Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  24 Dhu al-Hijjah 1437 Na: 1437/ 08 H
M.  Jumatatu, 26 Septemba 2016

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Sheria ya Dhidi ya Ugaidi Haikukusudiwa Kupambana na Uislamu?

Mara tu baada ya kuuwawa kwa wasichana watatu wa Kiislamu, waliokuwa wakishukiwa kushambulia Kituo cha Polisi cha Central jijini Mombasa, kama kawaida tukio hili lilidaiwa ni kupambana na misimamo mikali, licha ya hayo kiuhalisia, ni mbinu iliyo kusudiwa kuihofisha jamii ya Waislamu ndani ya majumba yao wenyewe. Washukiwa hao tayari washabandikwa lakabu za "magaidi waliojifinika", kama ilivyo ripotiwa na yale yanayoitwa kuwa ni mashirika tegemewa ya habari nchini na kimataifa. (Kenyan officers kill three veiled attackers in assault on ... - CNN.com www.cnn.com/2016/09/11/africa/kenya-police-station-attack/.Giving)  Huku Waislamu wengi wakiwa katika njia panda, wasijue ima kukemea shambulizi hilo, au kuwakana washukiwa hao! Kadhia muhimu zaidi hapa ni kujua athari/matokeo ambayo kwa kawaida hufuata baada ya matukio kama haya ya kusikitisha. Sisi, Hizb ut Tahrir Kenya, hivyo basi tunachukua fursa hii kufafanua nukta zifuatazo:  

Kwanza: Tangu kupitishwa Mswada Dhidi ya Ugaidi, ni dhahiri shahiri kuwa polisi wamekuwa wakijihusisha na mauaji nje ya sheria, aghalabu bila ya ima uchunguzi wa kina wa jambo hili, au bila ya agizo la mahakama. Polisi aghalabu wametuhumiwa kuvamia nyumba za washukiwa, kupandikiza silaha na kuwapiga risasi washukiwa. Tungependa kuonya vikali kuwa tukio hili lisitumiwe kama kawaida kuendeleza ukandamizaji wa jamii za Waislamu ambao sasa umefikia kilele, kuwatia hofu Waislamu hadi kufikia kuogopa kushikamana na dini yao. 

Pili: Vichwa vikuu vya habari katika vyombo vikuu vya habari: 'walikuwa ni magaidi waliojifinika waliovaa buibui nguo nyeusi inayo valiwa na wanawake wa Kiislamu ambayo hufinika miili yao]", hili laashiria waziwazi dori ya vyombo vya habari ambapo vinafanya kazi kwa karibu na serikali katika vita dhidi ya Uislamu. Vyombo hivi vya habari vinajenga kwa makusudi rai jumla ya kuwadhalilisha Waislamu; na mavazi yao kuwa ni hatari kwa usalama. Ilhali ukweli ni kwamba Uislamu ni mfumo ambao unasimama dhidi ya aina yoyote ya unyanyasaji na umwagaji damu muovu.

Tatu: Sera mbaya ya kigeni ya dola za Kimagharibi ikichanganywa na sheria za kuchukiza kama si za kuhadaa dhidi ya ugaidi huchochea zaidi vitendo vya kigaidi! Uislamu umeharamisha pakubwa uvamizi wa nchi kwa lengo la kuiba rasilimali zao asili na kuwakoloni kwani hili huchangia vitendo vya utovu wa usalama. Hapa ni lazima ieleweke kwamba njama au utapeli wa dola katika vitendo vya kigaidi ni katika kuendelea kupatiliza fursa ya kuwanyanyasa raia wao wenyewe na kuwafanya wasijue kuwa chimbuko la mateso na majanga yao yanatokana na mfumo wa kirasilimali. Ni nani asiyejua kwamba mfumo wa kirasilimali ndio chanzo cha ukosefu wa usalama, ufisadi, mauaji, ukabila na idhilali nyinginezo nyingi? 

Nne: Ni lazima ifahamike kuwa kuna njama ya kimataifa, inayo ongozwa na Amerika ya kutangaza vita viovu na vya kinyama dhidi ya Uislamu, kwa mbinu yoyote ile chini ya kisingizio cha vita dhidi ya ugaidi, uvukaji mipaka, misimamo mikali na kadhalika. Kwani Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, ambao unaweza kuongoza watu barabara katika nyanja zote za maisha kisiasa, kiuchumi na kijamii. Ni jambo lisilokuwa na budi kwa Amerika kuendelea kutangaza vita vya kudumu dhidi ya Uislamu kama mfumo mbadala, kwa mbinu zote kwa kuhofia kuvunjika kwa mfumo wake wenyewe na kubadilishwa kwa Uislamu. Ni wajibu kwa Waislamu kufahamu kuwa njia thabiti pekee ya mabadiliko, ni ile iliyo fafanuliwa na Mtume (saw), ambaye licha ya kufikwa na aina zote za unyama na mauaji mabaya chini ya minyororo ya Ujahiliya, kamwe yeye (saw) hakugeukia ghasia, unyama wala ukatili mpaka akafaulu kuasisi Dola yake ya Kiislamu mjini Madinah.        

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu