlo kwa watoto. Pia likinkuu, "Kati ya Juni 6 na Juni 27, tulitibu watoto 223 wanaoshukiwa kuwa na ukambi, watoto 72 walilazwa, na 13 walikufa katika zahanati tunayosaidia." Kwa upande mwingine, kitengo cha serikali cha kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kiliripoti kusajiliwa kwa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake huko Khartoum na Darfur, haswa katika mji wa El Geneina, katikati mwa jimbo la Darfur Magharibi. Katika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa Facebook mnamo siku ya Jumamosi, ilisema: "Kulikuwa na jumla ya kesi 42 za unyanyasaji wa kijinsia jijini Khartoum, huku kesi 21 za unyanyasaji wa kijinsia zinazohusiana na mzozo zikirekodiwa huko El Geneina", ikibainisha kuwa ripoti nyingi na ushuhuda zilirekodiwa dhidi ya wanachama wa Vikosi vya Msaada wa Haraka. Kitengo hicho hapo awali kilirekodi kesi 25 za unyanyasaji wa kijinsia huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini. Tangu Aprili 15, Sudan imekuwa ikishuhudia mapigano kati ya jeshi linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan, na Vikosi vya Msaada wa Haraka vinavyoongozwa na Mohamad Hamdan Dagalo. Mzozo huo umesababisha vifo vya takriban watu 2,800 na wengine zaidi ya milioni 2.8 kuwa wakimbizi.
Mapigano ambayo watoto na wanawake wa Sudan wanalipia gharama yake, na matokeo yake, wanaonja udhalilifu na kunyenyekeshwa. Hakuna ulinzi wala usalama. Mapigano hayo yamesababisha machafuko nchini humo na watu kuishi kwa hofu na ukosefu wa usalama.
Enyi Watu Wetu wa Sudan: Je, hamjauliza ni nani anayefaidika na mapigano haya, ni nani anayechochea moto wake, na kwa nini? Ni nani yuko nyuma ya wale wanaolingania kujitenga, kuichana Sudan, na kuifanya iwe mawindo rahisi kwa maadui zake?! Je, hamuoni uingiliaji kati wa nchi za kikoloni, balozi zao, mashirika na jumuiya zao kuvuna kutoka nyuma ya mafanikio haya na kutekeleza ajenda zao hadi nchi idhoofikr na mshiko wa watu kukazwa?!
Enyi Wanachuoni wa Kiislamu: Mko wapi mnaposhuhudia yanayowasibu vijana wenu, watoto wenu na wanawake wenu kwa kuzingatia mapigano haya?! Mko wapi wakati mapigano baina ya ndugu zenu yakiendelea na nyinyi mumenyamaza kimya, hamkatazi maovu haya wala kuonyesha uharamu wake?
Enyi Wanyoofu katika Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka: Je, hakuna mwenye busara miongoni mwenu wa kurekebisha njia kuwaongoza watu wake nchini Sudan kwenye usalama? Je, hakuna miongoni mwenu wa kuwatetea, kuwalinda, na kunyanyua juu bendera ya kutawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) ili wafanyi kazi wakusanyike nyuma yake na Mola wa walimwengu wote amnusuru?
Enyi Watu Wetu Nchini Sudan: Sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunasikitishwa na kile kinachotokea kwa dada zetu na watoto wetu nchini Sudan, na tunalaani vikali vitendo hivi. Tunatoeni wito kwenu kuyahami matukufu na heshima yenu; ambayo ni kwa kufanya kazi mara moja na Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, ili kutawala kwa Shariah ya Mola wenu Mlezi kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ili mupate izza hapa duniani na kesho Akhera.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |