Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  12 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 13
M.  Jumatatu, 20 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kunguru Akiwa ndio Kiongozi wa Watu, Atawaongoza Kwenye Nyumba ya Uharibifu!
(Imetafsiriwa)

Baada ya zaidi ya miezi sita ya wadhifa wa spika wa bunge kuwa wazi kufuatia kufutwa kazi kwa spika wa zamani, Mohammed al-Halbousi na uamuzi wa Mahakama ya Shirikisho, bunge la Iraq lilifanya kikao chake maalum cha kumchagua spika mpya mnamo siku ya Jumamosi Mei 18, 2024. Baada ya hekaheka kati ya kambi za kisiasa katika kipindi hiki, ugombea ulipunguzwa hadi wabunge watatu: wa kwanza, Salem Al-Issawi kutoka Muungano wa Utawala unaoongozwa na Khamis Al-Khanjar; wa pili, Mahmoud Al-Mashhadani kutoka Muungano wa Maendeleo unaoongozwa na aliyekuwa spika wa bunge Mohammed Al-Halbousi; na wa tatu, ni mbunge huru Amer Abdul Jabbar.

Al-Issawi alipata kura 158, Al-Mashhadani alipata kura 137, na Amer Abdul Jabbar alipata kura tatu, na kura 13 batili. Kwa hivyo, suala hilo halikutatuliwa kwani hakuna mgombea hata mmoja aliyepata idadi inayotakiwa ya kura, ambayo ni (50+1) jumla ya kura 166, kwa mujibu wa Ibara ya 55 ya Katiba ya Iraq na Ibara ya 12, Kifungu cha 3 cha kanuni za ndani za Baraza la Wawakilishi.

Hata hivyo, kilichotokea ni kwamba kikao hicho kuligeuka uwanja wa vita vya majogoo, vya kurushiana ngumi na kila upande kumtishia mwenzake. Machafuko haya yote na tabia ya fedheha ilikuwa kwa ajili ya vyeo na faida za kibinafsi. Hili halikuwashangaza watu wa Iraq, ambao wamenawa mikono yao na utawala wa kijeshi ulioletwa na mvamizi wa Kimarekani, na wamezoea vitendo kama hivyo na vibaya zaidi.

Ndiyo, mvamizi wa Kimarekani aliweza kuuhadaa Ummah. Tangu ilipoikalia nchi hiyo, ilianzisha ramani ya utendakazi wake wa kisiasa yenye mfumo mbovu wa upendeleo wa kimadhehebu na katiba yake ya ovu, na kuacha utabikishaji wa mfumo huu kwa kundi la khiyana la kisiasa ambalo linadai kwa uongo kuchaguliwa na watu wa Iraq. Wanaegemea vyeo na faida, wakipigana juu yake kama punda wapiganavyo.

Kwa hiyo, tunasema: Maafa yote ya umma huu unaoteseka yanasababishwa na mfumo uliowekwa na mvamizi pamoja na katiba yake iliyojaa hatari. Ni katiba iliyoundwa kuleta matatizo, si kuyatatua, na kuiweka nchi katika dimbwi la machafuko ya kisiasa, yanayosukumwa na vikaragosi hawa walioajiriwa.

Enyi Waislamu, Enyi Watu wa Iraq: Hizb ut Tahrir, ni kiongozi asiyewadanganya watu wake, imekulinganieni kwa muda mrefu ili kuwaongozeni kutoka katika machafuko mnayoishi ndani yake. Imewaonyesha kwamba hakuna wokovu kwenu na mateso yenu isipokuwa kwa kufanya kazi ya kuondoa mfumo huu uliopandikizwa na mvamizi pamoja na uchafu wake uliokuja nao. Lazima mufanye kazi kwa bidii katika kutabikisha Sharia ya Mwenyezi Mungu na kusimamisha mfumo wa Kiislamu, ambao unabeba wokovu wenu, heshima, na kuinuliwa, chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema:

[لَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَاباً فِيهِ ذِكْرُكُمْ أَفَلَا تَعْقِلُونَ]

“Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?” [Al-Anbiya:10]. Hivyo, mtafanya nini? Je, mutaitika?

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu