Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 17 Muharram 1443 | Na: 1443 H / 002 |
M. Jumatano, 25 Agosti 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watoto wa Syria Wanauawa, Lini Watanusuriwa?!
(Imetafsiriwa)
Mnamo siku ya Ijumaa, 20/8/2021, majeshi ya Assad na mshirika wake, Urusi, waliulenga mji wa Kansafra kwa makombora kadhaa, yaliyopelekea vifo vya watoto 4 kutoka familia moja na kujeruhiwa kwa raia wengine wawili. Majeshi haya mara kwa mara hulenga vijiji vya Jabal Az-Zawiya. Katika kisa kama hicho, vikosi vya Assad, mnamo Alhamisi alfajiri, vilitekeleza mauaji ya watoto 3, mama yao na mtoto mwengine katika kijiji cha Balshon, kama matokeo ya kumiminiwa mabomu na makombora ya Kirasnopol ya Urusi.
Ni mauaji, huku maana ya ibara zote zikiashiria ugaidi, jinai na ukatili. Miili ya watoto ilipulizwa vipande vipande, mkono tu ndio uliobakia kutoka kwao ambapo baba wa mmoja wa wahasiriwa hao aliwaaga kwa maumivu makali ya dhulma kwani alitamani kuona uso wa mwanawe kumtazama kwa mara ya mwisho.
Kwa hivyo, magaidi ni kina nani?! Watoto hawa wasio na hatia waliokuwa wamelala, au wauaji wao wahalifu ambao wanaendelea kuwadhuru wao na wanawake? Takriban watoto 13 wameuawa kaskazini magharibi mwa Syria katika siku tatu zilizopita, wengi wao walikuwa na umri wa kati ya miaka 4 na 14, akiwemo mtoto mmoja ambaye alikuwa bado hajatimu umri wa mwaka mmoja, kwa mujibu wa shirika la Save the Children, sasa ni ugaidi gani upi wanaongelea?! Je! Wao sio wanaoutekeleza na kuutawala? Mwenyezi Mungu anatutosheleza na ndiye Msaidizi Bora.
Wananyanyua miito ya uwongo na hufanya kazi ya kuavya majaribio ya watu wa Ash-Sham ili kujikomboa kutokana na dhulma na uhalifu wa Bashar na kuipindua serikali yake ya kikafiri inayopiga vitana kuanzishwa kwa mradi wa hadhara tukufu, ambao sifa zake zimeanza kuonekana kwenye upeo wa macho. Licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mnamo tarehe 5/3/2020, mchinjaji huyo na wafuasi wake hawakutii makubaliano hayo na waliendelea na uhalifu wao dhidi ya watu wa Idlib. Hakika, wao - na haswa Urusi – hawachukulii mashambulizi na mauaji yao kama ukiukaji wa makubaliano hayo ya usitishaji vita, bali ni ulipuaji mabomu wa kawaida!
Mateso ya watoto wa Syria yamezidi kuwa mabaya kutokana na vita, na uhamiaji wa kulazimishwa na kuhamishwa makaazi, ambayo ilisababisha wengi wao kufanya kazi ili kukidhi mahitaji ya familia zao, na kuwahatarisha kifo "chini ya rundo la takataka katika jaa la taka karibu na mji wa Idlib wakati wakikusanya vitu ambavyo vinaweza kutumika na kuuzwa.” Kwa hivyo, magaidi ni kina nani?! Ni hawa watoto wasio na hatia ambao hawakujua chochote juu ya maisha isipokuwa taabu na shida, au ni wale wahalifu wanaoeneza kifo na uharibifu?
Enyi watu wetu mjini Idlib na Ash-Sham: Watoto ndio mustakbali na ndio wanaoendeleza maisha. Kile ambacho Bashar mhalifu na wasaidizi wake wanakifanya sio chochote bali ni juhudi za kuavya azimio lenu na kukukatisheni tamaa hadi mjisalimishe kwake, mumuunge mkono na muachane na mapinduzi yenu ya baraka ambayo mnataka kuangushwa kwa serikali yake dhalimu, na kutawala kwa Mfumo imara na adilifu wa Mwenyezi Mungu.
Je! Ni ulimwengu tofauti ulioje kati ya mfumo usioheshimu kizazi chochote kwenu wala ahadi, unaua watoto na wanawake na kueneza kifo na uharibifu, na baina ya Mfumo wa Mola wa walimwengu unaokataza uovu na kueneza huruma, utulivu na ustawi. Kutoka kwa Nafi kutoka kwa Ibn Umar (ra):
«أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ رَأَى فِي بَعْضِ مَغَازِيهِ امْرَأَةً مَقْتُولَةً فَأَنْكَرَ ذَلِكَ وَنَهَى عَنْ قَتْلِ النِّسَاءِ وَالصِّبْيَانِ»
“…kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), aliona katika baadhi ya vita vyake maiti ya mwanamke aliyeuwawa, basi akakemea hilo na akakataza kuuwawa kwa wanawake na watoto” [Imesimuliwa na Ahmad].
Enyi watu wetu mjini Idlib na Ash-Sham: maadui wameitana na kuyashambulia mapinduzi yenu ya baraka. Mlivunjwa moyo na wale wanaodai kuwa ni (marafiki) zenu, na humna chengine ila kushikilia mstari wa uhai wa kheri (wema) hapa duniani na Akhera, na shikamaneni na kauli mbiu yenu, mliyoinyanyua tangu kuanzishwa kwake, "Ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo, fanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na mdai Mfumo wa Mola wa walimwengu utabikishwe juu yenu na muwe wa kwanza kuinusuru Dini hii na kurudisha heshima yake. Wallahi, hili ni heshima kubwa kwenu.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) domainnomeaning.com |