Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 7 Dhu al-Qi'dah 1442 | Na: 1442 H / 040 |
M. Ijumaa, 18 Juni 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji ya Kuogofya ya Familia Moja ya Kiislamu jijini Ontario, Canada, Mizizi Yake ni Hofu ya Uislamu Isababishwayo na Hotuba za Kisiasa na Sera za Kisekula za Dola za Kimagharibi
(Imetafsiriwa)
Mnamo Siku ya Jumapili tarehe 6 Juni, familia moja ya Kiislamu jijini London, Ontario, Canada iliuawa katika shambulizi la kuogofya la kigaidi na dereva ambaye aliwakanyaga kwa makusudi ndani ya lori, na kumuua nyanya mwenye umri wa miaka 74, baba mwenye umri wa miaka 46, mama mwenye umri wa miaka 44 na binti mwenye umri wa miaka 15. Mvulana wa miaka 9 pia alijeruhiwa vibaya. Polisi walisema kwamba kilikuwa ni "kitendo kilichopangwa tayari, kilichochochewa na chuki" na kwamba "wahasiriwa walilengwa kwa sababu ya imani yao ya Kiislamu." Shambulizi hilo linajiri kati ya wimbi linalokua la hofu ya Uislamu na chuki dhidi ya Waislamu nchini Canada. Katika miezi ya hivi karibuni, wanawake wengi wa Kiislamu waliovaa Hijab wameshambuliwa jijini Toronto, Montreal, London na miji mingine. Mnamo Septemba 2020, mwanamume Mwislamu aliuawa kwa kudungwa kisu nje ya msikiti huko0 Toronto. Na miaka minne iliyopita, mtu mwenye hofu ya Uislamu aliwaua watu 6 walipokuwa wakiswali katika Msikiti wa Jiji la Quebec. Kwa kweli, kulingana na Takwimu Canada, uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu nchini umeongezeka zaidi ya mara tatu kati ya 2012 na 2015, na zaidi ya visa 180 dhidi ya Waislamu mnamo 2019. Zaidi ya hayo, uchunguzi wa 2016 na Baraza la Wakala za Ontario Linalohudumia Wahamiaji, uligundua kuwa ni asilimia 32 pekee ya watu wa Ontario walikuwa na "hisia chanya" ya Uislamu, huku utafiti mmoja wa 2017 uliofanywa kwa Radio Canada ukiripoti kwamba raia mmoja kati ya wanne wa Canada angependelea marufuku ya uhamiaji wa Waislamu, na asilimia 51 ya wahojiwa nchini Canada na asilimia 57 jijini Quebec wakisema kwamba wanahisi kuwapo kwa Waislamu nchini kuliwafanya "kwa kiasi fulani" au "kuwa na wasiwasi sana" juu ya usalama.
Mitazamo kama hiyo iliyo enea, chuki na mashambulizi ya kidini dhidi ya Waislamu hayatokei ndani ya ombwe. Ni matokeo ya kuwaonyesha kwa mpangilio Waislamu na imani zao za Kiislamu kama watu waovu ambapo imefanyika katika dola nyingi za kisekula za Kimagharibi kwa miongo miwili iliyopita na wanasiasa wa rangi zote, vyombo vikuu vya habari na taasisi na mashirika anuwai. Hotuba za uchochezi za hofu ya Uislamu na wanasiasa na waandishi wa habari – dhidi ya kila kitu kuanzia hijab na niqab hadi sheria za ndoa na familia za Kiislamu, kutenganisha jinsia, kutetea matukufu ya Mtume (saw), kuunga mkono ukombozi wa Palestina kutoka kwa Mayahudi wanyakuzi, imani katika Ummah wa kiulimwengu wa Kiislamu, na nusra ya utekelezaji wa mfumo wa Kiislamu katika nchi za Waislamu - yamehalalishwa na kufichwa chini ya uongo wa "mjadala wa kisiasa", 'uhuru wa kujieleza' na 'kulinda maadili ya kidemokrasia'. Kwa kuongezea, utenganishaji kwa nguvu wa kanisa na dola na serikali za kisekula zenye msimamo mkali kumewanyanyapaa, kuwatenga, na kuwaonyesha kuwa waovu Waislamu walio wachache na kuwachukulia kama raia wa daraja la pili - kama inavyodhihirishwa na marufuku kwa imani anuwai za Kiislamu, kama hijab na niqab. Mswada Quebec wa 21 kwa mfano, unawapiga marufuku wafanyikazi wa sekta ya umma kuvaa hijab, "imeingiza hofu ya Uislamu ya kijinsia ndani ya taasisi" na imelaumiwa kwa kuongezeka kwa mashambulizi kwa wanawake Waislamu waliovaa mavazi ya Kiislamu katika mkoa wa Canada. Wakati huo huo, hatua mbaya za kupambana na ugaidi na msimamo mkali na serikali za kisekula za Kimagharibi zimewaorodhesha idadi ya Waislamu kama jamii za watuhumiwa, na adui wa ndani, kwa sababu ya kukuuza riwaya za kirongo ambazo zinachanganya imani za kisiasa na kijamii za Kiislamu pamoja na msimamo mkali na ghasia, na matishio ya usalama wa kitaifa, na kusababisha Waislamu kufanyiwa uchunguzi na ukamatwaji wa kibaguzi. Ikiwa ni sheria ya ugaidi ya C-51 ya Canada ambayo inalenga Waislamu kwa ufuatiliaji na kuwekwa kizuizini; au mswada wa Ufaransa wa kujitenga na mkakati wa KUZUIA wa Uingereza ambao unawanyanyapaa Waislamu kwa imani zao za Kiislamu; au 'ramani ya Kiislamu' ya kitaifa ya Austria ambayo inalitambulisha eneo la misikiti na mashirika ya Waislamu nchini kuupiga vita 'Uislamu wa kisiasa' - wote wanawajibika kuchochea moto wa hofu ya Uislamu na mashambulizi dhidi ya Waislamu.
Hofu hii ya Uislamu inayofadhiliwa na dola imechochewa na serikali za kisekula zinazojihusisha katika 'siasa za hofu' kupitia kuonyesha hisia ya kitambulisho cha Uislamu kwa Waislamu kama tishio kwa jamii zao kupigana na usilimishaji wa Waislamu wa Magharibi na kimataifa. Imeunda mazingira mwanana ya mauaji ya kiubaguzi wa rangi na ndio msukumo ulio nyuma ya janga la chuki dhidi ya Waislamu ambayo imetanda katika dola za Kimagharibi leo. Hili ni thibitisho ziada la jinsi mfumo na nidhamu ya kisekula zilivyo na dosari ya kimaumbile, zenye kugawanya watu, ubaguzi na hatari, na kwa nini kama Waislamu, tunahitaji kuuwasilisha Uislamu kama mfumo badali na muundo uliojaribiwa wa namna ya kuleta utulivu wa kweli na heshima baina ya watu wa imani tofauti za kidini.
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) domainnomeaning.com |