Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 4 Ramadan 1440 | Na: 1440/032 |
M. Alhamisi, 09 Mei 2019 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji Dhidi ya Watoto wa Yemen yanaendelea, ilhali Wauaji wanacheza dori ya Waweka Amani
Mnamo 26 Aprili, Umoja wa Mataifa ulipeperusha ripoti kwamba idadi ya waliofariki ndani ya Yemen kutokana na mzozo unaoendelea unatarajiwa kupita 230,000 mwishoni mwa 2019. Utafiti kwa kichwa “Tathmini ya Athari ya Vita Juu ya Maendeleo ndani ya Yemen”, pia iliripoti kuwa Wayemen 131,000 watakuwa wamefariki kutokana na athari mbaya za vita baina 2015 na 2019 mfano kutokana na njaa, maradhi na kukosekana kwa kliniki za afya. Kwa mujibu wa UN mwishoni mwa mwaka, mapigano yatakuwa yamechukuwa maisha ya watu 102,000. Janathan Moyer, muandishi kiongozi wa ripoti, alielezea kuwa vita ndani ya Yemen kuwa ni “moja ya mizozo yenye athari kubwa kindani tangu mwishoni mwa Vita Baridi." Pia alisema kuwa wengi wa wahanga wa mzozo wa Yemen ni watoto wa chini ya miaka 5 na kwamba mtoto 1 anafariki kutokana na vita na athari yake mbaya kwa kila dakika 12. Makundi ya misaada yanakadiria kuwa zaidi ya watoto 85,000 wamekufa njaa tangu 2015 na mamilioni zaidi wako hatua moja kando na ukame.
Hivi vita vya kiwakala baina ya Uingereza-Amerika vinapiganwa na vibaraka wao wa kienjeji na kimaeneo na –tawala za muungano unaongozwa na Saudi na ule wa Iran unaounga mkono Mahouthi –ili kuhifadhi maslahi yao ya kibinafsi ndani ya nchi na udhibiti wao wa rasilimali. Vita hivi vimesambaratisha miundombinu na maisha ya watu wa Yemen na kuleta vifo, ukame na maangamivu kwa watu wa Yemen na polepole vinaendelea kumaliza idadi wa Yemen. Watoto wa Yemen ni wahanga wa ulafi huu usiokuwa na maadili unaotokana na dola za kirasilimali ambazo hazitilii maanani athari mbaya zinazotokana na michezo yao ya kisiasa katika nchi na mataifa mageni, wakiwa tayari hata kuangamiza watu wote kwa ukame ili kuhudumia mahitaji yao. Marekani imetoa mabilioni ya dolari ya kisilaha kwa muungano unaongozwa na Saudi tangu kuanza kwa vita pamoja na kujaza mafuta, kutoa ujasusi na kutathmini ndege angani. Uingereza nayo imeuza takribani dolari billioni 5 ya zana za vita kwa Saudi Arabia tangu 2015 ikijumuisha ndege za kivita, ndege zisizokuwa na rubani (droni) na silaha.
Umoja wa Mataifa kwa upande wake inaendelea kufanya kazi ndani ya Yemen ili kuvipanua vita hivyo ili kupatiliza na kufanya biashara kwa kutumia njaa katika maisha ya watu. Kwani ndiyo inayotoa ilani kila kukicha kuwa Yemen iko katika hali mbaya ya kiukame ili kupata uungwaji mkono na misaada kwa mwito wa kuwa eti inapitia hali ngumu ilhali wanaiba misaada inayokusanya katika makongamano ya ufadhili na kuipeana kwa mashirika ya UN na mashirika maovu ya kienyeji ambayo yanafaulisha ajenda ya Amerika ndani ya Yemen. Kiwango kikubwa cha pesa kinakwenda kuajiri wafanyikazi wa mashirika haya ili kuwapotosha kimaadili na kifikra kupitia dolari na mishahara mikubwa, hivyo basi wakipatiliza hali ya kiuchumi inayosambaratika nchini humo.
Inawezekaje Umoja wa Mataifa kuaminiwa wakati tangu kuanza kwa vita ndani ya Yemen imepokea zaidi ya dolari bilioni 8 kutoka kwa makongamano ya wafadhili kwa ajili ya Yemen? Imepeana fedha hizo kwa vitengo vyake vingi lakini watu wa Yemen wanaendelea kupitia hali ngumu wakiumia kwa umasikini, ukame na maradhi. Shirika hili au Umoja wa Mataifa hautatui matatizo. Bali unaleta majanga na dhiki na kutengeneza mabilioni ya dolari kutokana na kuumia kwa watu na badala yake wanawapa makombo pekee.
Baada ya kutathmini haya, tunauliza ni vipi mtu mwenye akili anaweza kuamini kuwa wachocheaji, wafadhili, watiaji mafuta na washangiliaji wa vita hivi vya kutisha wataweza kuwa wadhamini wa amani wa ukweli ili kusitisha mauaji dhidi ya watoto Waislamu wa Yemen au kutenda kwa maslahi yao mema? Ima ni 'udhamini wa amani' wa UN au yale yanayoitwa 'mazungumzo ya amani' ndani ya London mnamo 26 Aprili baina ya katibu wa kigeni wa Uingereza na muwakilishi wa Marekani, Saudi Arabia, UAE na UN –hayatoleta jema lolote la kikweli kwa Waislamu wa Yemen. Wao ni kama mbwa mwitu wanaopigania juu ya mzoga wa waliyemuwinda. Hakika, Mwenyezi Mungu (swt) asema,
﴾وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ قَالُواْ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ * أَلا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـكِن لاَّ يَشْعُرُونَ﴿
“Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.” [Al-Baqara: 11-12]
Enyi Waislamu wa Yemen! Toeni nussrah yenu ili kwa dharura kusimamishwe uongozi wa kweli wa Kiislamu, Khilafah kwa njia ya Utume ambayo ndio njia pekee ya kumaliza mauaji haya dhidi ya watoto na familia zenu na kung'oa uingiliaji wa kikoloni wa aina yoyote katika ardhi yenu. Itaunganisha mioyo ya Waislamu wa Yemen kwa Aqeeda ya Kiislamu na Shari'ah bora ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuhakikisha kuwa kila raia chini ya utawala wake ametimizwa, amelindwa na kufurahia elimu na afya ya kiwango cha juu pasina na unyanyapaa na kurudisha sifa ya ‘Furaha ndani ya Yemen’ katika ardhi zenu.
Dr. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |