Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  18 Rabi' I 1444 Na: 1444 / 06
M.  Ijumaa, 14 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kumchagua Rais wa Iraq na Kuundwa kwa Serikali Hakumalizi Mateso ya Watu wa Iraq
(Imetafsiriwa)

Baada ya Baraza la Wawakilishi la Iraq kushindwa, mnamo Alhamisi, tarehe 13 Oktoba 2022, kumchagua rais wa Iraq, liliweza katika kikao chake cha pili leo, Ijumaa, Oktoba 14, 2022, kumchagua mgombea Abdul Latif Rashid, ambaye alimpa mgombea wa Mfumo wa Uratibu wa Kishia jukumu la kuunda serikali ijayo.

Haya yanajiri baada ya mwaka mmoja wa kulemaa kisiasa tangu uchaguzi wa mapema wa mnamo tarehe 10 Oktoba mwaka jana, ambapo nchi hiyo ilishuhudia panda shuka za kisiasa kutokana na mzozo kati ya muungano wa Mfumo wa Uratibu unaoongozwa na Nuri al-Maliki kwa upande mmoja na vuguvugu la Sadri linaloongozwa na Muqtada al-Sadr kwa upande mwingine. Al-Sadr alishinda uchaguzi na muungano wake mkubwa zaidi haukuweza kuunda serikali, kutokana na sharti kwamba mgombea wa kiti cha urais lazima apate kura za theluthi mbili ya viti vya ubunge, ambapo Mfumo wa Uratibu ulikuwa makini kuzuia kufanikiwa, na jambo ambalo lilimfanya kiongozi wa vuguvugu la Sadri kutangaza kujiuzulu manaibu wake na kufuatiwa na kujiondoa katika mchakato wa kisiasa, hii ilisababisha wafuasi wake kuandamana mabarabarani na mzozo kati yao na wafuasi wa Mfumo wa Uratibu ulianza, na kusababisha makabiliano ya kisilaha wakati mwingine, ambapo Muqtada al-Sadr alitangaza kumalizika kwa maandamano hayo na kuachana kabisa na maisha ya kisiasa.

Baada ya hapo, Mfumo wa Uratibu ulitoa hoja kwa msisitizo wa kufanya kikao cha Bunge, na kufikia kile walichotaka, na raisi wa nchi akachaguliwa, ambaye alimuidhinisha mgombeaji wa uratibu kuchukua nafasi ya uwaziri, licha ya kuanguka kwa makombora tisa kabla ya kikao kufanyika, yakilenga Eneo la Kijani. Kitengo cha Usalama cha Vyombo vya Habari kilithibitisha kuanguka kwake karibu na Afisi ya Waziri Mkuu na Uwanja wa Ndege wa Al-Muthanna.

Kwa hayo yaliyotangulia, ni dhahiri kuwa hakuna jipya, tungali tunawaona watu wale wale waliotawala ulingo wa siasa tangu 2003 na kugubikwa na ufisadi, kuua watu wasio na hatia na kuiba mali ya nchi, hasa kwa kimya cha kiongozi wa vuguvugu la Sadri, ambaye alikuwa akimpinga vikali Muhammad Shia'a al-Sudani kuwa waziri mkuu. Kwa hivyo, sasa tunakabiliwa na mandhari tatu: Ima kumridhisha al-Sadr kwa badali ya viti vikuu vya uwaziri, au kukoleza moto na kurudi kwa wafuasi wake barabarani hata bila yeye kutangaza hilo, au muungano wa al-Sadr pamoja na miungano mingine katika upinzani, ambayo itadhoofisha dori ya serikali, na kupelekea uchaguzi mwingine wa mapema.

Enyi Waislamu nchini Iraq:

Mateso na majanga yenu hayawezi kumalizwa kupitia kuunda serikali kutoka chama chochote, maadamu mfumo huu fisadi wa kidemokrasia ambao raisi wa nchi ameapa kuudumisha ungalipo, na maadamu munatawaliwa na katiba iliyotungwa na mvamizi ambaye amefunga shingo zenu na wanasiasa hao fisadi ambao hawazingatii kwenu mkataba wowote ya udugu wala ahadi ya ulinzi.

Basi waacheni wagombanie madaraka na kuumana wao kwa wao. Imarisheni utashi wenu na muungane kufanya kazi ya mabadiliko msingi, kung'oa mfumo fisadi na mabwana na wasaidizi wake, na fanyeni kazi katika kusimamisha mfumo unaotokana na imani yenu, mfumo ambao Mwenyezi Mungu ameukubali kwenu na ambao ndani yake mna hadhi na heshima yenu; mfumo wa Khilafah kwa njia ya Utume:

(لَقَدْ أَنْزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَاباً فِيهِ ذِكْرُكُمْ أَفَلا تَعْقِلُونَ)  

“Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?” [Al-Anbya: 21-10].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu