Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  15 Shawwal 1443 Na: 1443 / 24
M.  Jumapili, 15 Mei 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mkutano wa Mfalme na Biden ni Kujitolea kwa Kuendeleza Utawala wa Kikoloni wa Amerika wa Jordan kwa Badali ya Kutafuta Uthabiti Uliopo wa Utawala kupitia Uzi wa Usimamizi

(Imetafsiriwa)

Taarifa ya Ikulu ya White House ilisema mnamo Ijumaa, Mei 13, 2022, “Rais [Biden] anafuraha kumkaribisha Mtukufu Mfalme Abdullah II wa Jordan na Mwanamfalme wake Mtarajiwa Hussein kwenye Ikulu ya White House Mei 13, 2022. Ziara ya Mfalme Abdullah kwenda Washington, ambayo ni ya pili katika Utawala wa Biden, itaimarisha urafiki wa karibu na ushirikiano wa kudumu kati ya Marekani na Jordan. Jordan ni nguvu muhimu kwa utulivu katika Mashariki ya Kati na mshirika wa kimkakati wa Marekani. Rais alisisitiza uungaji mkono wake mkubwa kwa suluhisho la mataifa mawili kwa mzozo wa 'Israel' na Palestina na alibainisha haja ya kuhifadhi hadhi ya kihistoria katika Haram al-Sharif/Mlima wa Hekalu. Rais pia alisifu dori muhimu ya Ufalme wa Hashemiya wa Jordan kama msimamizi wa maeneo matakatifu ya Kiislamu jijini Jerusalem.

Mkutano huu wa saa moja ulitanguliwa na mikutano kadhaa iliyofanywa na Mfalme Abdullah II tangu mwanzo wa ziara yake nchini Marekani na wafanyakazi wa utawala wa Marekani, viongozi wa Congress na wanachama wa Kamati za Mahusiano ya Nje,  Ugawaji, na Huduma za Kijeshi za Seneti, pamoja na Kamati za Huduma za Kijeshi na Mambo ya Kigeni, na Kamati Ndogo ya Wizara ya Matumizi. Wizara ya mambo ya nje na shughuli za kigeni na programu zinazohusiana katika Baraza la Wawakilishi.

Ziara hii ilitanguliwa na mvutano na vurumai kutoka umbile la Kiyahudi na mashambulizi ya makundi ya walowezi kwenye Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na Ukingo wa Magharibi, licha ya mikutano ya mfalme huyo na viongozi wa Kiyahudi na Abbas katika kujaribu kutuliza na kuhifadhi hali iliyopo, ambayo ilishindikana kiasi kwamba viongozi wa Kiyahudi walitishia kuhujumu usimamizi wa Wahashemiya licha ya usalama na uratibu wa kiuchumi Baina yao, ambao haujawahi kuingiliwa. Kwa hiyo, ziara ya Mfalme nchini Marekani, na mikutano yake na nguzo za serikali za kundi la washawishi wakuu, ikiwa ni pamoja na mawaziri wa ulinzi, usalama wa taifa, jeshi, Spika wa Baraza la Wawakilishi, na kamati za Congress katika ngazi ya juu kabisa.

Pia alikutana na Mkuu wa Majeshi ya Marekani na Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Marekani binafsi bila ya kuwepo kwa maafisa wengine wa Jordan, jambo ambalo linatabiri kuwepo kwa matakwa mapya ya kijeshi ya Marekani ambayo yanafungua njia kwa kipindi kijacho cha utulivu katika serikali kulingana na madai hayo na kuyajibu, na Mfalme alikutana na washawishi wa kituo cha kisiasa cha Marekani, kuelezea umuhimu wa dori inayowasilishwa na kuchezwa na utawala nchini Jordan ili kuhifadhi maslahi ya Marekani katika eneo. Katika jaribio la kupata uungwaji mkono na kuunga mkono uthabiti wa kisiasa wa utawala huo ghasibu nchini Jordan, na kuhakikisha nafasi nzuri ya kuhifadhi nafasi yake katika kile kinachoitwa uhifadhi wa Hashemiya wa matakatifu ya Kiislamu ambayo Rais wa Marekani ameipongeza katika taarifa yake ya Ikulu ya Marekani, White House. Mkataba wa maelewano pia unajadiliwa, kuanzia mwaka ujao, kwa ajili ya msaada wa Marekani kati ya Marekani na Jordan kwa kuzingatia matakwa na makubaliano ya kimkakati ya kiuchumi, kijeshi na kiusalama ambayo yalikubaliwa wakati wa mikutano ya Mfalme na nguzo ya utawala wa Marekani, kwani za zamani zinaisha muda wake mwaka huu.

Licha ya makubaliano ya kijeshi mwaka jana na kambi za kijeshi na marupurupu yaliyotolewa serikali kwa utawala wa Marekani na nguzo zake, suala la kisiasa la Marekani kuridhika na kudumisha uhai wa utawala huo katika hadhi yake iliyopo bado limesitishwa kwa mujibu wa athari za mzozo wa kikoloni ya utiifu wa kisiasa wa Uingereza na maslahi yake tangu kuwepo kwa utawala wa Hashemiya na maslahi ya Marekani, ambayo ina ushawishi wa kiuchumi na usalama na kijeshi, kupitia zana zake katika Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, misaada yake ya kifedha na madeni ya makubwa mno. Badala yake, mikataba na kambi za kijeshi ambayo nchi imefungulia, na anga na ardhi zake zimeporwa, na inapepea kupitia vivuli vya vyombo vya habari vya Marekani na mara kwa mara kiboko cha mageuzi ya kisiasa na kiuchumi nchini Jordan, kupambana na rushwa, uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari, na ubadhirifu wa utawala na mali zake ng’ambo.

Enyi Watu wa Jordan, Enyi Waislamu:

Sio siri tena kwenu kwamba watawala wenu walioteuliwa na mkoloni kafiri wa Kimagharibi si watiifu kwenu, iwe katika kushughulikia mambo yenu na kuhifadhi maslahi yenu, au kutetea nchi zenu ambazo mali na ardhi zao zimeruhusiwa kuwanufaisha maadui zenu. Bali wanafanya kazi ya kufikia maslahi yao ili kuhifadhi viti vya utawala wao, na kuifukarisha nchi yao, na wala hawajali kuhusu Msikiti wa Al-Aqsa, Palestina, au hata nchi wanazozitawala, isipokuwa kwa kiwango ambacho kinawadhamini. kunusurika kwao katika utawala na mzunguko huku wakifanikisha maslahi ya Marekani, Uingereza na Magharibi, na hao ni maadui zenu waliomwaga damu zenu tangu walipoivunja dola yenu, Khilafah, hivyo umbile oga la Kiyahudi limekuwa likiua, kuharibu, na kurudisha shukrani kwa unyonge na fedheha ambayo watawala wenu walishuka kwa kuimarisha uhusiano wao wa kawaida wa usalama na kisiasa nalo.

Kuondokana na unyonge huu na kurudisha hadhi na fahari ya Ummah, ambazo umeishi nazo kwa mamia ya miaka, na kuikomboa nchi yake iliyokaliwa kwa mabavu, na kuukata mkono wa wakoloni dhidi ya kuiba uwezo wake, kunaweza tu kupatikana kupitia kuregea kwa dola ambayo amewahi kupata haya yote. Dola ya Khilafah inayohamasisha na kuongoza majeshi yake kuikomboa Palestina yote, na kwa hakika nchi zote za Kiislamu zilizokaliwa kwa mabavu, jambo ambalo ni jepesi, Mwenyezi Mungu akipenda, kwa taifa linalotamani kuuawa shahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

 (قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ)

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [At-Tawbah: 14]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu