Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  13 Rabi' I 1446 Na: 1446 / 01
M.  Jumatatu, 16 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Majeshi ya Waislamu Yanasukumwa na Marekani Popote Inapotaka, Lakini Hayasukumwi na Uungwana wa Al-Mu'tasim!
(Imetafsiriwa)

Kanuni msingi ya majeshi ya Waislamu ni kwamba wabebe Aqida ya Kiislamu (itikadi); ipasavyo, haijuzu kwao kuchukua hatua yoyote mpaka wajue hukmu ya Mwenyezi Mungu kuhusu hilo. Lakini kwa bahati mbaya wamejisalimisha kwa watawala wasaliti na vibaraka, wakitii amri zao na kutekeleza maamuzi yao hata wakiwa katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Hatujui ikiwa hilo ni kwa ajili ya faida ya kidunia?! Mwenyezi Mungu (swt) amekuahidini radhi zake na pepo pana mithili ya Mbingu na Ardhi. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّ اللهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنْفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْداً عَلَيْهِ حَقّاً فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ مِنَ اللهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُمْ بِهِ وَذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ]

“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.” [At-Tawbah: 111].

Tunachokiona katika uhalisia wetu mchungu ni kwamba Marekani iliweza kuyakusanya majeshi ya Waarabu (Saudi Arabia, Imarati, Bahrain, Qatar, Oman, Misri, Syria na Morocco) dhidi ya watu wake wenyewe, kutekeleza mipango yake ya kudhibiti visima vya mafuta na maji ya vuguvugu katika Ghuba katika Vita vya Dhoruba ya Jangwa. Katika operesheni ambayo Amerika iliita ‘Odyssey Dawn’ dhidi ya Libya, ikiongozwa na NATO, Qatar, Imarati na Jordan ilishiriki kwa ndege za kivita. Nchi hizi hizi zilishiriki na vikosi vya bora kupigana ardhini. Mnamo Machi 2015, jeshi la Al Saud lilisukumwa na amri ya Amerika ya kupigana vita nchini Yemen, ambavyo bado vinaendelea, katika kile kilichoitwa Operesheni ‘Decisive Storm’. Vita hivi vya dhulma viliacha nyuma nchini Yemen mchanganyiko wa uhamishaji makaazi, njaa, kipindupindu, na mateso ya kibinadamu ambayo yanachukuliwa kuwa mabaya zaidi ulimwenguni, kulingana na Umoja wa Mataifa. Hii ni pamoja na ushiriki wa baadhi ya nchi za eneo kama vile Jordan, Uturuki na nyenginezo katika njama za kijeshi ambazo Marekani inatekeleza katika eneo hilo!

Shauku na shughuli zote hizi bila mafanikio, tunaziona zikiganda na kutonyosha kidole mbele ya jinai za Mayahudi ambazo ni aibu kwa wanadamu, na zimekuwa zikiendelea kwa karibu mwaka mmoja, na kusababisha zaidi ya mashahidi elfu 41 katika Ukanda unaoheshimika wa Gaza, ambao wengi wao ni wanawake na watoto, na mashahidi 692 katika Ukingo wa Magharibi, wakiwemo watoto 159, kulingana na data kutoka Wizara ya Afya ya Palestina.

Kilicho kibaya na uchungu zaidi kuliko hili ni kwamba tunamkuta mtumishi mdhalilifu wa Marekani, baada ya kutuma jeshi la Uturuki Afghanistan chini ya bendera ya NATO, akijigamba kuwa analituma ili “kutekeleza misheni zake nchini Syria, Iraq, Libya na Somalia kwa njia bora zaidi.” Inaonekana kana kwamba ameisahau Karabakh huko Azerbaijan, kana kwamba kwa kusema hili anawachokoza watu wa Gaza na watu wote wa Palestina, na hata Umma wote wa Kiislamu, kwamba anajua jinsi ya kulielekeza jeshi hili sehemu yoyote ile duniani, lakini pale ambapo bwana wake Marekani anataka, isipokuwa Masra ya Mtume, Kiblah cha kwanza cha Waislamu na ardhi yao tukufu, na kwa ajili ya kuwanusuru watu wa Gaza, yeye haijui njia!

Haya yote yanatokea huku majeshi ya Waislamu yaliyotokana na utajiri wa Umma bado yakiwa yamekita katika kambi zao yakingoja uamuzi kutoka kwa mtawala msaliti anayelilinda umbile la Kiyahudi, kulinda mipaka yake na kuwazuia wale wenye wivu wa ulinzi huo miongoni mwa Umma kutokana na kuwafikia na kuwanusuru ndugu na dada zao, kama watawala wa Misri na Jordan wanavyofanya.

Enyi Umma wa Kiislamu na Majeshi ya Waislamu: Jueni ya kwamba Mayahudi hawakudumu katika uadui wao na dhulma yao kwa sababu ya ushujaa, kwani wao ni waoga zaidi katika viumbe vya Mwenyezi Mungu, bali waliendelea kwa sababu wamejihisi salama pamoja nanyi na wakatambua ya kwamba nyinyi hamtatoka chini ya vazi la watawala wenu. Ikiwa mutakibakia katika hali hii, damu hii yote safi ya Waislamu itatoa hoja dhidi yenu Siku ya Kiyama, siku ambayo mali wala cheo havitakuwa na manufaa yoyote.

Hivyo basi tembeeni katika utukufu wa dunia hii na Akhera. Hizb ut Tahrir inakuombeni mutimize wajibu wenu wa Kiislamu, kupindua tawala hizi za khiyana, na kusonga ili kuwanusuru kaka na dada zenu. Ili ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt), ya ukhalifa, tamkini, na bishara njema ya Mtume wake (saw) ya kuitakasa Ardhi iliyobarikiwa kutokana na uchafu wa Mayahudi, itimie kwa mikono yenu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu