Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  27 Safar 1444 Na: 1444 H / 07
M.  Ijumaa, 23 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir/ Wilayah Bangladesh Maandamano dhidi ya kile kinachoitwa Sera ya Kujizuia ya Serikali ya Hasina juu ya Mashambulizi ya Makombora na Mauaji ya Mwezi Mzima yaliyofanywa na Myanmar katika Mpaka wa Bangladesh

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir/ Wilayah Bangladesh leo (23/09/2022) siku ya Ijumaa baada ya Swala ya Ijumaa iliandaa mikutano ya hadhara katika majengo ya misikiti tofauti tofauti ya miji ya Dhaka na Chittagong kupinga kile kinachoitwa sera ya serikali ya kujizuia dhidi ya kuendelea kwa mashambulizi ya makombora na mauaji ya Myanmar kwenye mpaka wa Bangladesh. Ifuatayo ni sehemu kuu ya hotuba za wazungumzaji katika mikutano hiyo ya hadhara:

Enyi Watu! Usiku wa Septemba 9, kombora lililorushwa na jeshi la Myanmar lilimuua kijana wa Rohingya aitwaye Iqbal (17). Mapema siku hiyo hiyo saa sita mchana, mguu wa kijana wa Bangladesh ulilipuliwa na mlipuko wa mgodi katika eneo lililo kati ya nchi mbili linalopakana na Tumbru. Lakini inasikitisha sana kwamba ingawa ubwana wa nchi hii unatishiwa na uchokozi na ufyatuaji risasi wa mwezi mzima wa Myanmar ndani ya Bangladesh, utawala huo wa kihaini haujaonyesha hisia kali kwao, achilia mbali kupinga hali hiyo dhaifu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini uliutaja kama mzozo wa kindani wa Myanmar ndani ya mpaka wao na kutaka uingiliaji kati wa Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa. Serikali ya Hasina imeonyesha sura yake mbaya huko nyuma kwa kuwatelekeza Waislamu wa Rohingya na kuunga mkono jeshi la Myanmar linalochinja kinyama. Waislamu wa Rohingya walipokimbia moto wa Myanmar na kukimbilia Bangladesh, serikali ya kihaini ya Hasina "iliwafunga" wakimbizi wa Rohingya na kutoa 'usalama' kwa jeshi la Myanmar ili wasiwe tishio lolote kwa Myanmar! Si hivyo tu, walivunjia heshima jeshi letu la Kiislamu kwa kuwatuma kupanga paredi nchini Myanmar pamoja na jeshi la kikafiri la mauaji ya halaiki. Kwa hivyo hata Jeshi la Myanmar livamie mpaka wa Bangladesh kiasi gani, Sheikh Hasina kamwe hatachukua misimamo mikali dhidi yao kwa sababu Hasina na jeshi la junta la Myanmar wote wanadumisha utiifu wao kwa bwana wao wa kikoloni Uingereza, wakitumikia si chengine ila maslahi ya kijiografia ya bwana wake ambaye daima amekuwa ikiunga mkono utawala wa kijeshi wa Myanmar dhidi ya uingiliaji wa Marekani kupitia Aung San Suu Kyi. Kwa hivyo Hasina ametoa ushahidi mbele ya Mkuu wa Chama cha Labour Keir Starmer jijini London mnamo Jumamosi kwamba anatumikia maslahi ya kikanda ya bwana wake kwa kuilinda serikali ya Myanmar. Alimwambia kwamba Bangladesh inatekeleza ‘kijizuia kikamilifu’ licha ya athari za kuenea kwa mizozo ndani ya eneo lake (“PM Hasina: Bangladesh is exercising restraint over Myanmar border tension”, Dhaka Tribune, 17 September 2022). Mfano wa kile kinachoitwa kujizuia kwa serikali ya Hasina ni kwamba hakuna hatua madhubuti zilizowekwa dhidi ya jeshi la Myanmar mpakani, badala yake vituo vya uchunguzi vya SSC vimeondolewa katika maeneo karibu na mpaka.

Kwa upande mwingine, kile kinachoitwa maslahi ya wakoloni wa Amerika katika mauaji ya halaiki ya Rohingya na kuwaregesha makwao hakiko nje ya maslahi yake ya kijiografia na kisiasa. Vikwazo dhidi ya jeshi la Myanmar na Marekani kamwe havikutokana na chembe chembe za huruma kwa wakimbizi wa Rohingya, bali kama njama ya kutumia masaibu ya Waislamu wa Rohingya kutoa shinikizo kwa utawala wa kijeshi wa Myanmar. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony J. Blinken hivi karibuni alisema kuwa serikali yake inajitahidi kuongeza kwa kiasi kikubwa makaazi mapya ya wakimbizi wa Rohingya kutoka Bangladesh. Kwa hivyo Marekani inajaribu kuweka hai suala la wakimbizi wa Rohingya ili iweze kuweka shinikizo kwa utawala wa kijeshi wa Myanmar unaoungwa mkono na Uingereza. Cha kusikitisha ni kwamba Waislamu wa Rohingya wanaoteswa wamekuwa wahanga wanaochukiwa wa mzozo wa kijiografia wa mkoloni kafiri Uingereza-Marekani. Hata BNP haina ujasiri wa kuchukua msimamo mkali dhidi ya mauaji ya halaiki ya Rohingya nchini Myanmar au uingiliaji wa kijeshi wa jeshi la Myanmar kwenye mpaka wa Bangladesh kwa sababu mithili ya sheikh Hasina, wao pia wanafanya siasa za utumwa. Kwa hivyo, kama chama tawala, BNP pia inataka uingiliaji kati wa Umoja wa Mataifa na ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa kutatua mgogoro wa Rohingya kwa kuzingatia maslahi ya Marekani. Hii ni kama kumuomba mbwa mwitu kuwalinda kondoo! Tutarajie nini zaidi kutoka kwa watawala hawa wa kisekula wasaliti ambao daima wamejitolea kulinda maslahi ya kijiografia ya wakoloni wao Marekani-Uingereza kwa gharama ya Waislamu wa Rohingya wanaodhulumiwa na maslahi ya nchi!

Enyi Watu! Waislamu wa Rohingya ni kaka na dada zetu, na hatuwezi kuwaangusha kutokana na ugumba wa watawala watumwa wa kisekula. Mtume (saw) amesema, «الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لاَ يَظْلِمُهُ وَلاَ يُسْلِمُهُ» “Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwengine, hamdhulumu, wala hamsalimishi (kwa adui)” (Bukhari na Muslim). Tunahitaji kuukataa uongozi huu wa kitumwa wa kisekula na kujitahidi kuiregesha Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itatabanni maslahi ya kweli ya Waislamu wa Rohingya na kuliregesha Jimbo la Arakan chini ya kivuli cha Khilafah ili kuwapa ulinzi na hifadhi.

Enyi Maafisa Wanyofu wa Kijeshi! Nyinyi ndio kimbilio la mwisho la ubwana wa Ummah. Mwenyezi Mungu (swt) anakuamuruni:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُمْ مِنْ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ]

“Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mungu.” [Surah At-Tawbah: 123]. Na Umma wa Kiislamu unajua kwamba nyinyi pia muko tayari kutii amri hii ya Mwenyezi Mungu kwa kutoa jibu linalofaa kwa jeshi oga la Myanmar. Wakati utawala huu kibaraka unakutengenezeeni vikwazo vya nyinyi kufuata amri hii ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kukuwekeni kifungoni ndani ya kambi ili kulinda maslahi ya makafiri. Kwa hivyo munapaswa kuvishinda vizuizi hivi kwa kuwaondoa watawala wa sasa vibaraka wa kisekula. Hizb ut Tahrir inakulinganieni, toeni nusrah (msaada wa kimada) kwa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha Khilafah - dola ya Khilafah itakupeni fursa ya kutimiza agizo hili la Mwenyezi Mungu (swt) kupitia kukupelekeni kwenye mpaka wa Myanmar kwa ajili ya operesheni za kijeshi, ambapo kwazo ubwana wa Umma wa Kiislamu itahakikishwa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu