Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  28 Safar 1442 Na: 1442 / 03
M.  Alhamisi, 15 Oktoba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kukosekana kwa Utekelezwaji wa Sheria ya Mwenyezi Mungu ni Uhalifu Mkubwa ambao Hutengeneza Uwanja wa Kuzaana kwa Wahalifu na Kukwepa Kwao

(Imetafsiriwa)

Uhalifu wa kushambuliwa kwa kijana wa Zarqa ulitikisa hisia za jamii nchini Jordan kutokana na kuogofya kwake na kutokea kwake mchana kweupe uliofanywa na genge la wahalifu ambalo limezoea kufanya uhalifu mbele ya vyombo vya usalama na mahakama, katika wakati ambapo serikali nchini Jordan inazungumzia kuhusu ulinzi na usalama ambao watu wanafurahia, huku umasikini, ukosefu wa ajira na njaa vikiwa vimefikia kiwango ambacho hakiangazi ulinzi wala usalama, na huku ikizungumzia kuhusu utawala wa sheria, hakuna ubwana hata kwa dhulma hii, sheria dhalimu iliyoundwa na wanadamu ambayo imesababisha uhalifu, dhulma na uvamizi.

Ukweli ni kwamba haya yote yanatokea kwa sababu ya kukosekana kwa sheria ya Mwenyezi Mungu na kutotekelezwa kwa vifungu vya Uislamu, dini ambayo Mwenyezi Mungu ameikubali kwetu, na ndani yake akatunga sheria, vifungu na kanuni zinazodhibiti maisha yetu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, ambazo zinalinda jamii, watu wake binafsi na vipengee vyake vyote, na huyafanya maisha kuwa salama na amani, yaliyofungwa kutokana na ufisadi na wafisadi na kufukuza uhalifu na sifa ya uhalifu, kwani usalama wetu uko katika kutekeleza sheria ya Mola wetu,

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللّهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿

“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Maida: 50].

Uhalifu mkubwa na ardhi yenye rutuba kwa uhalifu mwingine, ikiwemo mauaji, utekaji nyara, unyanyasaji muovu na unyanyasaji wa kikatili, ni matunda ya sheria hii mbovu iliyotengenezwa na wanadamu ambayo mabaraza ya mabunge ya wawakilishi yanazitunga - ambayo leo wanaalika watu kushiriki katika uchaguzi wao - sheria hii ambayo haihifadhi uhai wa mwanadamu, haifikii uadilifu, na haidhamini riziki za watu na elimu, na haitibu wagonjwa wao, bali ndiyo inayoeneza ufisadi katika aina na zana zake zote.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 (يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالاً بَعِيداً)

“Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali.” [An-Nisa: 60].

Kwa hivyo, wahalifu ambao wamezoea uhalifu wanawezaje kuachwa huru kufanya uharibifu duniani chini ya macho ya serikali na vyombo vyake vya usalama, na kutotosheleza na ufisadi wa sheria na kanuni ambayo mahakama inatii, na kujitia upofu kwa maamuzi yao ya jinai yaliyotangulia pasi na adhabu za kuzuia, lau kama si kwa ufisadi wa mfumo wa utunzi wa sheria na kanuni iliyoundwa na mwanadamu isiyotosheleza na kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uadilifu kati ya watu, na unafiki na uingiliaji wa wapatanishi waovu kutoka kwa maafisa katika usalama, mahakama na mabaraza ya mabunge yenyewe, kana kwamba tunaishi sheria ya msituni?

Mojawapo ya uhalifu wa kinyama zaidi ni kwa huduma za usalama za serikali kushughulishwa na ufuatiliaji wa wabebaji wa Dawah ambao wanasema Mwenyezi Mungu ndiye Mola wetu na kulingania utabikishaji wa Uislamu ili usalama wa kweli utimie, ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameuonyesha katika maneno yake:

 (الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ)

“Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka.” [Al-Ana’m: 82].

Badala yake, juu ya hayo wanawakamata wabebaji wa Dawah, wanawahangaisha wake na watoto wao, wanakiuka utakatifu wa nyumba zao, na kuruhusu wafisadi na wahalifu kuleta uharibifu duniani bila kizuizi na hakuna adhabu za kuzuia ambazo Mwenyezi Mungu (swt) amezionyesha katika Wahyi ulio waziwazi,

 (وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ)

“Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike.” [Al-Baqara: 179].

Enyi Watu… Enyi Watu wetu nchini Jordan:

Tunawalingania muzikatae sheria hizi zilizotengenezwa na wanadamu na mfumo uliooza uliotengenezwa na wanadamu, na mufanye kazi ili kubadilisha hali hii kimsingi na kwa ukamilifu kwa kurudisha hukmu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu na kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume inayosimamisha uadilifu kati yenu na kuleta adhabu dhidi ya wale waliokosea, na ambayo kwayo Uislamu na Waislamu wanaheshimiwa, na watu wote wanaishi maisha ya amani kwa usalama, utulivu na ustawi chini ya Uislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu