Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  13 Rabi' II 1441 Na: 1441 H / 007
M.  Ijumaa, 13 Disemba 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Facebook Kufunga Kidhuluma Ukurasa wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Women & Shariah, Kunalenga Kunyamazisha Sauti za Wanawake Waislamu Wanaolingania Uislamu kama Mkombozi wao kutokana na Ukandamizaji Badala ya Uhuru wa Kimagharibi

Mnamo Ijumaa 29 Novemba, Facebook ilifunga kidhuluma ukurasa rasmi wa Kiingereza wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Women & Shariah, pasina na maelezo yoyote kuhusiana na hatua yao hiyo. Akaunti ilikuwa na wanaoipenda na wanaoifuata zaidi ya 40,000 huku baadhi ya post zake zikipata kufikia zaidi ya watu nusu milioni. Ukurasa ulikuwa umejikita katika kutatua masuala nyeti, matatizo na ukandamizaji unawaoathiri wanawake na watoto ulimwenguni na kuwasilisha mtazamo wa Kiislamu juu yake. Pia ililenga kuvunjilia mbali urongo na upotoshaji uliokita mizizi ya kizamani kuhusiana na misimamo na suluhisho zinazohusiana na wanawake chini ya Uislamu, kwa kuangazia ukweli wa cheo, haki, dori na majukumu ya mwanamke kama ilivyoelezewa na sheria za Shariah ya Kiislamu chini ya nidhamu ya kisiasa ya Kiislamu: Khilafah kwa msingi wa njia ya Utume.

Kwa miaka mingi, ukurasa uliendesha na kuangazia kampeni muhimu na zenye manufaa za kiulimwengu kuhusiana na mada tofauti tofauti zikijumuisha namna ya kusuluhisha mporomoko wa kiungo cha familia unaothiri jamii duniani; namna ya kusuluhisha janga la elimu linalokumba ulimwengu; na namna ya kupambana na changamoto nyingi na matatizo ambayo vijana Waislamu wanakumbana nayo leo katika kushikamana na kitambulisho chao cha Kiislamu. Napia ulilenga kuleta uzindushi wa kiulimwengu na kutoa suluhisho la matatizo yanayowakumba Waislamu duniani kote na hususan kuhusiana na wanawake na watoto ndani ya ardhi kama vile Syria, Palestina, Myanmar, Yemen, Kashmir, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Uchina. Ukurasa ulikuwa makini kuhakikisha kuwa post zake ziko na taarifa za ukweli kutoka katika vyanzo vinavyoheshimika na hakuna chochote katika uchafu au kinyume na maadili kilipigiwa debe. Hii ni kinyume na kurasa nyingi chafu na fisadi na nyinginezo ambazo zinapigia debe urongo wa wazi dhidi ya Uislamu ambazo Facebook inaziruhusu kufanyakazi pasina na kudhibitiwa.  Kwa kuongezea, akaunti ya “Women & Shariah” ni moja ya kurasa za Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, chama cha kiulimwengu kisichotumia nguvu na ambacho hakijawekewa vikwazo ndani ya dola za Kimagharibi zikijumuisha Amerika ambapo makao makuu ya Facebook yako. Kinyume chake tunafanyakazi wazi ndani ya nchi hizi ambamo tumeweza kufanya makongamano na warsha za umma nyingi na ambamo tunasambaza amali zetu za kisiasa na kuingiliana na umma katika mabarabara na mitandaoni. Hivyo basi, suali linabakia kwa Facebook ni kwa nini kampuni ambayo inajigamba kuwa ni jukwaa huru la kubadilishana fikra na mijadala itachukua hatua ya kudhibiti ukurasa ambao amali zake hazina tishio kwa mujtama wowote.  

Ni wazi hakuna sababu nyingine ya ubaguzi ya kufungwa kwa akaunti yetu pasina msingi wowote isipokuwa ni kwa kigezo cha fahamu za wanawake Waislamu kulingania UISLAMU kama njia yao ya kupata ukombozi kutokamana na ukandamizaji badala ya Uhuru wa Kimagharibi unaokwenda kinyume na masharti na sera zao! Bali wako tayari kuruhusu wengine kuzungmza uongo dhidi yetu kwa niaba yetu na kupigia debe mitazamo ya kudunisha kitambulisho chetu, badala ya kupeana jukwaa ili kuruhusu maoni ya kweli ya wanawake Waislamu ambao wanaunga mkono Uislamu kuenezwa. Kwa kuongezea, umaarufu wa ukurasa unaowasilisha ukweli kuhusiana na nidhamu ya Kiislamu ya Khilafah itakavyokuwa mlinzi, ngao na mtetezi wa wanawake badala ya kuendeleza upotoshaji na uhadaifu wa wazi ambao ulikuwa haukubaliki na kampuni ya mitandao ya kijamii. Kupitia kitendo hichi, Facebook imejiunga na kifungu kisichopendwa cha tawala za kimabavu na serikali za kisekula zenye misimamo mikali ambazo zinalenga kunyanyasa na kunyamazisha kupitia sera za kibabe, sauti za wanawake Waislamu ambao wameukataa uhuru wa kisekula na kukumbatia Uislamu kama msingi wa kitambulisho chao na kutafuta mabadaliko ya kweli ndani ya ardhi zao kupitia shariah na nidhamu ya uhakika. Lakini, tunapinga kunyamazishwa! Ukweli utasikika na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu!

Tunawalingania wale wanaounga mkono kuenezwa kwa ukweli na haki, na wale wanaotaka kuondosha hali ya ukandamizaji ambao mamilioni ya wanawake wanapitia hivi leo na kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya ardhi za Waislamu, tafadhali waunge mkono ukurasa wetu mpya kwa kuupenda, kuusambaza na kuufuata: https://www.facebook.com/WomenandShariah2.

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِؤُواْ نُورَ اللّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللّهُ إِلاَّ أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake japo kuwa makafiri watachukua. [Al-Tawba: 32]

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.domainnomeaning.com
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu