Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  11 Muharram 1444 Na: 1444 H / 01
M.  Jumanne, 09 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kupanda Huku Kikatili kwa Bei ya Mafuta ni Laana ya IMF na Mfumo Uliooza wa Kirasilimali

(Imetafsiriwa)

Wakati watu wa kawaida tayari wanapambana na kupanda kwa bei ya bidhaa za kila siku na gharama kubwa ya maisha, serikali ya Hasina, iliyozama katika ufisadi, ilitia chumvi kwenye vidonda vyao kwa kupandisha bei ya mafuta kwa hadi asilimia 51.7 ya kushtua mnamo Ijumaa usiku. Lita moja ya octane sasa inagharimu taka 135 (USD 1.43) ambayo hapo awali ilikuwa Taka 89. Bei ya petroli pia imeongezwa hadi Taka 130 (US$ 1.37) kutoka Taka 86 na bei ya dizeli na mafuta ya taa imeongezeka kutoka Taka 80 hadi Taka 114. Ili kutekeleza agizo la IMF la kuondoa kile kinachoitwa ruzuku za mafuta kwa ajili ya kupokea kifurushi chao cha uokoazi cha dolari bilioni 4.5, serikali hii ya kisekula inajificha nyuma ya uongo na udanganyifu. Wamepandisha bei kwa hasira wakitaja mtindo wa kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa, wakati bei ya mafuta imeshuka katika soko la kiulimwengu katika wiki za hivi karibuni huku hofu ya kushuka kwa uchumi ikiongezeka.

Zaidi ya hayo, mnamo Julai 27, Sheikh Hasina alidai kwa kiburi kwamba Bangladesh haiagizi petroli na octane kutoka nje kwa kuwa nchi hiyo inazipata hizi kama bidhaa pembeni zinazotokana na uchimbaji wa gesi. Wiki moja tu baada ya dai hili, serikali yake yenye kudanganya iliongeza bei ya bidhaa hizi mbili pia! Ukweli ni kwamba Shirika la Petroli la Bangladesh (BPC) lilipata faida ya Taka bilioni 48.119 tangu mwaka wa fedha wa 2014-15 kwa kuuza mafuta kwa watumiaji kwa bei ya juu kuliko soko la kiulimwengu. Na serikali shirikishi ya kirasilimali ya Hasina ilitumia faida hizi katika miradi yao mbalimbali ya uporaji mkubwa. Mawaziri wake wasio na haya pia hawakuweza kukataa ukweli huu ("Faida ya BPC iliyotumiwa kwenye miradi ya dev, Madai Nasrul Hamid", The Daily Star, Aug 7, 2022). Ili kufadhili uporaji wao kwa jina la maendeleo, sasa wananyonya damu ya watu kupitia kupandisha bei ya mafuta. Sasa sekta ya nishati, uchukuzi na kilimo itaathirika zaidi kwa sababu ya utegemezi wake mkubwa wa matumizi ya dizeli na mafuta ya taa. Haya yatasababisha gharama ya maisha kwa jumla, na kuongeza masaibu ya watu maskini na watu na tabaka la kati.

Taasisi mashuhuri hatari ya kirasilimali IMF daima huchukua fursa ya kulazimisha ajenda ya wakoloni na sera ya kibepari ya ubinafsishaji iliyo ulemaza uchumi wetu, haswa sekta yetu ya nishati. Kwa kufuata sera ya IMF, tawala zote za kisekula mtawalia kamwe hazikuwekeza katika usimamizi wa nishati ya serikali (BAPEX) na kuruhusu makampuni ya kigeni ya wakoloni kama vile Chevron, ConocoPhillips nk. kupora madini yetu ya gesi na mafuta chini ya mkataba wa Uzalishaji shirika (PSC). Waliikabidhi sekta ya uzalishaji umeme kwa makampuni ya kigeni yenye ulafi (kama vile Palli Biddut inayomilikiwa na kampuni ya Marekani) na makampuni ya ndani (kama vile Summit Group). Zamani wakoloni wangevamia ardhi hizo kwa ajili ya kutafuta maliasili na madini. Lakini sasa katika ‘ulimwengu huru’ wa leo, taasisi kama vile IMF na WB wakishirikiana na watawala vibaraka wasaliti hupora rasilimali za nchi na kulemaza ubwana wao wa nishati ili waendelee kuwa tegemezi kwa huruma ya makafiri. Kwa hivyo, tunaona kwamba kipote cha mabwenyenye na watawala wafisadi wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi wanajinufaisha katika sekta ya nishati kupitia mpango muovu wa ubinafsishaji wa IMF ambapo watu wa kawaida wanachukua ushuru wa bei ya mafuta inayoongezeka daima. Kwa hivyo, kwa kawaida, IMF haiishinikizi serikali kuacha kutoa ‘bima ya umeme’ kwa kipote cha Mabepari, bali inalazimisha kuondoa kile kinachoitwa ruzuku kwenye mafuta ambayo hufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa raia. Watawala vibaraka wa wakoloni wamevuka mipaka yao yote. Wanafuata kwa uaminifu maagizo ya mabwana zao bila kujali mateso ya watu. Idadi yote ya watu imefanywa kuwa mateka mikononi mwa viongozi hawa katili na mfumo wao dhalimu wa Kirasilimali. Ni wakati sasa wa kuvunjwa na pingu hizi za ukandamizaji unaoungwa mkono na nchi za Magharibi.

Enyi Watu, ni lazima mulinganie kuanzishwa tena kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume iliyoahidiwa kwa sababu ni Khilafah pekee ndiyo inayoweza kuwatoa watu katika masaibu haya. Khilafah haitakuwa na haja ya kutoa ruzuku sekta ya nishati kwa vile nishati na madini ziko katika kundi la ‘mali ya umma’ chini ya Uislamu; watu watazipata hizi moja kwa moja kwa gharama ya chini au bila malipo. Kimaumbile, hakutakuwa na nafasi ya ubinafsishaji wa rasilimali hizi ili kuhakikisha faida kubwa kwa matajiri kupitia uporaji wa pesa za watu. Khilafah, kutokana na matarajio yake ya kuwa dola kuu yenye nguvu duniani, itachukua hatua za kujitegemea kwa nguvu na nishati kupitia mpango wa haraka wa kukuuza uwezo. Kwa kutumia nishati na nguvu, Khilafah italenga katika kujitegemea kutengeneza mitambo na injini za kilimo, ujenzi, viwanda na majeshi.

Itapangilia uchumi wake kulingana na maagizo ya Sharia na haitaruhusu wakoloni au taasisi zao kama IMF, Benki ya Dunia kuingilia kati maswala ya kiuchumi ya Dola hii. Khalifah kamwe hatazigeukia taasisi hizi za kibeberu kwa ajili ya kuziomba usaidizi kwa sababu Khilafah kamwe haitatoa nafasi kwa mfumo wa fedha wa dolari usio na thamani ya kidhati. Uchumi utategemea bidhaa na huduma halisi na sarafu itategemezwa na dhahabu na fedha. Kwa hivyo, hakutakuwa na mfumko wa bei kama huo au kuongezeka kwa ghafla kwa bei ya vitu muhimu.

Mfumo wa Kirasilimali umetufikisha kwenye ukingo wa maangamivu, umetufanya tuwe na deni kwa dola za Kimagharibi na kuleta mateso kwa watu. Lakini ikiwa hatutamtegemei yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt), Yeye (swt) anaahidi kututengenezea njia ya kutoka katika matatizo haya:

(فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى)  

“basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.” [Taha: 123].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu