Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 20 Rabi' I 1444 | Na: 1444 H / 012 |
M. Jumapili, 16 Oktoba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa kukosekana Khilafah, Watoto wa Ummah wetu nchini Iraq Wanaanikwa kwa Hofu za Utaifa
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 29 Septemba 2022, shirika la Habari la ‘Arab News’ liliripoti juu ya mashambulizi ya droni yaliyoanzishwa na Iran kwa kile kinachoitwa mawakala wa waasi wa Kikurdi katika eneo hilo. Milipuko ilitokea katika mji wa Irbil, Kurdistan ya Iraq na kushambulia shule moja iliyokuwa imejaa wanafunzi. Waandishi wa habari katika eneo la tukio walisambaza picha za watoto wa shule waliotapakaa damu katika eneo la Kurdistan kaskazini mwa Iraq. Video zengine zilizotumwa na waandishi wa habari zilionyesha watoto wa shule ya Kikurdi waliopigwa na hofu wakisindikizwa kwenye usalama na kujihifadhi kwenye sehemu za milima karibu na mji wa Koya.
Jeshi la Iran linalojiita Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) lilirusha makombora kadhaa ya balestiki aina ya Fateh 360; kombora jipya Iran ililifanyia majaribio kwa mara ya kwanza mapema Septemba 2022. Droni 136 za kujiua za Shahed pia zilitumiwa katika eneo hilo - zile zile zilizotumwa hivi majuzi na Urusi katika vita vya Ukraine - na kuua watu wasiopungua 14 na kujeruhi 58, wakiwemo wanawake na watoto.
Hofu ambayo watoto wa Ummah huu wanapaswa kuistahimili ni ya kuendelea. Mahali panapopaswa kuwa salama zaidi, mahali pa kujifunza na ukuaji wa viongozi wetu wa kizazi kijacho pana haribiwa na utovu wa usalama uliopo chini ya ajenda za kitaifa za nchi zetu. Ni muhimu tutambue kwamba mauaji na majeraha haya sio tu uharibifu wa dhamana kama matokeo ya ulinzi halali wa taifa la mtu. Kanda zetu zote ni ukumbi wa vita ambapo maslahi ya kikoloni yanatafutwa na maisha ya watoto wetu wapendwa yamefanywa kuwa silaha ya kutumikia ulafi wa mabwenyenye.
Ned Price, afisa mmoja wa Marekani, alitoa taarifa yake kulaani mashambulizi ya utawala wa Iran dhidi ya Kurdistan ya Iraq. Malalamiko haya ya kinafiki juu ya hali ya haki za binadamu za Waislamu hayatatuhadaa. Haifichiki jinsi Marekani na washirika wao wanavyotekeleza mauaji, vikwazo, kuwaweka kizuizini na kuwatesa maelfu ya Waislamu kote duniani. Historia yao ya kutisha ya kuwaunga mkono madhalimu na kumwaga damu za Waislamu inajulikana vyema, na kwa kukosekana Khilafah, msimamizi na mlinzi wa Waislamu, mauaji haya yanayoendelea hayatakuwa na mwisho!
Osamah Golpy, mwandishi wa habari wa Kikurdi anaamini kuwa hii ilikuwa hatua ya makusudi kwa upande wa Tehran "kuweka ajenda kwani kuna angazo chache la maandamano na angazo zaidi la mashambulizi ya Iran ndani ya Kurdistan ya Iraq". Alisema: "Ufahamu wangu ni kwamba ilikuwa ya makusudi na wakati wake ulilengwa ili kutuma ujumbe huu kwa wadau mbalimbali, ikiwemo Jimbo la Kurdistan na makundi ya waasi wa Kikurdi ya Iran." Tukijua kwamba hakuna hata mmoja wa viongozi wetu katika ulimwengu wa Kiislamu aliye na mamlaka huru, hakika anachodokeza Golpy ni kitabu cha michezo ya kisiasa kinachotumiwa ambapo mizani za madaraka zinabadilishwa kupitia misukosuko ya ndani. Gharama wanayolipia watoto wetu wasio na hatia katika "Mchezo huu wa Maeneo" haina umuhimu kwa vyombo vyenye nia ovu vyenye udhibiti wa mambo yetu.
Mwenyezi Mungu (swt) haukubali mfarakano huu baina ya Waislamu ambao umetokana na fahamu hii fisadi ya utaifa. Wala Mwenyezi Mungu (swt) hakubali kugawanywa kwa ardhi za Kiislamu kuwa dola za kitaifa kwa misingi ya kitaifa au kikabila jambo ambalo linasababisha dhulma zinazotekelezwa dhidi ya Waislamu wa makabila tofauti tofauti na migogoro isiyo na maana baina ya Waislamu juu ya ardhi na madaraka. Quran iko wazi kwamba vita hivi vya kitaifa kati ya Waislamu ni Haramu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
(إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ)
“Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.” [Al-Hujraat: 10].
Ni lazima tufichue michezo hii ya kisiasa ya kitaifa ya kikoloni inayofanyika katika ardhi zetu za Kiislamu, na kamwe tusijihusishe na simulizi hizi za batili zinazoficha ajenda halisi dhidi ya Waislamu na Uislamu. Tunausihi Umma wa Mtume Mtukufu Muhammad (saw) kusimama na kuzungumza wazi dhidi ya utishaji na mauaji ya watoto wa Kiislamu ambao wana haki ya kusoma na kujiendeleza kwa usalama na kuheshimiwa kwa vipaji vyao kama viongozi wa mustakabali wa Dini hii ya Haki.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |