Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  24 Jumada I 1441 Na: 1441 / 06
M.  Jumapili, 19 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bajeti ya Mwaka 2020 ni Muendelezo wa Madhara ya Ufisadi wa Kiuchumi wa Kirasilimali Tutafurahia Suluhisho pekee kupitia Nidhamu ya Kiuchumi ya Dola ya Khilafah
(Imetafsiriwa)

Bunge la Chini la Jordan mnamo Jumatano jioni, 15/01/2020, lilipitisha kielelezo cha sheria ya bajeti ya serikali ya mwaka 2020 na kielelezo cha bajeti ya mwaka ya taasisi huru za Ummah. Ama bajeti ya mwaka 2020, imelaaniwa zaidi kuliko zilizoitangulia kwa kuongezeka viwango na asilimia, ambayo ni muendelezo wa mbinu ya utegemezi wa kisiasa wa kikoloni tangu kuanzishwa kwa serikali hii, ambayo iliunganisha uchumi wake, maisha na kuendelea kwa msaada wa kigeni na kodi mbali mbali na kuzuia kila kitu ambacho kitaufanya uchumi wake kujitegemea kulingana na utajiri wake uliofichwa ambao uchimbaji wao na uwekezaji ni marufuku. Sera yake ya kifedha, kama nchi zote za Waislamu, inategemea nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali ya Kimagharibi iliyotunga sheria ya kila mwaka inayoitwa Sheria ya Bajeti ambayo inaweka sehemu za mapato, matumizi, upungufu au ziada, na inahusishwa na mipango ya mabadiliko ya kiuchumi ya kikoloni ya kilafi na zana zao kama vile Shirika la Fedha la Kimataifa.

Bajeti hizo zinapelekea kufilisika na kuporomoka siku baada ya siku, na ziko kwenye mwenendo hatari wa juu kuhusiana na upungufu na deni linalokua. Deni lote la Ummah hadi mwisho wa Septemba mwaka jana lilikuwa dinari bilioni 30.05 au dola bilioni 42, hesabu ni asilimia 96.7 ya Pato la Taifa lililokadiriwa kwa mwaka wa 2019, kulingana na Wizara ya Fedha, ambapo takwimu za bajeti zilionyesha kuongezeka kwa mapungufu ya dinari bilioni 1.247, au dola bilioni mbili bila ruzuku ya nje, ikilinganishwa na mwaka jana tu, tukijua kuwa zaidi ya asilimia 90 ya mapato ya bajeti yatokamana na ushuru na mapato kutokamana na kuuza bidhaa, huduma na faini, yaani kutoka katika mifuko ya Ummah kwa ujumla.

Kuhusu bajeti ya ufadhili, ilifika zaidi ya dinari bilioni 6, kiwango kikubwa katika hiyo kwa kweli, ni mikopo ya riba ya nje na ya ndani, ambayo hutumika zaidi kulipia madeni ya ndani na nje na mapungufu ya kila mwaka, pamoja na matumizi ya bajeti, pamoja na deni komavu lenye thamani ya dinari bilioni 1.4 ya riba haramu kutoka katika deni la Ummah.

Vipi bajeti kama hizi, zinazoshuka kutoka mbaya hadi mbaya zaidi na ambazo ukuaji wa kiuchumi hupungua kila mwaka mpaka kufikia asilimia 1.9, kama serikali inavyodai, wanawezaje kuiokoa nchi na watu kutokamana na mporomoko ujao ambao unaonekana mbele ya macho ya kila mtu, isipokuwa kwa kudumisha uboreshaji wa vifaa vyao vya uokoaji kutokamana na zana za Makafiri  Wakoloni Wamagharibi wa Amerika na Ulaya ili kuiruhusu serikali kudumu katika kutumikia maslahi ya kisiasa na kiusalama ya Wamagharibi kwa kuona kwamba nidhamu ya utegemezi ilimradi inafanikisha maslahi haya, na kwa kiwango cha chini ambacho hakitoshelezi njaa ya watu, lakini badala yake kutosha kufadhili bajeti hizi ambazo wanalipa kwa kuridhika au kwa vitisho?

Tunarudia hapa yale ambayo tulisema awali kuhusu suluhisho la janga la kiuchumi nchini Jordan, na hatutachoka kurudia; kwamba tatizo sio uchumi kimsingi lakini badala yake ni tatizo kubwa la kisiasa ambalo liliibuka kwa kujitokeza kwa umbile la Jordan kwa njia ya kikoloni ambayo Kafiri Mkoloni, Muingereza na kisha Mmarekani, walitaka kukidhi maslahi yao katika eneo hilo, ambayo ni pamoja na kuipa serikali ya Kiyahudi njia za kuishi kwa  usalama,  kuwa na uchumi na mikataba ya kudhalilisha ambayo imegharimu Ummah utajiri wake na maisha ya watoto wake, ambayo serikali hutumia kuwatumikia Wakoloni hawa wanaoshindana kwa ajili ya maslahi yao kwa gharama ya Ummah katika nchi za Waislamu.

Nidhamu ya kiuchumi haiwezi kubadilishwa na aina ile ile ya nidhamu fisadi ambayo imeunda sera ya fedha kwa kuboresha ustadi hapa au pale au kwa kukabili watu wachache wafisadi wanaozalishwa na nidhamu fisadi ya kiuchumi kama hii, kama inavyotokea kila mwaka pamoja na mchezo wa mwisho wa mwaka katika bunge ambao wanachama wanaipiga serikali kwa maneno yao na kisha kupitisha bajeti na kuipongeza serikali kwa mafanikio yake, na ahadi ya malipo ya ziada matupu na foleni za soko kama vile kupunguza kodi ya uuzaji wa maziwa, kabichi na saladi!

Enyi Watu:

Tatizo la kimsingi ni kutengwa kwa Uislamu na nidhamu yake ya kiuchumi kutoka maishani na kuibadilisha kwa nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali ambayo inatenganisha dini na maisha na kwa hivyo kutoka kwa uchumi ambao wanadamu wote wanateseka kutokamana na vurugu zake. Katika dola ya Kiislamu, sera ya fedha inaunganishwa kwa lazima na Aqeedah ya Kiislamu ambayo inaifunga kikamilifu na nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu. Katika Uislamu, mistari ya bajeti ya mapato yake na matumizi yamefungika, na ni ya kudumu. Hairuhusiwi kuchukua pesa kutoka kwa wengine, na haitumiwi kwa njia isiyo halali. Na kwa sehemu ya mapato, ni vyanzo vilivyoainishwa kutoka kwa umiliki wa Ummah na umiliki wa serikali, kama vile Kharaj na Ngawira (Fai’) na vile vile Zaka. Vyanzo hivi ni vya kudumu, haviamuliwi na Khalifah au Baraza la Ummah. Na kwa sehemu ya matumizi, yameainishwa pia katika Uislamu na hukmu za sheria, na yanahusiana na jinsi vyanzo vya mapato kutoka umiliki wa Ummah, umiliki wa serikali, na Zaka, yanatumiwa na hili haliwezi kupitishwa na Khalifah, au baraza la Ummah.

Enyi Watu wa Jordan:

Kwa hivyo, suluhisho liko katika kushughulikia ufisadi wa kweli wa kiuchumi kwa kuachana na nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali, sera na zana zake, kutoka kwa kanuni zake zinazosimamiwa na shirika la kimataifa la kikoloni linalo koloni kupitia madeni na maagizo mabaya ya mageuzi, na hatutochoka kueleza kuwa suluhisho linaweza kuwa tu kwa kurudi kwa njia ya Uislamu na kuchukua suluhisho kutoka kwa uamuzi wake. Chama kimeonyesha katika makongamano mbali mbali ya kiuchumi ya kiulimwengu na katika vitabu vyake na kielelezo cha Katiba, nidhamu ya kiuchumi katika Uislamu, ambayo bila shaka sio tu inasuluhisha shida za kiuchumi za Waislamu, lakini ni mbadala kwa wanadamu wote ulimwenguni, kwani nidhamu ya kirasilimali inazingatia riba, uporaji, uizi, unyonyaji, uhasama na ushawishi. Hakuna shaka kuwa yote haya yatarudi hivi karibuni juu ya kutimia kwa bishara za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa kurudi Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi mungu.

(لِمِثْلِ هَٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ)

“Kwa mfano wa haya na watende watendao.” [As-Saffat: 61]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu