Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  18 Shawwal 1445 Na: 22 / H 1445
M.  Jumamosi, 27 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Hasina Yamfanya Aliyekuwa Jenerali Mkuu wa Polisi Benazir Ahmed Mtuhumiwa wa 'Kuziba' Ufisadi Mkuu wa baadhi ya ‘Vigogo wa Kisiasa’ wa Chama chake na Mabepari

(Imetafsiriwa)

Mkuu wa zamani wa majambazi wa serikali ya Hasina na mkuu wa gege la wakora la polisi na vikosi vya RAB - Benazir Ahmed na utajiri wa familia yake wenye thamani ya maelfu ya crore za Taka umechapishwa kwenye vyombo vya habari. Wananchi kamwe hawakushangazwa kujua utajiri wake; Badala yake, watu wanashangaa ni kwa sababu gani wakati huu serikali ya Hasina imemfanya mtumwa wake mwaminifu kuwa mtuhumiwa. Kwa kweli, Hasina - 'taji' la mafisadi na waporaji - mara kwa mara amegundua aina hii ya watumwa kwa miaka mingi ili 'kuziba' ufisadi mkuu wa baadhi ya vigogo wa kisiasa wa serikali yake na mabepari. Kwa baraka za mfumo huu wa kisekula uliooza, wameachwa huru kutokana na vita vya kisheria na wanafurahiya utajiri huu haramu. Kukamatwa kwa 'Casino Samrat' na 'Sahed Gong', kuzuiliwa kwa akaunti 617 za benki za MP Papul, mkewe na binti yake, nk, ni baadhi ya mifano ya michezo duni kama hiyo, ambayo serikali ya Hasina imeendeleza sana kuficha sura ya kweli ya ufisadi wake na kujifanya kuwa serikali haiwasazi hata kama ni wanachama fisadi wa chama au waaminifu.

Watu wanajua vizuri kuwa serikali ya Hasina imeubebesha mzigo umma kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia kuchapisha maelfu ya crone za taka kufadhili majambazi wa mabenki na imechukua hatua za kuunganisha benki zengine ili kuzilinda. Wizi huu wa kidijitali wa 'Prince' Sajeev Joy na ufisadi wa dolari bilioni 62 ndio gumzo la mji mitandao kijamii, lakini bado kungali hakuna jibu. Jina la Aziz Khan, mkuu wa kikundi ‘kidogo’ cha mkutano, limeibuka kwenye orodha ya mabilionea wakubwa wa Singapore kwa uporaji mkubwa wa sekta ya umeme na nishati wakati wa serikali ya Hasina, akiwa na angalau dolari bilioni 1.12 katika mali nchini Singapore, kulingana na Forbes. Licha ya habari za wizi wa mabenki na ulanguzi wa angalau dolari bilioni 1 kwenda Singapore dhidi ya S. Alam, kijana wa wizi wa wizi wa mabenki wa nchi hiyo, anayejulikana kama mshika fedha wa familia ya Sheikh, Chemba ya Mahakama ya Upeo ya Kisekula ilisimamishwa Uchunguzi wa S. Alam na kutoa agizo. Na wale ambao majina yao yapo kwenye nyaraka za Panama na Ripoti ya Benki ya Swiss hawagusiki. Mifano hii ya ufisadi wa kimfumo ni 'michache tu lakini sio ya mwisho'. Uhalisia ni kwamba ufisadi ni sehemu muhimu ya mfumo uliopo wa kisekula usio thamini Mungu na kiwanda cha watawala mafisadi na mabepari. Kwa sababu maadili haya yanawafanya watu kupagawa juu ya kupata manufaa makubwa zaidi za kidunia na kugeuza fikra zao kutoka kwa siku ya hukumu ya Akhera, yaani ‘Ulimwengu ni mkubwa, kula na ushibe!' Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ * حَتَّى زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ]

“Kumekushughulisheni kutafuta wingi. Mpaka mje makaburini!” [At-Takasur: 1-2].

Enyi watu, njia pekee ya kutokana na hali hii ni kung’oa fikra ya kisekula kutoka kwa jamii na kurudisha mfumo wa Khilafah. Katika Khilafah, sheria na kanuni zote zinaamuliwa kwa msingi wa maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu. Matokeo yake, hakuna mtawala anayeweza kutunga sheria za kuhalalisha uporaji wake, kwa ambavyo hawezi kumuondolea mtu adhabu na kutojali sheria kwa uhalifu wake. Pindi mwanamke mmoja kutoka kabila tukufu na lenye ushawishi la Banu Makhzum la Makka aliposhtakiwa na kupatikana na hatia ya wizi, Waislamu wengine walikuja Rasulallah (saw) na pendekezo la kutokukata mikono yake kama adhabu. Rasulallah (saw) alikasirika sana na akasema:

«أَتَشْفَعُ فِي حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللَّهِ؟ ثُمَّ قَامَ فَخَطَبَ قَالَ: يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا ضَلَّ مَنْ قَبْلَكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ وَإِذَا سَرَقَ الضَّعِيفُ فِيهِمْ أَقَامُوا عَلَيْهِ الْحَدَّ، وَايْمُ اللَّهِ لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعَ مُحَمَّدٌ يَدَهَا»

“Je, mnashufaiya katika hadd (sheria ya Mwenyezi Mungu) miongoni mwa Hudud zake? Kisha akasimama na kuhutubia akisema: Enyi watu! Hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu walikuwa anapoiba mtukufu humuacha na anapoiba mnyonge wao humsimamishia adhabu (hadd). Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Lau Fatima binti Muhammad angeiba, Muhammad angeukata mkono wake.” (Bukhari, Nasa'i na Ibn Majah).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu