Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  28 Jumada I 1441 Na: 1441 H / 012
M.  Alhamisi, 23 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tunaionya Japan Itahadhari na Matokeo ya Kuiunga mkono Serikali ya Wauaji ya Myanmar katika Mauaji yao ya Halaiki ya Warohingya, kwa kuwa Khilafah ya Uongofu inayokaribia kwa hakika italishughulikia suala hili kwa umakinifu

Japan imeifuata India, kibaraka mwingine wa washambuliaji wa Kimagharibi, kwa kuiunga mkono serikali ya Myanmar kuhusiana na Mauaji ya halaiki ya Waislamu Warohingya. Balozi wa Japan nchini Myanmar, Ichiro Maruyama, bila aibu alisema siku chache zilizopita katika mkutano na waandishi wa habari kuwa hakukuwa na mauaji ya halaiki nchini Myanmar, badala yake ni ‘msako wa kupambana na ugaidi’ dhidi ya shirika la Kijihad la ‘Arakan Rohingya Salvation Army’ (Reuters, Januari, 15, 2020)! Hesabu za kutisha za kuenea ubakaji, mauaji ya watu wengi na kuviteketeza vijiji vyote, na ukimbizi wa Warohingya 740,000 ndani ya Bangladesh yote yametupiliwa mbali na Japan kwa sababu ya njama za kupambana na ugaidi zinazopigiwa debe ulimwenguni na Masalabiyina wa Kimagharibi. Kwa kweli, msimamo rasmi wa Japan kuhusiana na mauaji ya halaiki ya Warohingya sio ‘kupinga’ hasa, badala yake ‘wanaidhinisha’ mauaji ya jumla ya Waislamu Warohingya ili kuingiliana na ‘vita dhidi ya Uislamu’ vinavyoongozwa na Amerika. Inasikitisha sana kuwa Japan imesahau uhusiano wa karibu iliyokuwa nao na Khilafah ya Uthmaniya wakati wa Sultan Abdul Hamid Khan na mfalme wao maarufu Meiji aliyeibadilisha Japan kutoka jimbo la kujitenga na kuwa nguvu ya kiviwanda ulimwenguni. Tofauti na Mtawala Meiji aliyekuwa kiongozi mwenye maono na mwenye shauku kubwa juu ya Uislamu, tangu kushindwa Japan na Amerika, watawala watiifu wa Japan wamekuwa wakiishusha nchi yao kwa kufuata kiupofu njia ya uongo na udanganyifu mkubwa ya Amerika. Kwa hivyo, tumewaona wao wakipeleka majeshi yao kwenye vita vya Amerika kwenda Afghanistan ambavyo msingi wake ni uongo. Na sasa, twaiona serikali ya Japan bila aibu inahalalisha mauaji ya Waislamu kwa kisingizio cha kupigana na kinachojulikana kama ‘Ugaidi wa Kiislamu’.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, inataka kutuma ujumbe mkali kwa Japan kuwa haifai kuunga mkono ukatili dhidi ya Waislamu Warohingya. Hata ingawa kwa sasa ni madhaifu na wanakandamizwa kwa sababu ya usaliti na kutokuwa na uwezo kwa watawala wa serikali ya taifa letu, udhaifu huu utamalizika kama mlezi na mlinzi wao wa kweli, Khilafah ya Uongofu ya pili kwa njia ya Utume, inakaribia kusimamishwa tena kwa matakwa yake Mwenyezi Mungu (swt) karibuni. Dola ya Khilafah inayokaribia hakika itaishughulikia ipasavyo Myanmar kwa dhuluma ambazo inawafanyia Ummah wetu mpendwa, na pia itazihesabu zile nchi ambazo ziliunga mkono nchi hii yenye vita vya chuki. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie alisema:

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imamu ni ngao watu hupigana nyuma yake na hutaka hifadhi kwake.” [Muslim]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu