Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 13 Rajab 1440 | Na: 1440/026 |
M. Jumatano, 20 Machi 2019 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ongezeko la Takwimu Sio Jipya Bali Halina Budi kwa Zabuni za Kifedha Kabla ya Kongamano la Wafadhili la Brussels kwa Ajili ya Syria
(Imetafsiriwa)
Vita katili nchi Syria dhidi ya raia vimeingia mwaka wake wa tisa mnamo Machi 15. Zaidi ya watu nusu milioni wamekufa, kwa mujibu wa ripoti za kimataifa, na shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria limenakili vifo 19800 vya watoto tangu 2011. Inakisiwa watoto milioni 8.6 wanahitaji msaada wa dharura, na sasa zaidi ya watoto milioni 6 hawana makao au wanaishi kama wakimbizi, na baadhi ya milioni 2.5 yao hawendi shule. Zaidi ya watoto milioni 3 wako katika hatari ya mabomu ya ardhini, huku takriban asilimia 40 ya wale waliouwawa na mabomu ya ardhini wakiwa ni watoto.
Na huu hapa Umoja wa Mataifa na mashirika yake ya kibinadamu yanayo endela kuibua hofu na kuonya kuhusu hatari za vita hivi vinavyo endelea, hususan kwa watoto. Mnamo Machi 11, shirika la Umoja wa Mataifa la Hazina ya Dharura ya Kimataifa (UNICEF) lilisema, “Mnamo 2018 pekee, watoto 1,106 waliuwawa katika mapigano hayo – idadi ya juu zaidi ya watoto kuuwawa ndani ya mwaka mmoja tangu kuanza kwa vita hivyo.” Taarifa mithili ya hii ilitolewa mwanzoni mwa 2018 na Mwakilishi wa UNICEF nchini Syria kwa anwani, “Kuanza kwa mwaka na umwagikaji wa damu nchini Syria; zaidi ya watoto 30 waliuwawa katika wiki mbili za kwanza za 2018’. Ripoti za awali zimeonyesha kuwa watoto wanaongezeka kubeba athari ya vita nchini Syria, wakiwasilisha takriban asilimia 23 ya raia majeruhi mnamo 2016. Kati ya 2016 na 2018, Umoja wa Mataifa umerekodi vifo vya takriban watoto 2,500. Kama alivyo sema awali Mkurugenzi wa Eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa UNICEF, “Ni vita juu ya watoto, maelfu ya watoto wameuwawa na wangali wanauwawa.”
Takwimu zinazo ongezeka sio mpya au hata za kushangaza usoni mwa vita hivi vya kuendelea na katili dhidi ya raia wote, hususan watoto, kama baadhi wanavyo viona kuwa visokuwa na budi kama vilivyo vita vyengine.
Miaka minane sasa, na ripoti hizo hizo na maonyo ya kurudiwa rudiwa yanaendelea kutolewa na mashirika haya, huku takwimu zikibadilika kila mwaka katika viwango vya juu vya kushtua mno huku idadi ya vifo vya watoto ikiendelea kuongezeka …
Takwimu zinazotumiwa kwa zabuni za kifedha, kama Umoja wa Mataifa ilivyotoa taarifa ifuatayo siku chache kabla ya Kongamano la Wafadhili la Brussels ili kusaidia mustakbali wa Syria na eneo hilo, lililofanyika mnamo Alhamisi, 14 Machi, ambapo michango ilikuwa chini kuliko ilivyotarajiwa, kwa mujibu wa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa aliye sema, “Tuliomba $ 9 bilioni lakini kiwango cha ahadi kilikuwa $ 6 bilioni pekee.” Umoja wa Mataifa uliweka mahitaji ya kifedha ya 2019 kuwa dolari bilioni 5.5 ili kuwasaidia zaidi ya wakimbizi 5.6 milioni walio nje ya nchi yao, huku ikikisiwa mahitaji ya dolari 3.3 bilioni kwa wakimbizi wa ndani kwa ndani!!
Takwimu kubwa za kifedha huongezeka kila takwimu za vifo zinapodumu kuongezeka, ikiwasilisha swali: Je, zinatumiwa kwa mafukara na wakimbizi kama ilivyo pangwa?! Je, zimebadilisha hali ya watoto wanaokufa kutokana na mashini za kivita za kinyama za kimataifa?!
Nchi za kikoloni zinazofuja mali na kulenga kuwanyima chakula watu, na ziko mbali na utu, ambao wanajigamba nao, huyapa mashirika ambayo ni ala za dola hizi kuu za kikoloni viwango vikubwa vya pesa ili kutekeleza sera zao ulimwenguni!! Yanauwa watoto wetu na kisha kuwalilia juu yao na kumwaga machozi ya mamba ili kufuja na kuendelea kumakinisha udhibiti wao, bali utawala wao juu ya biladi za Kiislamu, bali hata juu ya ulimwengu mzima.
Huku Batil ikiwa na nguvu, Haki ina nguvu na ufunguzi, hifadhi na usalama vitaenea na watoto wa Waislamu watafurahia wepesi na dhamana na wataishi utotoni mwao chini ya uadilifu wa Uislamu. Na hilo haliko mbali, kwani ni ahadi ya Mola wa Walimwengu kuwa matokeo mema ni kwa watu wema.
Enyi Waislamu! Jueni kuwa kuondoa mateso ya wanadamu na sio tu kwa watoto itakuwa ni kwa kupitia kutoa ahadi ya utiifu (Bay’ah) kwa Khalifah ili kutawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kupitia kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kwani ndio itakayoizuia mikono ya wanaoharibu usalama na hifadhi yetu na itakomesha mateso yetu na mateso ya watoto wetu, kupoza nyoyo zetu, kurudisha furaha ndani ya nyoyo zetu na kuleta izza na jaha miongoni mwa mataifa, kwa hivyo hatusubiri pesa zao, ambazo kwao zitakuwa ni chanzo cha majuto kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyo sema:
﴾إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنْفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ﴿
“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [Al-Anfal: 36]
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |